Tani moja ya mitumba yaondolewa sokoni

Tani moja ya mitumba yaondolewa sokoni

Mwaka mpya

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2016
Posts
213
Reaction score
222
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameondoa kwenye soko zaidi ya tani moja ya nguo za ndani za mitumba ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa shirika hilo la kuhakikisha nguo hizo hazitumiwi na Watanzania.

Operesheni ya kuondoa nguo hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Soko la Tandika, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, Mkaguzi wa TBS, Emmanuel Saimon, alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa mikakati ya shirika ya kuondoa nguo hizo kwenye soko kwa sababu zina madhara kiafya.

Alisema miongoni mwa malengo ya uwapo wa shirika hilo ni kulinda afya za walaji, hivyo wanaondoa nguo hizo kwenye soko kwa sababu zina madhara.

Alitaja baadhi ya madhara ya kiafya yanayosababishwa na nguo hizo kuwa ni pamoja na magonjwa ya ngozi ikiwamo kansa.“Kwa hiyo tunatoa wito kwa Watanzania wasipende kuvaa nguo za ndani za mitumba zina madhara ndiyo maana tunaziondoa,” alisema na kuongeza kwamba nguo hizo zikishaondolewa zinateketezwa.Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa nguo hizo kutojihusisha na biashara hizo ili kuepuka hasara.Alisema msako huo unaendeshwa na maofisa wa shirika hilo nchi nzima.Aliongeza kuwa tangazo la kupiga marufuku nguo hizo lililotolewa kwenye vyombo vya habari na sasa zoezi linaloendelea ni utekelezaji wa kuondoa nguo hizo.“Utekelezaji huu ni kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya viwango ya 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani za mitumba.

Licha ya unafuu wa gharama za upatikanaji wa nguo za mitumba nchini, serikali kupitia shirika letu imepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo hizo, ikiwamo soksi, sidiria na nguo za kulalia kwa sababu zina madhara kwa mtumiaji," alisema.Agizo hilo linahusisha nchi nzima, kwani mara nyingi nguo za ndani za mitumbazimekuwa zikitumiwa na jinsia zote mbili, lakini wanawake ndio wameonekana kuwawateja wakubwa wa nguo hizo wao.Wakizungumza wakati wa zoezi la kuondoa nguo hizo, baadhi ya wananchi waliunga mkono hatua hiyo wakisema pamoja na kuvutiwa na unafuu wa bei, lakini madhara yake ni makubwa.
NGUO%20ZA%20NDANI%20MITUMBA.jpg
 

Attachments

  • NGUO%20ZA%20NDANI%20MITUMBA.jpg
    NGUO%20ZA%20NDANI%20MITUMBA.jpg
    3.4 KB · Views: 28
ila kuvaa chupi ya mtumba ni uzembe maana kariakoo chupi mpya zipo unapata kwa buku tu

ndo maana magonjwa ya kina mama hayaishi kila kukicha
 
kazi nzuri TBS, siku nyingine hakikisheni haziingii nchini na sio kungojea zije ndio mfanye uvamizi wa kuziondoa, kinga ni bora kuliko tiba!
 
Huwa sipendi kuona demu anavaa hizi chupi za mitumbani au hata chupi iliyochoka.

Ili kuwaelimisha Psychologically ni kumfanyia shopping ya vyupi 10 na vijizawadi vingine tu ila lengo ikiwa kumbadilisha kimawazo kuhusu vyupi vya mtumbani.

It's very dangerous kwa watu wetu.
 
Huwa sipendi kuona demu anavaa hizi chupi za mitumbani au hata chupi iliyochoka.

Ili kuwaelimisha Psychologically ni kumfanyia shopping ya vyupi 10 na vijizawadi vingine tu ila lengo ikiwa kumbadilisha kimawazo kuhusu vyupi vya mtumbani.

It's very dangerous kwa watu wetu.
Ni wazo zuri..sasa kwa sisi wanaume na mifumo dume yetu ya kibantu wanaume wangapi wanaweza kuinama au kuingia dukani kuchagua kyupi cha mpendwa wake..mtihani uko hapo ila tukiamua kubadilika inawezekana.

Hongera kwa kuliona i hope wewe ni mfano hai!
 
Hivi unaanzaje kuvaa nguo ya ndani ilovaliwa na mtu mwingine???? Big noo
 
Ni wazo zuri..sasa kwa sisi wanaume na mifumo dume yetu ya kibantu wanaume wangapi wanaweza kuinama au kuingia dukani kuchagua kyupi cha mpendwa wake..mtihani uko hapo ila tukiamua kubadilika inawezekana.

Hongera kwa kuliona i hope wewe ni mfano hai!
Mzee mbona ni kawaida sana kumnunulia mwenza nguo za ndani, mimi tangu nimeoa nguo za ndani za wife nanunua Mimi, ugumu haupo Bali tu ni mazoea
 
Back
Top Bottom