KERO TANROADS imeridhia ujenzi huu eneo la barabarani karibu na Ofisi ya DC Ubungo?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kuna jambo linaendelea naona kuna dalili ya kitu fulani ambacho hakipo sawa, kuna ujenzi wa kituo cha mafuta (Sheli) umeanza Mitaa ya Luguruni.


Wameanza kujaza kifusi katika sehemu ambayo nafikiri siyo sahihi kwa sababu, kwanza ipo kwenye roundabout ya kwenda kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya.

Kwa maana hiyo Sheli itakuwa kero kwa magari kuingia na kutoka kwenye kituo hicho, na pale patapokuwa na msafara kero itaongezeka maradufu.

Pili, kituo kinajengwa takribani Mita 300 kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ubungo.

Tatu, kwa plan za barabara zilivyo pale, ujenzi pale sidhani kama unaruhusiwa. Je, TANROADS WANAJUA? Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya Je?

Kwa sasa kifusi kimekuwa kikijazwa hapo usiku tu siyo mchana, inawezekana hiyo inaashiria kwamba kinachofanywa siyo halali.

 
kuna maeneo mengi yanajengwa kiholela, akija kiongozi anayefata sheria utasikia vilio kumbe ni makosa ya wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…