Yeye ndiye aliyepandikiza mbegu nzuri ya Watanzania kukataa kuburuzwa na kusimamia haki zao, ambapo kupitia kwake mwanga wa ukombozi katika siasa za vyama vingi ulienea kote nchini.
Jambo hili alilifanya zaidi hapa Kigoma, kwa maana nyingine, Kigoma ndio mkoa wa kwanza kuonesha kwa vitendo utayari wa kupokea vyama vingi nchini, yote ni kwa sababu ya kazi ya ‘Uamsho’ ya Dkt. Kabourou. Ni mbegu hii ya mageuzi aliyoipanda ndiyo iliyofanya wakati flani Mkoa wote wa Kigoma ukawa na idadi kubwa ya wabunge kutoka vyama vya upinzani.
Namkumbuka sana Dkt. Kabourou, nilipenda sana jina lake. Nilipenda alivyojiamini. Poleni wana Kigoma na watanzania kwa ujumla.
Lakini tutoapo wasifu wa marehemu, basi tusiongezee na hisia zetu. Unasema kupitia yeye ukombozi wa vyama vingi ulienea chini. Na kuna sehemu unasema yeye alikuwa mbunge wa kwanza wa upinzani basi ni vema ukasema kwa Kigoma.
Ninachokumbuka vuguvugu la vyama wakati huo kabla halijaanza, kuna watu kama Mtikila waliokuwa wanaleta vuguvugu, hata mfumo wa vyama vingi kuanzishwa. Kuna akina Mabere Marando, Kasanga Tumbo, Kuna Mzee Mapalala, Mzee Mtei, na wengineo ambao hawa waliongoza kuweka vuguvugu la kudai vyama vingi bila kumsahau Oscar Kambona. So unaposema kupitia kwake mwanga wa ukombozi ulienea nchini je waliokuwepo kabla ya yeye kuja toka Marekani?
Pia kudai Kigoma ilionesha mfano si kweli kwani wakati huo kuna majimbo yaliyotoa wabunge wa upinzani, kama Kilimanjaro, Arusha, Mara amabako Balozi Ndombho alishinda kwenye jimbo la Baba wa taifa Mwl Nyerere kama mpinzani. Akina Marando walikuwa wabunge pia wote toka upinzani.
Mhe. Zitto tueleze historia ila tusipindishe histroria ili kukuza mambo.
Wakati huo wasomi wengi walirudi nchini. Nakumbuka Cheyo Chama chake kilitikisa maeneo ya Shinyanga hasa huko Bariadi. Sasa, ukisema alikuwa mbunge wa kwanza bila kuchanganua wapi inaonesha kama yeye ndiye alikuwa mwanamageuzi wa kwanza Tanzania.
Namkubali, na nilimpenda sana. Ila tuwetunaweka historia sawa. Si kueleza kwa hisia binafsi. Asante kwa mengine yote uloeleza kikubwa ni kumuenzi kwa kile alichosimamia.
Mungu amlaze mahala pema. Amen!