TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,297
- 28,006
Sina hakika kama hili lilishawasilishwa hapa.
Katika siku za hivi karibuni nilivutiwa na matangazo ya televisheni yaliyodhaminiwana TANESCO juu ya matumizi bora ya nishati ya umeme kwa kutumia vifaa vya umeme vya majumbani vyenye ufanisi bora. Pia yapo matangazo mengine yanayohimiza utumiajia wa vifaa vya aina hiyo kutoka kwa makampuni mbalimbali. Najua lengo ni kuhimiza matumizi bora ya nishati ya umeme.
Binafsi naona kampeni hii ingesogea mbele zaidi kwa designer/'architectures' wetu wa majengo marefu hapa nchini. Kumekuwa na majengo marefu hapa nchini ambayo hayazingatii suala la matumizi makini ya nishati ya umeme. Jengo utakuta limebandikwa vioo kuta karibu zote jambo linaloongeza joto ndani wakati wa jua (green house effect) kiasi kwamba inalazimika kuwasha AC(air conditioners) kutwa nzima, wakati jengo lingesanifiwa kwa kufuata utaratibu wa kutumia 'natural ventilation' (mfano soko la KariaKoo), nina imani gharama kubwa zinazotumika kuwasha AC kutwa nzima zingepungua, hivyo kuiwezesha TANESCO kusambaza umeme sehemu nyingine ambazo zinahitaji umeme.
Sitaki kuamini kuwa designer/'architectures' wetu hawajui madhara ya kutusanifia majengo yanayo sababisha 'green house effect'.
Nawasilisha!