Tanzania Construction Bank

keyonce

Member
Jul 29, 2015
14
22
Hivi ni kwanini serikali yetu hii ya Tanzania isitufungulie watanzania bank ya wakandarasi tu, iwepo kwa ajili ya kufinance miradi wanayopata wakandarasi.
pale mkandarasasi anapopata mradi anakuwa na uhakika wa kupata finance kutoka kwenye hiyo benki ya wakandarasi wa kitanzania kwa kutumia hiyo contract tu ya mradi aliyopata.

hii itasaidia kuinua uchumi wa Tanzania na itawapa watu wengi fursa ya kujiajili katika hiyo sekta na vile vile itasaidia wakandarasi wa kitanzania kupanua wigo hata kwenye nchi za wengine katika hiyo sekta. vile vile itatuwezesha wakandarasi wa kitanzania kufanya miradi mikubwa ambayo hupewa kampuni kutoka nje.

Naomba Serikali waliangalie hili suala la kutufungulia Watanzania Benki kwa ajili ya wakandarasi.
 
Wachache watakaokuelewa,kampuni nyingi za ndani za Ukandarasi hushindwa kupata project za maana kutokana na Mitaji lakini kama Serikali na Wataalamu wa Uchumi wataliona hili linaweza kuwa jibu sahihi kwa kampuni za ndani na ukuaji wa Uchumi,linafaida nyingi.

Hata kama kusiwepo na Bank hii lakini pia kampuni ziruhusiwe kupata mkopo kwa kutumia Contract katika bank zetu hizi za ndani.
 
serikali inawaza kuanzisha benki ya wanawake ila wakandarasi wangefanya kama walimu waanzishe benki yao vinginevyo watakuwa wanaaona watu toka nje wanachukua pesa wao wanabaaki wakihangaika
 
ni wazo zuri, lakini kuna baadhi ya wakandarasi wakipewa advance payment wanaingia mitini hutawaona tena. hilo ili lifanikiwa kila mkandarasi atahitaji kijidhamini si kwamba mkataba ndo uwe dhamana
 
Wazo zuri sana,hiyo bank itatusaidia sana sisi wakandarasi wazawa,litainua hali zetu kichumi kwa kiasi kikubwa,itatufanya tuaminike na kupata miradi mikubwa,itasaidia sana kukuza ajira ktk sekta hii kwani sekta hii inaajiri watu wengi sana lkn pia ni vema kuzingatia namna bora ya kuanzisha bank ya wakandarasi na hao wakandarasi wakanunua shares na wakatozwa riba kdg
 
TIB, inafanya hiyo kazi tayar,

Tatizo makampuni mengi yanafanya kazi kiujanja janja, hayana cash flow nzuri,mali za kuaminika wala wataalam wakuaminika!

Wataalam wao wanahamhama sana, na mitambo ni full kukodisha ndo maana hawaend benk wala hawapati kazi kubwa kubwa
 
Back
Top Bottom