Sidhani kama Kenya inaweza kuifundisha Tanzania jinsi ya kutafuta pesa na kuzitumia vizuri, badala yake ni kwamba Tanzania ndio inapaswa kuwafundisha wakenya jinsi ya "Financial management'.
Tatizo la hizo nchi ulizozitaja, hasa kwa Kenya sio Eurobond wala kukopa pesa, tatizo ni uwezo mdogo wa Kenya katika kupanga matumizi ya miradi yenye kuleta faida na usimamizi wa miradi kutokana na uwezo mdogo, ukabila, rushwa na upendeleo.
Hakuna mchumi yeyote nje ya serikali ya Jubilee aliyekubaliana na ujenzi wa SGR ya Kenya kutoka mwanzo, watu wenye akili walisema waziwazi kwamba huu mradi hauna faida kwa Kenya, gharama zake zipo juu sana hivyo hakuna sababu ya kujengwa kwa sasa.
Nani asiyejua kwamba Lamu Port pia haiwezi kuleta faida kwa Kenya, nani asiyejua kwamba baadhi ya viwanja vya ndege vilijengwa kama ISiolo lakini ni hasara kwa Kenya, nani asiyejua kwamba Kenya inataka kujenga bomba la mafuta toka Lokachiar hadi Lamu ambalo halina faida kwa Serikali?
Miradi kama hii hata ukipewa mikopo bila interest haiwezi kurudisha hiyo pesa. Wacha kulaumu Eurobonds, tatizo ni uwezo mdogo wa viongozi wenu katika kupanga vipaumbele vya nchi na matumizi mazuri ya Fedha.