TANU ilivyoingia mikoa ya kusini ya Tanganyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANU ilivyoingia mikoa ya kusini ya Tanganyika

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mohamed Said, Feb 23, 2012.

 1. Mohamed Said

  Mohamed Said Verified User

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 2, 2008
  Messages: 10,769
  Likes Received: 5,759
  Trophy Points: 280
  Hapana Haja ya Kuiogopa Historia ya Uhuru wa Tanganyika

  MohamedSaid


  Mzee Yusuf Halimoja karudi tena safari hii anasemakatika kichwa cha makala yake, "Sijasema Uhuru Uliletwa na Nyerere" (JamhuriJanuari 31 Februari 6 2012). Katika makala hii wakati mnakasha (majadilano)unanogayeye katangaza kuwa anajitoa. Waswahili tuna msemo, "ametoa mbukwa." Juu ya hukokujitoa madam kanitaja katika makala yake sina budi nami kumpa majibu yangu katikayale niyajuayo katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Mzee Halimoja labda kwautu uzima huwa anasema mengi. Mimi sitajibu kila aliloandika ila nitapita mleambamo nahisi wasomaji watafaidika na kitu kipya ambacho hawakuwa wakikijuakabla ya hapo.

  Si kweli kuwa Nyerere aliongoza juhudi za uhurupeke yake. Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka 1952 na akapokelewa na rais wa TAA AbdulwahidSykes na alikuta mambo yako mbali sana. Kirilo kenda UNO na kurudi, TAA ishazungumza na Kamati yaUmoja wa Mataifa inayosimamia nchi zilizokuwa chini ya Udhamini na ishapelekamapendekezo ya katiba kwa Gavana Twining, TAA imeshaunda Kamati ya Siasa naikapeleka viongozi wake (Abbas Sykes, Japhet Kirilo na Saadan AbduKandoro) kutembea nchi nzima kuzungumzana wananchi kuhusu madhila ya ukoloni.Juu ya hayo yote TAA imeshafanya uhusiano na vyama vingine vya siasa kama African NationalCongress (ANC) ya Northern Rhodesia chini ya Kenneth Kaunda. (Ally Sykes hadileo ana barua kadhaa alizokuwa akiandikiana na Kaunda kabla Kaunda hatahajauana na Nyerere). Vilevile Abdulwahid alikuwa kafanya mkutano na Kenyatta wakatiwala Kenyatta hajasikia jina la Nyerere. Nia ya mikutano hii ilikuwa kuunganishajuhudi za TAA na KAU katika kupambana na Waingereza.

  Kwa wengi mambo haya ni mageni katika masikioyao wameleweshwa na propaganda za TAA hakikuwa chama cha siasa. Simlaumu MzeeHalimoja naamini kabisa kuwa yeye haya hakuwa anayajua. Kwa Mzee Halimoja siasaTanganyika haikuwezekana bila Nyerere na TANU chama ambacho Nyerere mwenyewe walahana chimbuko nacho. Halimoja anazungumza kuhusu ujasiri wa Nyerere. Sawahapana neno lakini je anaujua ujasiri wa Schneider Abdillahi Plantan katika TAAkiasi ambacho Waingereza walimkamata na kumweka kuzuizini? Je Halimoja anajuakisa cha Dome Okochi Budohi Mkenya kadi yake ya TANU na 6 kazi aliyokuwaakifanya katika harakati za TAA kabla hawajaunda TANU akiwa ndiye kiunganishokati ya TAA na KAU ya Kenyatta? Ninaweza kumpa mifano kocho. Budohi alikamatwamwaka 1955 pamoja na wanaharakati wengine wa Kenya kwa tuhuma za kuwa Mau Mau.Budohi alifungwa kisiwa cha Lamu kuazia 1955 hadi 1963 Kenya ilipokuwainakaribia kupata uhuru ndipo alipoachiwa. Budohi akifahamiana vyema kabisa nawazee wangu na nimejifunza mengi kutoka kwake kuhusu TAA na TANU. Lakini kama MzeeHalimoja anataka kubaki na historia ya Nyerere inayoanza na TANU 1954 nakupuuza michango ya wengine mimi sina ugomvi na hilo. Naamini kwa haya machachemsomaji kapata yale ambayo hakuwa anayajua kabla na keshatambua kuwa TAAkilikuwa chama cha siasa hata kabla Nyerere hajakutana na Abdu Sykes Dar esSalaam mwaka 1952.

