Tanzania agricultural television (tatv) / channel | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania agricultural television (tatv) / channel

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sabi Sanda, Apr 28, 2010.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakuu,

  Jana kupitia TBC Taifa nilimsikia Mkulima mmoja wa Korosho akisema kuwa hawajui ni umbali gani unatakiwa uwepo kati ya mkorosho mmoja na mwingine wakati wa kupanda. Habari hii kwa kweli ilinisikitisha sana. Nchi hii kwa sasa ina upungufu wa Maafisa Ugani wasiopungua 11,000. Kama kweli tunataka kuleta mapinduzi ya kweli katika kilimo hatuna njia nyingine bali kuhakikisha kuwa wakulima wetu wanaelimika kiasi cha kutosha. Moja ya njia rahisi na yenye gharama nafuu katika kuwaelimisha wakulima wetu kwa kiwango kikubwa ni kuendesha SHAMBA DARASA kupitia njia ya Televisheni. Uwekezaji wa shilingi milioni 10 tu kila mwaka kwa miaka mitano katika kila kijiji kwa ajili ya umeme jua utatusaidia kwa kiwango kikubwa. Tunaweza kuamua kuwa na Televisheni Maalum ya Kilimo kwa ajili ya kuwafikia wakulima wetu kwa mamilioni au TBC inaweza kuwezeshwa kwa kupatiwa angalau shilingi bilioni 10 kila mwaka kwa miaka 10 na kuanzisha CHANNEL MAALUM YA KILIMO na kuhakikisha inapatikana kila kona ya nchi hii.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,239
  Trophy Points: 280
  Sabi Sanda, unaona mbali, TBC inamwaga channel zaidi ya 100 hivi karibuni, sio jumu tena la TBC kuanzisha kipindi, bali kilas wizara inakuwa na programu yake, kila mamlaka ya mazao inakuwa na programu yake kama ilivyo DSTV, hadi JF, tukiamu tunakwenda hewani. Zile podcast kama za Mzee Mwanakijiji, na ma online radio kibao ikiwemo Bongo Radio, sasa ni kwa wote, tatizo sio bure bakli kwa Decoda, inalipiwa elfu 5,000 tuu!.
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Apr 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Hii imetulia..Tutakuwa tumekwenda mbali kihabari na Tanzania yetu.
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Na mipira watamuonyesha nani?
   
 5. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Sawa wazo zuri.Lakini tatizo litakuwa ni uendeshaji tu.kwa sababu kama kukitu wa-Tz kinacho tu shinda basi ni Management ya Miradi.
   
 6. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli nimeamini kuwa KILIO NA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU.

  Hatuna njia bila televisheni na redio maalum za elimu safari yetu ya maendeleo itakuwa ndefu kupita kiasi.

  Pasco, asante sana kwa hiyo update. Wengine tumeandika sana kuhusu hili. Inatia moyo kuona kuwa sasa Serikali imekubali kutumia Televisheni kufundisha wanafunzi wetu wakianzia na wale wa sekondari. Bila shaka tutafika.
   
 7. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pasco,

  Hebu tupe update ya hizo channels toka TBC.
   
Loading...