Elections 2010 Tanzania Bila Makamu wa Rais!

Hii imekaaje??? Kutoka kwenye katiba yetu ibara ya 38 (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, kiti cha
Rais kitakuwa ki wazi, na uchaguzi wa Rais utafanyika au nafasi
hiyo itajazwa vinginevyo kwa mujibu wa Katiba hii, kadri
itakavyokuwa, kila mara litokeapo lolote kati ya mambo
yafuatayo:-
(a) baada ya Bunge kuvunjwa;

Unajua kwa nini wamesema "Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii," unajua kuna masharti gani mengine?

Kikatiba Kikwete ni Rais na Shein ni Makamu mpaka hapo Kikwete na Bilal watakapoapishwa .
 
Jamani tuache porojo,

Hebu tuombe wanaojua watuelezee, tuwe makini kidogo kwenye kulijadili hili tuache jokes........
 
Kwa nini unafikiri Shein si Makamu wa Rais?

Technically Shein ni Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar, hiki si kitu kipya, kina Jumbe na Mwinyi washakalia hivi vyeo pamoja kwa miaka.
Soma hii imetoka ibara ya 50 ya katiba yetu :: (2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-
(a) muda wake utakapokwisha;
(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;
(c) atakapojiuzulu;
(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Rais
kuwa wazi;
 
Kwa hiyo kiapo kile kinasema mtu hawezi kuwa makamu wa rais wa Tanzania bara? hebu tupe sehemu ya kiapo inayosema hivyo.

Alikuwa Makamu kwa sababu ya kiapo alichokula 2005...sasa kala kipya 2010 kile cha zamani kimekufa...na ana ADC kwa sasa...huwezi kuwa makamu ukawa na hisi sifa
 
Jamani tuache porojo,

Hebu tuombe wanaojua watuelezee, tuwe makini kidogo kwenye kulijadili hili tuache jokes........

Hakuna sehemu yoyote katika katiba inayosema rais wa Zanzibar hawezi kuwa makamu wa rais, kama ipo nielimisheni.

Katiba inasema rais, na makamu wake by inference, wataendelea kushika vyeo hivyo mpaka rais mteule na makamu wa rais mteule watakapoapishwa.

Kwa hiyo sasa hivi Shein ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa sababu Makamu wa Rais mpya bado hajaapishwa, na pia ni rais wa Zanzibar kwa sababu kachaguliwa.
 
kwani nchi hii hata ina rais au!!???

We acha utoto. hata kama rais aliyemadarakani humpendi, wengine walimchagua na wanampenda. Ndiyo maana hakupata kura asilimia 100. Inaonekana hujapata elimu ya kujitambua wewe.
U better b thinking twice, b4 u say something about somebody.
Huyo Kikwete unayemdharau anauwezo wa kuifunga hii JF kesho. Ila kwa kuwa anajua watu kama nyie mpo ndo maana ameacha freedom of expression kama hizi.

Expand ur horizon.
 
Soma hii imetoka ibara ya 50 ya katiba yetu :: (2) Makamu wa Rais atashika kiti hicho hadi-
(a) muda wake utakapokwisha;
(b) akifariki dunia akiwa katika madaraka;
(c) atakapojiuzulu;
(d) atakapoapishwa kuwa Rais baada ya kiti cha Rais
kuwa wazi
;

Atakapoapishwa kuwa Rais wa Zanzibar, au wa muungano ? Kimsingi, makamu wa Rais wa Muungano atakapoapishwa kuwa Rais wa Muungano (mara kiti hicho kinapobaki wazi) basi atakoma kuwa makamu wa Rais.
 
Alikuwa Makamu kwa sababu ya kiapo alichokula 2005...sasa kala kipya 2010 kile cha zamani kimekufa...na ana ADC kwa sasa...huwezi kuwa makamu ukawa na hisi sifa

Aliyekwambia kiapo cha urais wa Zanzibar "kinaua" kiapo cha umakamu wa rais nani? Umeitoa wapi hii concept? Naomba tuongee na ushahidi na tusitoe vitu hewani, katiba ninayo hapa, naomba kifungu gani hiki kinachosema hivi. Labda nitajifunza kitu kipya leo.

Huwezi hata kusema hakuna precedent, Aboud Jumbe Mwinyi pamoja na Ally Hassan Mwinyi wote wawili washawahi kushika nyadhifa za urais wa Zanzibar na umakamu wa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, sasa cha ajabu ni kipi hapa?
 
