TANROADS Biharamulo, Ngara wanadunda TARURA Arusha kama vile

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,584
2,000
Maajabu ya tumbuzi ya Arusha ya meneja TARURA kuwa hajaleta wananchi kushuhudia vishindo vya awamu ya tano tumeyaona.

Kuwa TANROADS au TARURA Biharamulo na Ngara wangali wanadunda maofisini hata katika ubovu huu wa barabara uliopo usio mfano? Ama kweli kama hii si moja ya maajabu ya Mussa basi maajabu hayo yatakuwa hayapo tena.

Mambo yamekuwa siasa siasa tu hadi ina kera kwa kweli. Kwamba ni tija katika utendaji? Basi Meneja TARURA yule asingetumbuliwa ila kwa sababu hakujaza watu kushuhudia vile vishindo vyetu vya awamu hii, basi jambo limezua jambo.

Hali Biharamulo, Ngara iko kama ilivyo pichani.

Mbaya zaidi kwa ubovu uhusiano na barabara ya Rusahunga Ngara na Rusumo, jana katika eneo la nyabugombe, moja ya maeneo yanayopigiwa kelele kila leo, pana mtu kafa pale kwa ajali ya gari.

Kwa hakika maisha yale hayakuwa na sababu yoyote ile ya kupotea kwani hizi ni zile ajali za wazi zinazosababishwa na mamlaka na ambazo zingeweza kuepukika.

Hadi wafe wangapi ndipo busara kuweza kutumika japo kufanya marekebisho kidogo tu?

Hata kama mameneja nyie mnahamasisha mno kisiasa na hivyo kuendelea kudunda, si muyazibe basi japo haya mashimo au kurekebisha hizi sehemu zilizo mbaya zaidi zenye kuhatarisha zaidi maisha ya watu? Hii ni hata kama mmeamua wenye magari yao wale hasara vilivyo?


IMG_20200710_105815.jpgJafo fika barabara hii kumsaidia Eng. Kamwelwe kusafisha uozo huu.

IMG_20200710_105850.jpg


IMG_20200710_092750.jpg
 

Attachments

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,584
2,000
Ok, tumeelewa,wasalimie huko wahangaza,Kabanga,Rulenge,Nyamiyaga,Bushubi nk
Bila shaka mmetanguliza salamu na malori ya vifusi yanakuja nyuma.

Kama si hivyo, eng. Kamwelwe hammtendei haki.

Mnadhani hata inahitaji mtu kutokea maeneo uliyoorodhesha kulalamika?

Mnadhani utalii ni mpaka aje daktari bingwa KIA, JKNIA au CIA?
 

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
1,564
2,000
Huko ndiko kwenye kipimo cha wananchi kustahimili barabara mbovu, kama alivyothibitisha Jaffo mwenyewe kwa kushauri meneja aliyetumbuliwa apelekwe Buhigwe au Kakonko!. Hivi wabunge wa huko wako likizo?. :oops: 🤔
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,584
2,000
Huko ndiko kwenye kipimo cha wananchi kustahimili barabara mbovu, kama alivyothibitisha Jaffo mwenyewe kwa kushauri meneja aliyetumbuliwa apelekwe Buhigwe au Kakonko!. Hivi wabunge wa huko wako likizo?. :oops: 🤔
Nadhani wapiga kura walioko kwenye njia hii hawana influence yoyote kwa wabunge wala Rais.

Maeneo inakopita hii barabara yako sparsely populated nadhani ndiyo tatizo kubwa.

Hii barabara kutoiangalia kitaifa ni kupotea maboya vilivyo.
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
4,584
2,000
Hilo balaa ni la TANROAD, tarura una waonea tu.
Mkuu si nia yangu kumwonea mtu ndiyo maana nilitumia kiambishi "au" wala siyo "na".

Natumaini wanisoma mkuu.

Hata hivyo huyu TANROADS kama ndiyo mwenye hili balaa basi ni jipu kuliko lilokuwa limeangaziwa na askofu Gwajima - la usoni na lenye kung'aa kama tochi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom