Tanzania: Cement sh 5,000 yawezekana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania: Cement sh 5,000 yawezekana!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BONGOLALA, Oct 27, 2010.

 1. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,395
  Trophy Points: 280
  Eti wataalamu wa cement wameohojiwa leo itv na tbc1 kuhusu bei ya cement kuwa sh 5,000 haiwezekani kutokana na gharama ya usafirishaji kuwa kubwa!

  Wana JF, nauliza mbona bei ya soda huwa karibu sawa tz nzima? Maana Tanga, Mbeya na Dar kuna viwanda vya cement.

  Okey, Dar, Mbeya, Mwanza na Moshi kuna viwanda vya soda. Je, utofauti au uwiano wa bei ya soda na cement kwanini utofautiane Mtwara, Kigoma, Rukwa?

  Ninavyojua distributor hupewa bei tofauti kutegemea umbali.

  Pili wamesahau hatuna reli ndio maana hatujui bidhaa zinagharama gani kusafirisha. Pia Libya huweka ruzuku ktk bei ya bidhaa kitu ambacho Dr Slaa pia atakifanya. Inakuaje cement itoke Pakistan iwe bei chini kuliko yetu? Jibu ni technology yetu hafifu!

  Cha kushangaza hawa wawekezaji wa viwanda vya cement ni kampuni tofauti lakini hukaa Sea Cliff pamoja kesho yake bei inapanda kwa Twiga, Tembo na Simba cement; inakuaje na wakati kiwanda cha Twiga walisema bei itashuka kwakuwa wanatumia gesi ya Songosongo?
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tujimwage kwa wingi tarehe 31 mkuu cement ishuke...Kila kona mafisadi tanzania ndugu yangu...NAMNUKUU CHIZI MMOJA ANAITWA CHILIGATI alisema tumechoshwa na wanaobeba vijimfuko vimojavimoja vya cement, aliwwaambia wananchi wa KIGAMBONI kuhusu sakata la kuhamishwa kupisha mji mpya...
   
 3. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Kwa mtu yeyote mwenye akili huwezi kwenda kumwuluza mwekezaji eti Gharama ya kuzalisha mfuko wa cement ni sh. ngapi au kumwuliza eti kama gharama ya cement inaweza kushuka. Hata ningekuwa mimi mwekezaji lazima nitakwambia haiwezi kushuka kwani ni nani asiyetaka faida.

  Lakini kama Dr Slaa alivyo sema Tanzania hakuna tena utaifa. Yaani mwekezaji ndo anasikilizwa zaidi kuliko serikali. Serikali ikiamua tena ikatoa na ruzuku kwanini gharama isishuke? Ingekuwa enzi za Nyerere mwandishi wa habari angewekwa ndani kwanza ili ashike adabu.

  Ni ujuha kumsikiliza mwekezaji ili akupangie bei. Ni mawazo mgando bacause s/he is there for profit only. So they can do and say anything inorder tomake more profit for them. TBC na huyo mtangazaji walinishangaza kweli, unamfuata mwekezaji kumwuliza swali kama hilo. Sijui uwezo wao wa kuelewa na kuchanganua mambo hukoje! Jambo la aibu kabisa.

  Nazidi kushawishika kumchagua Dr Slaa.
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ngoja wasubiri 31 October ndio watajua kuwa inawezekana
   
 5. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mkuu apa umemaliza kila kitu.

  Ivi kweli mwandishi wa ktv, citzentv wanaweza kuwa **** vile??

  Bila aibu anampamba kwa kumuita mtaalamu wa kimataifa.
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kumbe kiwandani inawezekana, ndo alichosema slaa kwa bei ya kiwandani usafirishaji ni kitu kingine, mbona mbeya wanakiwanda cha tembo na bado bei ipo juuu! Hawa watu vipi????
   
 7. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  kistajabu ya musa , utayaona ya filauni
   
Loading...