  Mzee Halimoja kazungumzia kuhusu AbdulwahidSykes kuwa kwa nini natumia rejea zake. Napenda kumafahamisha kitu kimoja.Historia ya Nyerere na TANU itakuwa salama na ikafahamika kama inavyofahamikakatika historia rasmi mfano wa hii ya Mzee Halimoja ikiwa tu Abdulwahid Sykesutamtoa katika historia ya TAA na TANU na historia ya Nyerere mwenyewe. Lakinipale tu utamkapomleta marehemu Abdu katika historia ya TAA na TANU itakubidiuachane na Nyerere kwanza na urudi robo karne nyuma kupata mwanzo wa harakatina hapo ndipo unapambana na Nyaraka za Sykes na hazitakuwa za Abdulwahid baliza baba yake. Hapo ndipo utakapojua umuhimu wa nyaraka hizi. Kueleza yaliyomohumo katika nyaraka hizo inataka mada itakayojitegemea yenyewe kwani ni historiainayorudi nyuma karne moja. John Iliffe aliondoka na baadhi ya nyaraka hiziambazo alikabidhiwa na binti yake Abdu Sykes, Daisy Aisha wakati Daisyalipokuwa mwanafunzi wake wa historia miaka ya 1960 katikati Chuo Kikuu Cha Dares Salaam na Iliffe hajazirejesha hadi leo. Nyaraka hizo ndizo zilizomsaidiaIllife kuandika historia ya TAA. Kwa nini historia ya harakati ipatikane kwamtu mmoja tu Abdu Sykes kama anavyouliza Mzee Halimoja, jibu lake ni hili, babayake Abdu, Kleist Sykes ndiye aliyeasisi harakati za siasa Tanganyika mwaka1929 na ameacha nyuma hazina kubwa ya maandiko. Anaetaka kujua zaidi na asome "KleistSykes, The Townsman" na Daisy Sykes katika "Modern Tanzania," kitabukilichohaririwa na John Illife.

  Mzee Halimoja anasema Nyerere ndiye aliyeandikakatiba ya TANU. Nataka nimweke sawa Mzee Halimoja kuhusu katiba ya TANU. Katibaya TANU haikuandikwa na yeyote yule. Kwa ufupi ni kuwa Nyerere hakuandikakatiba ya TANU. TAA Political Sub Committee ilinakili katiba ya ConventionPeoples Party (CPP) ya Kwame Nkrumah neno kwa neno. Mzee Halimoja akitakaushahidi aitafute katiba ya CPP na aifananishe na katiba ya TANU. Hilo lakwanza. Kitu cha pili napenda kumsahihisha kwa heshima zote Mzee Halimoja kuwahiyo ilani namba 14 aliyoeleza kuwa ilitolewa na Waingereza haikuwa namba 14bali namba tano ikijulikana kama Government Circular No. 5 (1 August 1953)ikiwakumbusha viongozi wa TAA kutojiingiza katika siasa. Haya yalitokea baadaya serikali kuwa na ushahidi kuwa TAA ilikuwa inafanya siasa dhahir shahirjambo ambalo Mzee Halimoja hataki kulisikia sharti siasa iwe na Nyerere yumo.Baada ya kuona akina Abdu Sykes na Hamza Mwapachu hawasikii wameshikilia tu kuwasakamaWaingereza na serikali yao ikatoka Government Circular No.6. Hapa kuna kisa chakuhadithia lakini kwa makala hii tutajitoa nje ya maudhui. Kipindi hiki wengiwalikikimbia chama wakabaki wanamji. Abdulwahid ilibaki kidogo apoteze kaziyake kama Market Master Soko la Kariakoo. Hii ndiyo historia ya siasa ya TAA naTANU niijuayo mie, historia ambayo wazee wangu walikuwa wachezaji wa kikosi chakwanza na wakinihadithia siku zote hadi walipotangulia mbele ya haki. Jambo latatu Mzee Halimoja hasemi kweli kuhusu historia ya TANU katika sehemu zileambazo kanisa lilikuwa na nguvu. Ukweli ni kuwa waliochelewa kuingia TANU siWarufiji na Wangindo bali watu wa Masasi, Peramiho na kwengineko kutokana nashinikizo la Kanisa. Niruhusu msomaji mpenzi nikudokolee kidogo mambo kutoka katikahazina ya wazee wangu.

  Mkutano wa kwanza wa TANU 1955 ulihudhuriwa naSalum Mpunga na Ali Ibrahim Mnjawale kutoka Lindi. Mkutano huu ulifanyika Dares Salaam Ukumbi wa Hindu Mandal. Baadaya mkutano, wakati wajumbe wengine wanaondoka kurudi kwenye majimbo yao, Mpungana Mnjawale walibakia nyuma kukutana na uongozi wa makao makuu wa Julius Nyerere,Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe, Said Chamwenyewe, OscarKambona na wengineo. Mpunga na Mnjawale waliwafahamisha viongozi wa makao makuukuhusu hali mbaya ya siasa Jimbo la Kusini. Mbali na kampeni za kuipinga TANUza Liwali Yustino Mponda ambae Mzee Halimoja anamfahamu vyema kabisa, katikaziara yake Lindi Gavana Twining aliwatahadharisha Waafriika wa Tanganyikawasijihusishe na "wafanya fujo" wanaotaka kuzusha vurugu. Twining alikuwaakitoa onyo hili akiikusudia TANU. Hotuba hii ya Gavana iliwatisha wananchi wengikutoka sehemu za kusini kujiunga na TANU.

