Wafanya biashara wa bongo hawajiamini na wao wameweka mbele tamaa ya kupata tu, ndiyo kwa maana ukinunua bidhaa dukani ukishailipa tu umejifunga na hiyo bidhaa hata kama baada ya nusu saa utakuwa hukuipenda basi huwezi kirudisha tofauti na nchi nyengine unaweza kununua bidhaa na kuirudisha tena dukani hata baada ya siku saba ilimradi usiichafue au kuiharibu.
Maduka mengi ya bongo yanayouza vitu vya electronic hayatoi warrant kabisa, ikikutokea bahati mbaya bidhaa ikiharibika kwa fluctuations za umeme basi ndio imeisha hiyo hasara juu yako. Ipo haja ya serikali kuunda chombo cha kumsimamia mlaji na kukataza hizi risiti zinazokataza kurudisha bidhaa dukani hata kama umeuziwa ikiwa mbovu.