Mantombazane
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 579
- 367
Mimi ni mfanya biashara katika eneo la Mbezi mwisho. Tanroads na Dawasco wanaendesha zoezi la kubomoa majengo yote yaliyo juu ya bomba la maji kwa Dawasco na yale yaliyojengwa kwenye hifadhi ya barabara ya Tanroads ambazo walishazuiliwa kujenga. Tatizo la bomoa bomoa hii tunaona kama kuna upendeleo au rushwa kimtindo fulani. Utakuta majengo yamewekwa X wakati wa kubomoa utashangaa mengine yanabomolewa yote, mengine nusu na mengine yanaachwa.Hii inawafanya baadhi ya wafanyabiashara waliobomolewa nusu na ambao hawajabolewa kuendelea na biashara wakati wengine tumefukuzwa.
Tunahisi kuna rushwa inatembea ndio maana tinga tinga linakuwa selective. Sisi tunasema kama wameamua kubomoa majengo yote waliyoweka X wabomoe completely kama wenye majengo wenyewe wamepuuza kubomoa. Lakini mtindo wa kubomolea wengine na wengine kuwaruka kimtindo hatuukubali vinginevyo watuache wote tuendelee na biashara. Kama ni majengo ya kawaida au vighorofa ili mradi viko sehemu isiyotakiwa vibomolewe bila ubaguzi. Tanroads na Dawasco acheni ubaguzi kwenye bomoa bomoa!