TANZANIA: Baraka na laana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANZANIA: Baraka na laana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by whizkid, Nov 22, 2011.

 1. whizkid

  whizkid JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  WanaJF,

  Abarikiwe yeyote mwenye nia au uwezo wa kuchangia kwa hali/mali/mawazo katika mambo ya msingi yenye maslahi kwa umma wa Tanzania - awe raia au mgeni, mfadhili wa nje au wa ndani, maskini au tajiri, jinsia yeyote ile bila kujali itikadi ya kisiasa, kidini wala kikabila - ni rafiki wa haki. Mungu na taifa liendelee kumbariki.

  Alaaniwe yeyote anayetumia uwezo wake wa kimaarifa au kifedha kuukandamiza umma wa Tanzania, iwe fedha za umma, zake mwenyewe au za kukopa, za wafadhili wa nje au ndani, halali au si halali, anayeshabikia sera kandamizi, ufisadi na mafisadi, awe mtawala au mtawaliwa, anayeshiriki au kushirikishwa katika kutukandamiza watanzania, raia au mgeni - ni adui wa haki! Mungu na taifa liendelee kumlaani.

  Wanaofaidika na aina yeyote ile ya "wizi wa haki" unaofanywa na serikali tawala ya CCM hata siku moja hawawezi kuwa mstari wa mbele kutetea haki kwenye mapambano au majadiliano ya "kulikomboa" taifa letu. Napata tumaini jema kwa kutambua kuwa nguvu ya umma ni kubwa mno na inazidi kupata uelewa wa nini kinachofanyika na nini kifanyike.

  Mwenye macho haambiwi tazama. Mwenye maskio haambiwi sikia. Hata asiyeona na/au asiyesikia, huitaji kutumia nguvu ya ziada kutambua lipi ni sawa na lipi si sawa. Yupi rafiki na yupi adui. Saa ya mapinduzi imefika. Nawasilisha


  [HR][/HR]1. Majibu ya uzi huu ni kielelezo cha yupi anayestahili baraka za mungu na za taifa na yupi anayestahili laana.
  2. Nimetumia Katiba ya JMT ibara ya 18 kifungu 1 na 2, Uhuru wa Maoni - sheria ya 1984 namba 15 ibara ya 6.
   
Loading...