Tanzania: Energy Efficiency in Buildings | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Energy Efficiency in Buildings

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by TUJITEGEMEE, Feb 27, 2012.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Sina hakika kama hili lilishawasilishwa hapa.

  Katika siku za hivi karibuni nilivutiwa na matangazo ya televisheni yaliyodhaminiwana TANESCO juu ya matumizi bora ya nishati ya umeme kwa kutumia vifaa vya umeme vya majumbani vyenye ufanisi bora. Pia yapo matangazo mengine yanayohimiza utumiajia wa vifaa vya aina hiyo kutoka kwa makampuni mbalimbali. Najua lengo ni kuhimiza matumizi bora ya nishati ya umeme.

  Binafsi naona kampeni hii ingesogea mbele zaidi kwa designer/'architectures' wetu wa majengo marefu hapa nchini. Kumekuwa na majengo marefu hapa nchini ambayo hayazingatii suala la matumizi makini ya nishati ya umeme. Jengo utakuta limebandikwa vioo kuta karibu zote jambo linaloongeza joto ndani wakati wa jua (green house effect) kiasi kwamba inalazimika kuwasha AC(air conditioners) kutwa nzima, wakati jengo lingesanifiwa kwa kufuata utaratibu wa kutumia 'natural ventilation' (mfano soko la KariaKoo), nina imani gharama kubwa zinazotumika kuwasha AC kutwa nzima zingepungua, hivyo kuiwezesha TANESCO kusambaza umeme sehemu nyingine ambazo zinahitaji umeme.

  Sitaki kuamini kuwa designer/'architectures' wetu hawajui madhara ya kutusanifia majengo yanayo sababisha 'green house effect'.

  Nawasilisha!
   
 2. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tena hivi vioo vinaongeza joto hata nje ya jengo lenyewe. Ukipita pale Quality Plaza, njia panda ya Chan'gombe wakati wa jua kali utahisi joto linaongezeka.
   
 3. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  mkuu wakati mwingine swali hili huwa najiuliza mara kwa mara kwamba, hivi wahusika wa mipango miji hawa wanopitisha vibali vya ujenzi wa majengo haya kweli hawajaligundua tatizo hili?
   
 4. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Inshu imekaa kitaalamu kidogo!! Msanifu jengo ni msanifu jengo, Lighting A/c designer ni kitu kingine kabisa. Na mlaji/mteja naye ni mwingine!
  Tukianza kwa msanifu wa jengo: Anadesign kulingana na requirements za mteja wake kwa kufuata nini mteja anataka na nini hataki kutokana na matumizi ya jengo husika na uwezo wa mteja, tukija kwa mtu wa umeme! atapewa michoro iliyokamilika kutoka kwa msanifu jengo na kila sehemu ikiwa imeshaainishwa matumizi yake na kazi yake inakuwa inaanzia hapo na kuikamilisha kutokana na uhitaji unaotakiwa.
  Sasa tukija kwenye inshu ya matumizi ya A/C, hapa ni sera za kampuni/serikali husika kuhusu matumizi ya umeme majumbani. Kuna baadhi ya nchi vitu kama A/C vinakuwa controlled na utility company mfano: wanawasha na kuzima kwa kila baada ya nusu saa au dakika 45 on, 30 minutes off, hivyo inakuwa rahisi kupunguza matumizi ya umeme yasiyo yalazima na mteja hawezi kuhisi anaonewa au kupunjwa au vinginevyo, lakini kwetu sisi hata kama ndani ilishakuwa kero, bado A/C limewashwa utadhani mtu kalazimishwa.
   
 5. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #5
  Feb 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  @ WA-UKENYENGE: Kweli kabisa ishu imekaa kitaalamu kabisa, kwa jinsi ulivyofafanua.

