Tanzania Athletics Special Thread | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania Athletics Special Thread

Discussion in 'Sports' started by Mbu, May 2, 2010.

 1. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ..Jamani eee,

  kumradhi wale waliozaliwa baada ya Azimio la Arusha. Sisi wengine tulijionea vipaji ambavyo kwakweli leo hii tunajiuliza kulikoni vipaji hivi vimetoweka kwenye Riadha hapa nchini. Leo hii hatufui dafu hata kwa Wakenya? Tunashuhudia wahabeshi wakitajirika tu kwenye mbio ambazo miaka na miaka tulikuwa na washiriki mahiri kabisa.

  UMISETA jamani, UMISETA!!! ...tufanye nini kuzalisha tena vipaji?

  [​IMG]

  Filbert Bayi.

  Huyu bado anashikilia Commonwealth record ya 3:33:2 aliyoivunja miaka Thelathini na sita (ndiyo 36!!!) iliyopita kule Christchurch New Zealand mwaka 1974 mbio za mita 1500!!!

  Mbali na record hiyo, alivunja 1m record 1975, na alitupatia medali ya fedha kwenye 3000m steeple chase kwenye michezo ya Olympic Uursi mwaka 1980.

  [​IMG]

  Suleiman Nyambui.

  Alituletea medali ya fedha baada ya kuibuka kidedea kwenye mchuano wa 5000m kwenye michezo ya Olympic 1980 kule Urusi.

  Licha ya hayo, alikuwa mwakilishi wetu mzuri tu chuoni UTEP (University of Texas at El Paso) ambako February 1981, alivunja world indoor 5,000 meter record kwa kutumia muda wa 13:20.4.


  [​IMG]

  Gidamis Shahanga,

  ...huyu alikuwa anatutoa kimasomaso kwenye mchuano wa Mbio ndefu za 10,000m na Marathon!

  1988 East and Central African Championships - gold medal (10,000 metres)
  1984 Rotterdam Marathon - gold medal
  1982 Commonwealth Games - gold medal (10,000 metres)
  1979 All African Games - silver medal (marathon)
  1978 Commonwealth Games - gold medal (marathon)

  [​IMG]

  Juma Ikangaa!

  1982 Commonwealth Games - Brisbane Australia Silver Medal
  1988-1990 2nd place Boston Marathon
  1989 Winner New York Marathon
  1987 Winner Beijing Marathon
  1986 Winner, second place 1983 Fukuoka JPN Marathon
  1984, 1986 Winner; second place 1988 Tokyo Marathon
  1983, 1984 Winner Melbourne Marathon

  ...Pamoja na wengineo wengi, mfano Nzael Kyomo, Mwinga Mwanjala, Mossi Ally, Zakayo Marekwa, ukoo wa kina Naali, na wengineo Taifa linahitaji kuzalisha, kukuza na kutoa wanariadha wapya wataolinyanyua juu kwa mara nyingine tena Jina la Tanzania kwenye Riadha.

  Tufanyeje...? UMISETA ipo??? wafadhili je?
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mambo yetu ni kukurupuka tu dakika za mwisho. Commonwealth games za mwaka huu 2010 zinafanyika New Delhi India. Timu zetu za Ndondi na riadha zipo tayari?

  ...yaani hawa kina Nyambui wana set viwango muda huu, tena kwanza wakutane kupanga...wakati michezo inaanza October 3, 2010 ??? wanajua bado miezi minne tu imebakia ya maandalizi?

  Walikuwa wapi kujiandaa tangu kumalizika michezo ile ya Commonwealth 2006 kule Melbourne Australia na 2008 Olympic games Beijing China?...
  yaani leo hii ndio mnapanga mikakati ya kukaa mpange viwango??? Wenzetu tayari wanajiandaa na Olympic 2014 itayofanyika Uingereza!!

  Acheni hizo za "funika kombe mwanaharamu apite!"... tumewachagua nyinyi kwa kuthamini mchango wenu kwenye riadha Tanzania, mnatuangusha!!!

  Juma Ikangaa alisema na ninamnukuu; "To win means nothing without the will to prepare.”
   
 3. Loner

  Loner JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I agree with you totally... Ni kweli kwamba tunahitaji kufanya mambo mengi kupromote Athletes here in Tanzania... Kuna marathon's hapa Nchini lakini ukiangalia professional's are very few... Most of them are amateur's.... Na Umiseta doe's not help student's get motivated... of we had school scholarship's for sport's ingekua vizuri sana. Unakuta unampa kijana motivation ya sport's with benefits ya elimu.
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...bwana wee, yaani mimi nachoka kabisa. I hope dada Shy-Rose unanisoma,...NMB mgeuze ukurasa mwingine, badala ya misaada ya madawati (hata Vodafone wanatoa), jadilianeni mfadhili pia UMISETA (kama bado ipo, maana miaka mingi sijaisikia michezo hii).

  Sponsors wengine kama Zein, bro Kelvin japo wewe ni mwana mpira wa kikapu si unanisoma? Tigo, Vodacom... deals ndio hizi wajameni...Kaka Andrew Minja wa Serengeti, ulikuwa na msingi mzuri tu pale Muhimbili Primary, nawe ulikuwa mkimbiaji enzi zile au sio? Promotion wazee!

  I hope debe hili haliendi bure au kujaliwa na wajanja huko chama cha riadha.
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...asanteni sana ZARA TOURS kwa ku sponsor mashindano yale,...tunahitaji ushirikiano wenu zaidi.

   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Kwa hisani ya Blog ya Michuzi,...Ahsanteni TIGO kwa kudhamini Ngorongoro Marathon ya Mwaka huu 2010... Juhudi zenu zaidi zinahitajika kuibua vipaji!...

   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...who prepares to plan, prepares to fail...

  ...Jamani eee, nimechoka kuona wahabeshi na wakenya tu wanashinda hizi mbio, hatuwezi kujipangia mipango na maandalizi hata kuwaiga basi???
   
 8. Loner

  Loner JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inabidi Project kama hizo tufanyiye kazi sana... Asante kwa insight juu ya hiyo topic..
   
Loading...