Tanganyika ilikuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu,na watanganyika walikuwepo chini ya tawala zao za kitemi lakini hawakuyumba.
Wakaja Wajermani baadae Waingereza Tanganyika ipo wala haikuyumba.
1954 akaja mgeni mwingine anaitwa TANU takampokea akafanya harakati zake zote hadi 1964 Tanganyika akaungana na Zanzibar akazaliwa Tanzania lakini hatukuyumba.
Mwaka 1977 TANU na ASP wakaungana akazaliwa CCM hatukuyumba.
Kati ya mwaka 1980 hadi 1985 Tanzania ilipitia kipindi kigumu kiuchumi kuliko wakati wowote ule tukaambiwa tufunge mikanda tukafunga mikanda maduka hayana kitu sukari,chunvi,sabani dawa za meno nk mpaka upange mstari almaarufu kama bidhaa adimu ,watanzania tukavumilia na nchi haikuyumba.
Mwaka 1993 Vyama vingi vikaanzishwa watabiri uchwala wakaonya tutayumba lakini wapi hatukuyumba ndio tukashuhudia kukua kwa demokrasia manyanyaso madogomadogo ya watawala yakatoweka kama moshi,kodi ya kichwa,kunyang'anywa mali kwa raia bila hiyari yao kama kuku,mbuzi,ng'ombe na michango isiyokuwa na kichwa wala miguu iliyopewa jina la kwenda kuimarisha chama ikatoweka, ingawa mali hiyo tuliyoichangia kama watanzania kama viwanja vya michezo kote mikoani vikaitwa vya CCM,na majengo na vitega uchumi vyote vilivyopatikana kabla 1993 ni mali ya wananchi wote wa Tanzania tukadhurumiwa lakini hatukuyumba.
Kama watanzania walipita katika mageuzi makubwa namna hiyo na uonevu mkubwa namna hiyo hawakuyumba,
Kwa nini leo tunaambiwa Tanzania bila CCM itayumba?
Mimi nasema nchi hata kama itaongozwa na NLD haitayumba hizo ni propaganda za wanasiasa ili waendelee kututafuna ova.