  Nimewalenga hasa madesigner kuhusu hili kwa sababu wao ndio wanajua kabisa kuwa bidhaa wanayomwandalia mteja ina ubora kiasi gani kwa kuzingatia matumizi ya nishati. Pamoja na matakwa ya mteja mimi nadhani designers wetu wanayonafasi ya kumshauri mteja vyema, juu ya bidhaa anayohitaji kwa manufaa ya mteja mwenyewe na afya ya uchumi wa taifa.

  Pia Bodi ya wahandisi-ERB (nikiamini iko karibu na designers wetu) inalojukumu la kuhamasisha washikadau wote katika sekta ya Ujenzi wa majengo hapa nchini namna bora ya kujenga majengo yenye ufanisi katika matumizi ya nishati ya umeme.
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Inaonyesha kuwa vinafanya kazi yake, vina reflect jua hivyo kuzuia ndani ya jengo kupata joto hii inapunguza gharama za AC.
   
 7. j

  jerecamp Member

  #7
  Feb 27, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa kuna mambo ya msingi ya kuzingatia ndugu zangu, tunaweza kufika kwenye sustainable architecture kama bodi na manispaa zetu zingeweka viwango kuwa ni nyumba inayopitishwa kujengwa inapunguza kwa asilimia ngapi matumizi ya umeme ( energy). wenzetu wana aina za nyumba wanaziita passivhaus more than 80% ni renewable energy.
   
 8. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ni kweli vinafanya kazi yake, vina reflect jua. Lakini kazi vinayoifanya ni ya kuamisha tatizo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Kwa hiyo majengo ambayo hayana reflectors za miale ya jua ambayo yako karibu na jengo hilo la vioo yatalazimika kutumia AC maradufu.
   
 9. d

  dav22 JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 1,902
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  yap hiyo ni kweli kabisa lile jengo kwa nje joto kali sana zaidi ya hata mitaani....nadhani wabongo sasa hivi hawa marchtecture wanatumia design ambazo haziko compatible na mazingira yetu maana huku kwetu joto sana so vioo sio tija sana tofauti na kule nje ambako hali ya hewa ni baridi kali so vioo vinasaidia katika kuongeza joto ndani ya jengo
   
 10. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Ni kweli, hili tatizo lipo checki hii hoteli Las Vegas inareflect jua hadi vitu vinayeyuka Las Vegas Hotel MGM Mirage Knew of Pool 'Death Ray' Back in 2008 - ABC News
   
 11. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Nadhani ile wizara inayoongozwa na Mama Prof. Tibaijuka inaweza kusaidia kupunguza tatizo hili. Ukizingatia Mama mwenyewe anaouzoefu wa kutosha kuhusu makazi endelevu na bora.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Madesa ndo nguzo ya elimu yetu ya bongo. Kwenye uhalisia kitu tunachijari ni kupunguza njaa nyumbani. Well, hata hivyo ujenzi wetu haufuati taratibu za kazi hata kidogo.
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  ERB wenyewe wamejaa Civil and Structural Engineers, hawajui kutofautisha kati ya Computer Engineer na Electrical Engineer yaani ni kazi kweli kweli. Anyway, bado tuna changamoto nyingi na bahati mbaya baada ya mradi kuisha sijui kama huwa tunarudi kuangalia kama jengo halisababishi usumbufu wowote ndani au nje tofauti na ilivyokusudiwa.
   
 14. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2014
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  RED: Ni kweli kabisa lazima hili lifanyiwe kazi
   
 15. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2014
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Mimi nilivyomuelewa mleta uzi ni kwamba ni vizuri kwavile tuna matatizo ya umeme hawa Architects wanapochora nyumba wangekuwa wanakuja na designs ambazo ni ENERGY EFFICIENT; nadhani hata wateja wao wangefurahi kama wangeshauriwa kujenga nyumba ambazo zisingetumia umeme mwingi kama kwa mfano kuwa na madirisha makubwa yanayoelekezwa jinsi upepo unavyovuma kuruhusu ventillation ambayo inaweza kupunguza matumizi ya air conditioners. Pia materials zinazotumiwa kujengea pia zinaweza kucontribute tawards efficient energy utilization.
   
Loading...