  Mpunga na Mnjawale waliomba Nyerere aendemajimbo ya kusini kuhamasisha wananchi ili wakabiliane na fitna za Gavana Twiningna kampeni za kupinga TANU zilizokuwa zikiendeshwa na Liwali Yustino Mponda. Ukwelini kuwa Nyerere hakutaka kwenda katika ziara ile akijua kuwa huko alikuwaanakwenda kupambana na kanisa lake uso kwa macho. Juu hayo yote Mpunga naMnjawale katika kikao kile walimsisitizia Nyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindiambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANU kupata ufanisi Newala, Songea,Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya TANU. Katikasehemu hizo Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU. SheikhSuleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wote waliungamkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili. Baada ya kufikia makubaliano,Mpunga na Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari ya Nyerere. Ali MwinyiTambwe na Rajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoawasiwasi na woga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.

  Nyerere na msafara wake ulipokelewa na uongoziwa TANU wa Lindi huko Mbanji, kijiji kidogo nje ya mji. Msafara wa Nyerereulipowasili Mbanji ilikuwa kiasi cha saa moja jioni hivi na giza lilikuwalinaanza kutanda. Mbali na Mpunga na wale wajumbe wawili waliokutana na Nyereremjini Dar es Salaam mwezi uliopita, hakuna hata mtu kati ya umma ule uliokujakupokea ujumbe kutoka makao makuu ya TANU aliyekuwa anajua Nyerere anafananavipi. Mpunga, dereva wa lori, alijibagua kutoka kwa lile kundi la watu akawaamesimama pembeni ili Nyerere apate kumuona. Baada ya Nyerere kumtia Mpungamachoni, Mpunga alimwendea kumsalimu Nyerere, Tambwe na Diwani; kisha aliligeukialile kundi la watu kumtambulisha Nyerere kwa wananchi akilitaja jina lake kwasauti kubwa. Baada ya hapo aliutambulisha ule ujumbe wa Nyerere. Nyerere naujumbe wake ulisindikizwa kwa shangwe na kundi la watu hadi ofisi ya TANUkwenye nyumba ya Suleiman Masudi Mnonji. Kupakana na ofisi ya TANU ilikuweponyumba ya seremala mmoja, Issa bin Ali Naliwanda. Hii ndiyo nyumbailiyochaguliwa alale Nyerere na ujumbe wake, si kwa sababu ilikuwa nzuri kupitazote. Ilichaguliwa na kupewa heshima hii kwa sababu ilikuwa karibu sana naofisi ya TANU na hivyo basi ilirahisishia TANU kazi ya ulinzi wa Nyerere. Sikuiliyofuata ilikuwa Jumapili na Nyerere aliwaomba wenyeji wake apelekwe kanisanikwa ajili ya ibada.

  Kanisa Katoliki mjini Lindi ni jengo la faharilililoko ufukweni katika Bahari ya Hindi. Lindi ulikuwa mji wa Waislam. Mbalina mlio wa kengele za kanisa hakuna mtu pale mjini aliyekuwa akishughulishwa nakile kilichokuwa kikifanyika kwenye viwanja vya kanisa. Watu wachache waliokuwawakienda kusali kanisani walikuwa Wakristo waliokuja Lindi kutoka sehemunyingine za Tanganyika kufanya kazi katika ofisi za serikali. Ghafla mahalahapa palipokuwa pweke, palipopuuzwa kwa miaka na Waislam wa mjini, pakawamuhimu kwa sababu rais wa TANU ambae alikuwa Mkatoliki alikuwa na haja yakuhudhuria ibada pale kanisani. Hakuna mtu katika uongozi wa TANU wa Lindialiyejua ndani ya kanisa lile kulikuwa vipi wala hapakuwa na yoyote kati yaoaliyewahi kuingia ndani ya kanisa, si Lindi wala mahali popote pale. Uongozi waTANU wa Waislam mjini Lindi haukumwamini Mkristo yoyote kumsindikiza Nyererekanisani ili kumpa ulinzi. Baada ya kujadili suala hilo kwa urefu hatimayeiliamuliwa kuwa Mpunga na wanachama wachache Waislam wenye kuaminika lazimawamsindikize Nyerere kanisani na wengine wabakie nje kulinda mlango.

