Watu wengi hawajalipwa, muda sio mrefu mama yangu amabae yupo wilaya ya mkuranga, amenipigia na amesema hakuna mkulima hata mmoja aliepata hela yake, sio wa kilo chache au nyingi. Mimi pia nipo huku kusini, watu wengi hawajalipwa. Kwa mfano wilaya ya nanyumbu watu pekee ambao wanaendelea kulipwa tena kwa kusuasua ni wa mangaka pekee, ni wale wa kilo chache tu. Lkn pia ninaofisi Tandahimba, huko pia hali mbaya zaidi afadhali hata nanyumbu. Kama hiyo haitoshi, Jana wananchi walishinda ktk ofisi ya mkuu wa wilaya ya Masasi, wakishinikiza kulipwa Pesa zao. Mmoja wa mkulima alisema yeye anadai Pesa zake za kilo 466, tu, ambayo wala haihitaji uhakiki. Habari ndo hiyo.