1. Vasco da Gama alipopitia Bagamoyo alishangazwa sana na utajiri na majengo makali ... akipita leo ataona nini? hatuna mentality ya continuity. Ulaya, Marekani, Uchina, India, nk - leo ni nchi za maendeleo hata ka vile zinaficha wamaskini wao. Mawazoni mwangu - sababu ni mzee alianza kujenga 'nyumba' ya miti, mtoto wake alianza kufyatua matofari, mjukuu wake alijenga gorofa akitumia matofari... sisi huku watoto na wajukuu wanaishi ndani ya nyumba ya udongo ilojengwa na baba/babu afu ikibomoka - tunahama na kujenga nyumba nyingine ya udongo. Sijui ni uvivu ama kutokuwa na mentality ya ku-invest kwa generation ijayo. Kwa mfano, ka viongozi wetu wangekazana kujenga mabarabara baada ya kupata uhuru - hata ka majenzi yangemalizika baada ya miaka kumi, leo tungekuwa mbali. Mazao ya mkulima yakisafirishwa kirahisi kwenda mjini ama viwandani, basi wamjini na mkulima watatajirika.
2. Tunategemea kuendelezwa na wa-nje ambao wanatuogopa tukiendelea, na pia watapoteza soko na mazao ... kwa nini watatusaidia? Mbona hatustuswi na wakina IMF ambao masharti yao watupayo tukiwa na njaa ni ya kuendeleza nchi zao badala ya zetu????? Wakati viwanda vyetu, masipitali, mashule, nk yanabomoka, wanatupa mkopo wenye masharti ya kulima mazao ya biashara...
3. Labda hewa joto inatufanya tuwe wavivu kujenga... Ulaya, kibanda kitakuwa baridi nusu ya mwaka, kwa hiyo kila generation inataka kujenga jumba zuri la kuzuia baridi... again, plan za viongozi hazionyeshi kuwa lengo urgent la ku-invest in future. Seemingly, viongozi na sisi wengi tuna mentality ya kutojali kesho ka tumbo lajazwa leo. Hatujiulizi maisha ya mjukuu yatakuwaje na tuanze kujenga nini ili wafaidike...
4. Sirikali zatufanya wananchi tuwe vipofu wakati viongozi wakiiuza nchi yetu bila sisi kunufaika. Wananchi tunahitaji kuamka na kuanza kuwauliza viongozi 'mliitumiaje?'
5. Hatuna effective tax collecting system... matajiri wanaficha pesa kirahisi tu, na wengi hawana lengo la kunufaisha ama kutajirisha nchi ... back to that mentality ya 'leo' tu, fvck 'kesho'.
6. Kuna wengi wenye mentality ya 'maintaining caste system' ... hawataki kumuendeleza mtumishi wao kwa sababu hawataki kumlipa vizuri ama kumpoteza - kwa hiyo wanamnyima... viongozi pia wana mentality hii. Mtajiri mmoja atamponda mwingine ili awe yeye tu tajiri ... hata ka kuna mali nyingi tu.
7. Rome haikujengwa kwa 'siku moja'. Sisi wengi tunataka jengo liibuke baada ya 'siku moja' ama si maendeleo afu hatuanzi kujenga... sadly, tunapima maendeleo na nchi ambazo zimekuwa na uhuru wa miaka 200, na tunataka hayo maendeleo yaibuke 'leo' bila jasho lingi. Juzi niliiona picha ya gari la zamani la jeshi la USA... lilikuwa la mbao na bila madirisha. Walianzia mbali...
8. Najua nchi yetu ni maskini... lakini kwani si dola moja yanunua vingi kwetu kuliko Marekani? Sasa hivi vipimo vya waUlaya vina-equate kwetu? $500 itanunua mengi Tz kuliko Ulaya ... ama? Tunahitaji vipimo vya maendeleo tofauti na hivi vya UN... kwa mfano, nani ana barabara nzuri, masipitali bora, nk badala ya wangapi walipwa dola 1000. Just a thought.