  Jumapili hiyo Nyerere aliingia ndani ya kanisaKatoliki mjini Lindi akifuatwa nyuma na walinzi wake Waislam wakiongozwa naSalum Mpunga, dereva wa lori shupavu. Misa hii maalum ilidumu katika fikra za wale Wakristowaliokuwepo pale kanisani kwa miaka mingi kwa kuwa tukio hilo liliwagusa sanaWakristo walioshuhudia mkasa ule ndani ya kanisa la Lindi. Hii huenda ilikuwamara ya kwanza na ya mwisho kwa Nyerere kumsalia Mungu wake huku akiwaamesimamiwa na Waislam. DC mkoloni alikataa kutoa kibali kwa TANU kufanyamkutano wa hadhara. Akiwa amekasirika sana, Shabaan Msangi aliitisha mkutano wadharura wa tawi uliohudhuriwa na Nyerere na Tambwe. Baada ya mkutano huo Tambwealikwenda kumwona DC. Ruhusa ilitolewa, na adhuhuri hiyo siku ya Jumapili,katika kiwanja ambacho Wazungu walikuwa wakicheza gofu, ambako mwaka mmojauliopita Gavana Edward Francis Twining alitoa hotuba iliyowavunja moyoWaafrika, Nyerere alihutubia mkutano wa hadhara. Kamwe haijapata kutokea kablaya siku ile katika historia nzima ya Jimbo la Kusini, watu wengi kiasi hichokujumuika mahali pamoja. Wazungu na Wahindi pamoja na askari, watu wakiwawamekaa na wengine wamesimama katika ya jua kali walikuja kumsikiliza Nyerereakihutubia. Ili kuhakikisha amani na usalama pale mkutanoni serikali iliwekaaskari waliouzunguka uwanja mzima wa mkutano. Nyerere aliwafikishia watu uleujumbe wa TANU wa kuwa, kutawaliwa ni fedheha, na Waafrika wa Tanganyika lazimawadai uhuru wao. Uingereza ilikuwa ikiitawala Tanganyika chini ya udhamini kwaniaba ya Umoja wa Mataifa, na wakati ukiwa muafaka inabidi Uingereza ikabidhinchi kwa wananchi wenyewe. TANU ilikuwa imewasili Jimbo la Kusini.

  Wasomaji wapenzi katika makala yangu iliyopitanilimpa changamoto Mzee Halimoja aeleze ni akina nani waliingiza TANU kwao hukoMasasi na Peramiho. Ukweli ni kuwa hata kugusia hili katika makala yakeiliyopita hakuthubutu. Nimempa changamoto aeleze hicho anachokiita "mchango wapekee wa Nyerere" katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Hilo vilevile limemshinda.Nashukuru kuwa kanijibu ingawa kakwepa baadhi ya mambo muhimu lakini kwa kufanyahivyo kanipa mimi nafasi ya kueleza yale ambayo naamini wengi walikuwahawayajui. Nyerere hakuwa peke yake katika kuupigania uhuru wa Tanganyika walahakuandika katiba ya TANU wala harakati za kupigania uhuru hakuzianzisha yeye. Nadhanihaya niliyoandika yanatosha kwa sasa na ningependa kumaliza kwa kuuliza swali. Nanileo anawakumbuka wazalendo hawa nilowataja katika makala haya? Je hawastahiliwatu hawa kuenziwa pamoja na Nyerere?

   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,794
  Likes Received: 5,065
  Trophy Points: 280
  Mohamed Said,

  ..OK, Nyerere hakuandika katiba ya Tanu,hakuanzisha harakati za uhuru, etc etc.

  ..hebu basi tueleze mchango wa Mwalimu Nyerere ktk harakati za uhuru ni upi?

  NB:

  ..wakati mwingine nadhani mnavyomponda Nyerere ndiyo mnazidi kumpa sifa hata zile asizostahili.

  ..kwa mfano, ilikuwaje mtu huyu frm no where, hana hili wala lile, aje na makaptura yake mjini halafu apewe nafasi kuongoza waungwana wenye heshima zao ktk jambo zito kama kupigania uhuru?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Oh boy yeye mohammed said anataka watu waamini Nyerere alianza siasa mwaka 1952 alipokuja Dar. Je ni kweli?
   
 4. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  MS. Heshima yako.
  Ushauri: Badilisha Font uliyotumia au jaribu kuongeza size ya font . au hili tatizo ni kwenye browser yangu pekee?
  .
   
 5. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mzee Mohamed Saidi, sema chochote kuhusu Baraza la Mtihani la Tanzania kuwafelisha makusudi vijana wa kiislam. Hili la TAA, TANU, ASP, CCM na mchango wa wazee wa kiislam limechuja. Jee vijana wa kiislam pale Ndanda kususa mitihani ya taifa ya kidato cha sita ni cha kiungwana? jee huko ndio kupambana na mfumo kristo kwa ufanisi?
   
Loading...