Taaluma ya ujenzi ni pana sana kuliko watu wanavyoichukulia; uwepo wa wahandisi pekee pasipo kuweko na sera zinazompa nguvu mhandisi ni kazi bure!
Tanzania ina wataalam wabobezi wa ujenzi lakini Hatusikilizwi kabisa, wanasiasa wame-dominate field nzima ya ujenzi kiasi cha kuifanya isikue.
Kwa taaluma yangu niliyoipata China katika masuala ya ujenzi, Daraja la Kilosa halikutakiwa kuzidi masaa 6 liwe limejengwa upya.
Teknolojia inayotumika na nchi yetu kushughulika na
Emergency Construction ni ya kizamani sana!
Tutawalaumu bure wahandisi wetu. Tatizo kubwa katika sekta hii nchi yetu haina sera nzuri za ku-hold wabobezi nguli wa ujenzi katika system kwasababu za kisiasa.
Na ikitokea mtaalam ukajitoa kuitumikia nchi unaonekana kama boya mwenye kiherehere utakwamishwa kila hatua na automatically mfumo utakushusha, either ufanane nao au utolewe kafara (yapo mengi ya kusema yanayokera kimfumo)
Ujenzi wa dharura unafanywaje?
Kila makao makuu ya mkoa au wilaya walipaswa kuyajua madaraja yote hususani yasiyo na njia mbadala na kuyaandalia
pre casted beam, piers and slab, ambapo kukiwa na dharula inakuwa rahisi kubeba na kuzipeleka site na kuziunganisha ili kupata
span inayotakiwa!
Temporary platform kwa daraja kama la Kilosa hazikutakiwa kuzidi hata masaa 4 ziwe tayali zipo site! (kikao cha maamuzi kama hayo Wahandisi wa mkoa walipaswa kufanya hata kwenye simu tu
Call conference!. Maandishi yanakuja baadaye watu wakiwa site. Nguvu iliyotumika kupeleka wanasiasa site kwa helikopita ingefaa kubeba "Portland Cement"
Ni aibu kwa barabara inayounganisha inchi zaidi ya nne kufungwa siku 4, kwa kidaraja ambacho kilitakiwa kujengwa hata na fundi mchundo tu within 6 hrs lakini imeshindikana. Waziri wa Ujenzi yupo, Mkurugenzi wa Tanroads yupo, mameneja wapo, wahandisi wapo!
Ngoja nisiseme mengi lakini ukweli ni kwamba bila mikakati ya kisera Tanzania tutadumazana akili bure.
NOTE: Waliopo kwenye mfumo ni either wamedumazwa na mfumo ulivyo au mfumo uliwabeba kukalia nafasi za maamuzi pasi na uwezo.
........."Nothing will change".......