Tani moja ya Mitumba yaondolewa Sokoni

Tani moja ya Mitumba yaondolewa Sokoni

Joined
Sep 17, 2018
Posts
7
Reaction score
14
Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wameondoa kwenye soko zaidi ya tani moja ya nguo za ndani za mitumba ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa shirika hilo la kuhakikisha nguo hizo hazitumiwi na Watanzania.

Operesheni ya kuondoa nguo hizo ilifanyika mwishoni mwa wiki katika Soko la Tandika, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo, Mkaguzi wa TBS, Emmanuel Saimon, alisema hatua hiyo ni mwendelezo wa mikakati ya shirika ya kuondoa nguo hizo kwenye soko kwa sababu zina madhara kiafya.

Alisema miongoni mwa malengo ya uwapo wa shirika hilo ni kulinda afya za walaji, hivyo wanaondoa nguo hizo kwenye soko kwa sababu zina madhara.

Alitaja baadhi ya madhara ya kiafya yanayosababishwa na nguo hizo kuwa ni pamoja na magonjwa ya ngozi ikiwamo kansa.“Kwa hiyo tunatoa wito kwa Watanzania wasipende kuvaa nguo za ndani za mitumba zina madhara ndiyo maana tunaziondoa,” alisema na kuongeza kwamba nguo hizo zikishaondolewa zinateketezwa.Alitoa wito kwa wafanyabiashara wa nguo hizo kutojihusisha na biashara hizo ili kuepuka hasara.Alisema msako huo unaendeshwa na maofisa wa shirika hilo nchi nzima.Aliongeza kuwa tangazo la kupiga marufuku nguo hizo lililotolewa kwenye vyombo vya habari na sasa zoezi linaloendelea ni utekelezaji wa kuondoa nguo hizo.“Utekelezaji huu ni kwa mujibu wa matakwa ya sheria ya viwango ya 2009 inayozuia matumizi ya nguo za ndani za mitumba.

Licha ya unafuu wa gharama za upatikanaji wa nguo za mitumba nchini, serikali kupitia shirika letu imepiga marufuku biashara ya uuzwaji wa nguo hizo, ikiwamo soksi, sidiria na nguo za kulalia kwa sababu zina madhara kwa mtumiaji," alisema.Agizo hilo linahusisha nchi nzima, kwani mara nyingi nguo za ndani za mitumbazimekuwa zikitumiwa na jinsia zote mbili, lakini wanawake ndio wameonekana kuwawateja wakubwa wa nguo hizo wao.Wakizungumza wakati wa zoezi la kuondoa nguo hizo, baadhi ya wananchi waliunga mkono hatua hiyo wakisema pamoja na kuvutiwa na unafuu wa bei, lakini madhara yake ni makubwa.

Mmoja wa wakazi wa Tandika, Joyce Joseph, aliunga mkono hatua hiyo na kuwataka Watanzania watafakari mara mbili kabla ya kuingia mfukoni na kutoa kununua nguo.

“Fikiria leo hii unavaa nguo yako ya ndani na baada ya kuichoka unampa ndugu yako utajisikiaje?” Alihoji.

Muungwana Blog
 
Back
Top Bottom