esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 555
SERIKALI imesema hadi ku kia Desemba 31 mwaka 2018, korosho zilizokuwa zimenunuliwa na ziko kwenye maghala makuu ni tani 197,132.9. Sambamba na hayo, akaunti 131 zimefungiwa na serikali kutokana na kuthibitika kuwa wamiliki wa akaunti hizo, wanafanya biashara ya korosho nje ya mfumo wa stakabadhi ghalani, maarufu kangomba.
Hayo yameelezwa jana jijini hapa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema akaunti hizo wamezifungia baada ya kujiridhisha kwa asilimia 100 kuwa wamiliki wake ni watu wanaofanya biashara ya kangomba. “Korosho zote za wakulima zimenunuliwa, na nikisema hivyo namaanisha korosho zilizoko kwenye maghala makuu na hizi hazihusishi zile ambazo bado ziko mikononi mwa wakulima au zilizoko kwenye maghala ya vyama vya ushirika.
“Aidha tumekuwa tukifanya uhakiki wa wakulima kabla ya kuwalipa na kama tulivyokuwa tumeainishiwa kuwa serikali itanunua korosho ya mkulima na atalipwa mkulima. “Watu hawa walikuwa wanafanya biashara kinyume na sheria, hawalipi kodi, wanawanyonya wakulima, watu wa kangomba ambao tumewabaini akaunti zao tumezifreeze, na hawatarudishiwa korosho zao na wala hawatalipwa kwa sababu hawa ni wahujumu wa uchumi.
” Hasunga alisema kwa sasa uhakiki unaendelea na kuwa mpaka Desemba 31 mwaka jana, tayari vyama 466 kati ya vyama 504 vilivyopo mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na kati ya vyama 617 vilivyopo nchi nzima. Kuhusu fedha zilizolipwa, Hasunga alisema fedha ambazo serikali imepeleka benki zaidi ya Sh bilioni 242.38 huku fedha zilizoingia moja kwa moja kwenye akaunti za wakulima na Sh bilioni 223.551.
Alisema fedha ambazo hazijawakia wakulima pamoja na kuwa zimepelekwa benki kutokana na matatizo mbalimbali, yakiwemo ya kutoona majina yaliyopelekwa ili walipwe na yale yaliyoko kwenye akaunti ni Sh bilioni 9.8. “ Kuna fedha ambazo pamoja na kupelekwa benki, mfumo wa benki umeshindwa kutuma fedha na Sh bilioni 9.8 kutokana na sababu ikiwa ni majina yanatofautiana na majina ambayo yameletwa kutoka kwenye vyama vya ushirika. Mfano jina lililoletwa na chama cha ushirika linasema alipwe Abdalla Hussein Abadallah lakini jina la mwenye akaunti linaonesha na Abadala Husein Mwinijuma benki haiwezi kumlimpa.
“ Hivyo wakulima wametakiwa kufanya marekebisho ya taarifa zao na kuthibitishwa kuwa wao ndio wamiliki wa akaunti hizo watalipwa kabla ya serikali haijakia maamuzi mengine,” alisema. Aidha, Hasunga alisema pia akaunti 1,604 zimezuiliwa mpaka hapo itakapokamilika uhakiki wa kujiridhisha kama wamiliki wa akaunti hizo sio watu wa kangomba, huku 225 zikipelekwa kwenye uhakiki zaidi.
Hasunga alisema mpaka Desemba 31 mwaka jana, wakulima waliokuwa wamelipwa ni 158, 505, huku baadhi ya wakulima ambao huzalisha kilo 1,500 kwa mwaka ambao thamani ya korosho zao ni Sh bilioni 159.69 wamepelekwa kwenye uhakiki wa pili. “ Uhakiki wa awali ulikuwa ni wakulima wanaozalisha chini ya kilo 1,500, lakini hawa wanaozalisha zaidi ya hapo ndio ambao uhakiki wao unakwenda sambamba na kutuonesha shamba ambalo amevuna kiasi hicho cha korosho ili tujiridhie kuwa ni mkulima na sio kangomba.
Aidha, serikali inawaalika wenye viwanda vya kubangua korosho ili kusaidia kufanya kazi hiyo na si kwa ajili ya kununua korosho gha. Hasunga alisema kwa sasa wameingia mkataba na baadhi ya wamiliki wa viwanda kwa ajili ya kubangua korosho na kuwa kamwe hawauzi korosho gha. “Tumeanza kubangua korosho baada ya kuingia mikataba na baadhi ya viwanda, hapa hatuwauzii, Bodi ya Mazao ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko ndio itakayofanya kazi ya kutafuta masoko ya korosho iliyobanguliwa.
Aliongeza: “Hawa wenye viwanda ndio tunaowakaribisha kwenye meza ya majadiliano ili waje kutusaidia kubangua tu na wakimaliza kazi yao tunawalipa gharama ya kazi hiyo. Hivyo tunaowaita ni wenye viwanda na si wanunuzi wa korosho gha. Katika hatua nyingine, Hasunga alielezea mikakati ya wizara iliyopo katika kuhakikisha wanaongeza uzalishaji katika zao la korosho, kwa kuongeza mikoa ya uzalishaji kutoka saba iliyopo hadi mikoa 17.