We acha utoto. hata kama rais aliyemadarakani humpendi, wengine walimchagua na wanampenda. Ndiyo maana hakupata kura asilimia 100. Inaonekana hujapata elimu ya kujitambua wewe.
U better b thinking twice, b4 u say something about somebody.
Huyo Kikwete unayemdharau anauwezo wa kuifunga hii JF kesho. Ila kwa kuwa anajua watu kama nyie mpo ndo maana ameacha freedom of expression kama hizi.

Expand ur horizon.

Du! Swahiba una hasira!!
Msamehe tu kwani maumivu ya uchakachuaji bado hayajamwisha.
 
Aliyekwambia kiapo cha urais wa Zanzibar "kinaua" kiapo cha umakamu wa rais nani? Umeitoa wapi hii concept? Naomba tuongee na ushahidi na tusitoe vitu hewani, katiba ninayo hapa, naomba kifungu gani hiki kinachosema hivi. Labda nitajifunza kitu kipya leo.

Punguza jazba kaka...utaharibu hoja zako bure...hapa twaelimishana ungekuwa mwalimu darasani si ungemaliza misitu kwa kukata fimbo?
Vitu nvingine viko so implied siyo lazima viwe kwenye hiyo katiba...msome mtoa hoja vizuri na utujulishe(kama waweza) uhalisi wa mambo...yote katika mema ya nchi yetu....ila kama wataka ngumi ni PM tukutane Gymkhana
 
Uko kote Mbali mimi najiuliza JK alienda Zenji leo kama nani?

JK bado ni rais na atabaki kuwa rais mpaka rais mpya aapishwe, na dalili zote zinaonyesha kuwa rais mpya atakuwa yeye.

Hii ni kwa mujibu wa katiba, nchi haiwezi kuwa na "power vacuum" inabidi iwe na rais wakati wote.
 
Kaka hiyo ya kufunga hii JF unatisha watu..there should be a strong reason for him to do so...the rest is betwen you guys.
 
Kwa nini unafikiri Shein si Makamu wa Rais?

Technically Shein ni Makamu wa Rais wa Muungano na Rais wa Zanzibar, hiki si kitu kipya, kina Jumbe na Mwinyi washakalia hivi vyeo pamoja kwa miaka.

Yes, Dr. Shain ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
 
Punguza jazba kaka...utaharibu hoja zako bure...hapa twaelimishana ungekuwa mwalimu darasani si ungemaliza misitu kwa kukata fimbo?
Vitu nvingine viko so implied siyo lazima viwe kwenye hiyo katiba...msome mtoa hoja vizuri na utujulishe(kama waweza) uhalisi wa mambo...yote katika mema ya nchi yetu....ila kama wataka ngumi ni PM tukutane Gymkhana

Jazba unayo wewe unayerukia mambo bila kujali katiba inasemaje.

So far tumeona, rais wa muungano na makamu wake watabaki kuwa rais na makamu mpaka rais na makamu wapya waapishwe, kwa hiyo JK ni rais wa muungano na Shein ni makamu wake bado.

Na Shein kashaapishwa kuwa rais wa Zanzibar, kitu ambacho, kinyume na wengine mnavyotaka tuamini, hakimuondolei umakamu wake wa rais katika jamhuri ya muungano.

Kwa hiyo, mpaka makamu wa rais mpya atakapoapishwa , Shein ni Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Cheo cha Makamu wa Rais, kama kile cha rais, hakitakiwi kukaa kitupu.
 
Jazba unayo wewe unayerukia mambo bila kujali katiba inasemaje.

So far tumeona, rais wa muungano na makamu wake watabaki kuwa rais na makamu mpaka rais na makamu wapya waapishwe, kwa hiyo JK ni rais wa muungano na Shein ni makamu wake bado.(weka ibara)

Na Shein kashaapishwa kuwa rais wa Zanzibar, kitu ambacho, kinyume na wengine mnavyotaka tuamini, hakimuondolei umakamu wake wa rais katika jamhuri ya muungano.(weka ibara)

Kwa hiyo, mpaka makamu wa rais mpya atakapoapishwa , Shein ni Rais wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Cheo cha Makamu wa Rais, kama kile cha rais, hakitakiwi kukaa kitupu.
(tusomee hiyo katiba ni ibara gani hii)
 
Back
Top Bottom