Tanzania bara ni nchi gani?

Tanzania bara ni nchi gani?

Hakuna wala sehemu inayoitwa Tanzania Bara. Bali kuna Tanzania na pia Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania.
 
Ukiwa na kiherehere cha kuvunja muungano tunakukill!!Simpo
 
Hakuna kitu huwa kinanikera na kuniuma kumsikia mtu akisema Tanzania Bara, kwanini viongozi wetu hawana uthubutu wa kusema Tanganyika?
 
Hakuna kitu huwa kinanikera na kuniuma kumsikia mtu akisema Tanzania Bara, kwanini viongozi wetu hawana uthubutu wa kusema Tanganyika?

matatizo ya uhuru ndani ya kisahani hayo.. hawana uchungu nayo.
kama kweli wanapenda umoja momba muungano wa afrika mashariki wanasita. kenya,uganda na rwanda wanasonga mbele. na kuiacha tz na unafiki wake
shida yao ni kuitawala zanzibar lkn game is over tushashtuka. TUNAWAWACHA MJIJADILI UPUUZI Sznz ileeeeeee
 
inaonekana Nyerere anakukosesha sana usingizi eee

Umeona eeh, yaani hakuna tofauti na shetani anavyokosa kupumua pale Jina la Yesu Kristu wa Nazarete litamkwapo na waaminio.
 
Mbaya zaidi tunaaminishwa historia ambayo ilishapitwa, kwanini huo muungano usibaki kuwa historia kama matukio mengine?
 

Hapo umeumiza kichwa? Nyerere kafanya si sawa, kafanya makosa. Kama umekubaliana na hilo bila kuumiza kichwa kwanini uwe na dhanna ya kuwa mimi Nyerere aniumiza kichwa?

Anawaumiza vichwa wale wanaoyaona makosa ya Nyerere lakini wanashindwa kusema kuwa ni makosa, kwa ujinga wao tu.
 
Vipi kuhusu Kikwete kuizika Tanganyika ilhali ibado ICU

Kikwete kasema kinaga ubaga:

Nawaomba wajumbe mnapojadili aina ya Muungano unaofaa Tanzania muwe watulivu! Epukeni jazba!

- Madai ya Serikali Tatu si jambo jipya! Mwaka 1984 ilikuwa hoja iliyopelekea machafuko huko Zanzibar.

- Suala la Serikali Tatu Wajumbe mlizungumze limalizike. Kama zinakubaliwa, zikubaliwe; kama kukataliwa ijulikane!

Source: https://www.jamiiforums.com/katiba-...-hotuba-ya-rais-uzinduzi-wa-bunge-maalum.html

Sasa wewe hapo ni nini usichokielewa, kwanini maleta mambo ya kufikiri vichwani mwenu, hivi kusema ukweli huwa kunawashinda nini?

Amma kweli kuna "watu wana viwanda vya uongo" - Kikwete.
 
inaonekana Nyerere anakukosesha sana usingizi eee

Kwanza irudi Tanganyika na mipaka yake harafu tungane na Burundi au Malawi zanzibar tuachane nao hakuna chochote miaka 50 chakunivunia kwa kungana nao ni wavivu wa.zenji
 
Tunajiita wa Tanzania sababu ya muungano wa nch mbili,muungano kama utakufa,tunabaki ya Tanganyika na Zanzibar,kama ni serikal 3,kuna Tanganyika,Zanzibar na Tanzania(Tanganyika+Zanzibar)
 
Kama ilikufa na Visiwani ilitakiwa ife pia ili kizaliwe kitu kipya Tanzania. Sasa Tanganyika ilikufa na Zanzibar ikaponaponaje?

Hapooo sasa ndipo tunapopewa majibu rais kwa maswali magumu! Na sijui trh 9 Dec. kila mwaka huwa tunasheherekea uhuru wa nchi gani kama Tanganyika ilikufa!!!
 
Najuaga kuna Tanzania(Tanganyika) na Zanzibar(visiwani)

Sikuwahi kutambulisha watu kuwa Tanzania ni bara na Zanzibar ni visiwani.

Bado napata shida kuambiwa Zanzibar ni Tanzania...hata kwenye masomo ya uraia na historia shule ya msingi sikuwahi kufunzwa kuichora Zanzibar kama vile niwezavyo Tanzania...ilikuwa unaweka polygon shapes tu kwenye bahari ya hindi kuashiria Zanzibar.

*an apology for offensive words
 
Tuwalaumu viongozi wetu wanao onekana dhairi kuiogopa znz nikijiuliza kwa nini sipati jibu mpaka leo!

Hakuza nchi znz ila najuwa kuna bara na visiwani na kama kuna znz basi pia tanganyika ipo.

Hakuna kitu bara,bara hata kenya wanatumia bali kwa neno tanzania ni muungano wa tanganyika na zanzibar,wazanzibar walikataa kuitoa muhanga nchi yao kwa kukabidhi madaraka ktk muungano,zanzibar wanauchungu zaidi uhuru wao ni wa mapinduzi na kumwagika damu nyingi sana lkn tanganyika sisi uhuru wetu ni wa kudai tu kwa jina jengine ni uhuru wa mezani tu,kwa hiyo tutakuwa tunawasakama wazanzibar lkn wana uchungu sana na nchi yao,sisi kwa hila tu za kutaka kuimeza znz ndio tukaiua tanganyika yetu kwa kutojua athari zake.
 
Hapooo sasa ndipo tunapopewa majibu rais kwa maswali magumu! Na sijui trh 9 Dec. kila mwaka huwa tunasheherekea uhuru wa nchi gani kama Tanganyika ilikufa!!!

Wao wanasema tunahadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania bara. Watawala wa CCM wana vituko sana. Nawasifu watu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na Chama cha Wakulima wa Tanganyika (TFA) kwa kuendelea kulienzi jina la nchi yangu ambayo wazazi wetu walipigania kuwa nchi huru na ijitawale! Jina TANZANIA lina GUNDU ndio maana hatuendelei wala kufanikiwa hata ktk michezo tu!!
 
Kama ilikufa na Visiwani ilitakiwa ife pia ili kizaliwe kitu kipya Tanzania. Sasa Tanganyika ilikufa na Zanzibar ikaponaponaje?

Wazanzibar wana akili na uchungu na nchi yao,zanzibar uhuru wao ni wa kimapinduzi na kumwaga damu sio huu wa kwetu tanganyika wa mezani na sherehe hata kofi hajapigwa mtu,wazanzibar hawawezi kuwa wapuuzi km sisi kuiua tanganyika yetu,na wanaogopa kuvunja muungano kwa kuwa tanzania nayo itakufa na haitakuwepo yena duniani,nchi itaanza upya kuzaliwa kitu ambacho kitawakost sana wabara,nawapa hongera sana wazanzibar kwa kuithamini na kujua uchungu wa uhuru wao wa kimapinduzi sio sisi wa kupewa mezani huku tunasherekea.
 
Back
Top Bottom