Tangu siku hiyo huwa sina hamu na siku ya Valentine !!

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,520
764
::
Wakati huo nilikuwa kidato cha tano.Mkoani Mara katika shule maarufu Musoma tech.Kwa wale ambao wanajua shule hiyo watakubaliana nami juu ya vurugu,ugomvi na hata uhuru kupita kiasi waliokuwa nao wanafunzi miaka kadhaa iliyopita.Kwa wakati huo palitokea upungufu wa chakula shuleni tukaawacha O-level wakitumia salio kidogo huku mpishi maarufu "Matogoro" akiendeleza mgao wa chakula kwa hesabu.
::
Baada ya kufunga shule bila kutegemea sikuwa na pesa wala mawasiliano na nyumbani.Mawasiliano ya simu kama Mpesa hayakuwepo ukijitahidi sana unatumia EMO kwa posta.Hivyo nilienda kwa jamaa mmoja mwenye familia yake,mke na watoto wawili.
::
Sikuwa mgeni sana nyumba hii,nilipenda watoto wa nyumba hii,kuwasimulia hadithi na nilikuwa mpole.Nilipofika nilipokelewa na House girl kwa tabasamu zito na kuniambia "Yaani! Mama atafurahi leo kila anakusifu,yule kijana mpole,mcheshi na anapenda watoto sijui atakuja lini"
Naam,alinipokea vema
::
Ukweli ni kuwa yule Mama alikuwa akinipenda kuliko hata ndugu yake au wa mume wake,japo sikuwa na udugu na hiyo familia.Mara nyingi sana alinitembelea shuleni kwa gari lake,alinipa pesa ya matumizi shuleni,na alipenda sana kila weekend niende kwake,japo sikufanya vile.
::
Wiki moja nikiwa pale,,Valentine day ilifika.Na mama mwenye nyumba aliamka na alijikwatua vema na mume wake,,ambaye ndiye mwenyeji wangu katika nyumba ile (tulitoka kijiji kimoja) alimuaga mkewe akimwambia atarudi kumchukua waende Valentine.Alituaga muda wa saa 4 asubuhi
::
Tulibaki mimi,house girl,mama mwenye nyumba na watoto.
Baada ya muda house girl aliondoka kwa Tax na kwenda walikoagizwa na mama mwenye nyumba.Nilibaki na mama pale huku akinitania "Hivi huwa unajua kuongea? Sijawahi kuona kijana mwenye aibu kama wewe!" Ni kweli hulka yangu hunifanya niwe mkimya niwapo ugenini!
::
Tuliendelea kubaki pamoja,akinipa vyakula vinywaji na alitaka kuninywesha nikakataa.Wanawake! Acha mwanamke aitwe mwanamke! Muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kunichezea,kunikimbiza na cha ajabu kwangu,alianza kunidadisi kama amependeza au vipi!
::
Nilipoona dalili hizo,mm! Niliaga kwenda kutembea mitaani lakini alinikatalia akisema nisubiri house girl arudi,,niliendelea kuona maigizo mara abadili nguo,mara ajaribie kwangu staili za busu!
Ilipofika saa 12 jioni house girl alirudi na watoto,,na mama alimkumbuka mumewe ambaye alimuahidi atarudi alikuwa hajarudi.
::
Aliendelea kumsubiri hadi ilipofika saa 3 usiku tunaenda kulala alikuwa mpweke.
Usiku wa saa 5 usiku niligutuka usingizini baada ya kusikia mtu anagonga mlangoni na nilipofungua mlango wa chumba alikuwa mama mwenye nyumba.Du! Aliniziba mdomo na kunivuta kuelekea chumbani kwake,nilienda kama mbuzi aendae machijoni!
::
Tulipofika chumbani,alianza kunipapasa,kunirusha kitandani,,lakini nilianza kujifaragua na kutaka kutoka mikononi mwake.
Ile nimemsukuma tu,na kutaka kutoka alinivuta,nikainama kama nimetazama uvunguni
::
Loo! Mumewe alisikika "Mnafanya nini nyinyi".Kwa wepesi wa ajabu Mama alijibu "Yaan mume wangu,yule panya amenirukia kitandani,,ikabidi nimuite huyu kijana,ametafuta hadi amechoka"
Mume wake akisema "Pole sana mke wangu,,pole sana kijana" Tuliendelea kumtafuta panya huyo wa uongo na kweli.
Alipokosa,niliwaacha na ugomvi wa kindoa mke akachachamaa alikuwa wapi Valentine yote na kwa nini alimdanganya.
Tangu siku hiyo,sina hamu na Valentine
=
Tags
Lisa Mtambuzi saudari@Zion daughter Purple@Lara 1 Preta@Rich woman@Tamatheo@Mentor na wote wenye Valentine wao
 
Last edited by a moderator:
Hahaaa kwahio we ndo panya..lol..mama ana mitego!! Ila sio ndo ukose hamu bwana ,nadhan ni long ago na yule si mkeo useme atakusumbua..huwez kuwanyima raha familia na mpenzio/wapenzio kiisa ya old school story bana! Jiachiee nothing lasts foreve..life is too short focus n the future..past is past.. Unless ktk hii story bas uwe una date na mke wa mtu,so waogopa kufumaniwa ila kama ni vingine,si sababu ya kuchukia Va-day!ok?
 
Hahahahahahahahaha! Tetra, umenifurahisha sana, Basi nakuomba leo mimi nikutoe Valentine Tukapate chakula cha jioni pale JD Hotel, Posta! Ila kwa masharti ya kutochukua chumba. Loh!
 
Hahahahahahahahaha! Tetra, umenifurahisha sana, Basi nakuomba leo mimi nikutoe Valentine Tukapate chakula cha jioni pale JD Hotel, Posta! Ila kwa masharti ya kutochukua chumba. Loh!

Mmmm naogopa kibano cha mzee,,hii Valentine itabidi nitulie kwangu kabisaaa
 
Hahaaa kwahio we ndo panya..lol..mama ana mitego!! Ila sio ndo ukose hamu bwana ,nadhan ni long ago na yule si mkeo useme atakusumbua..huwez kuwanyima raha familia na mpenzio/wapenzio kiisa ya old school story bana! Jiachiee nothing lasts foreve..life is too short focus n the future..past is past.. Unless ktk hii story bas uwe una date na mke wa mtu,so waogopa kufumaniwa ila kama ni vingine,si sababu ya kuchukia Va-day!ok?
Swts
am single but kila nikikumbuka yaliyonitokea mm! nahofu may be hata hawa ma single wengine wanaweza kugonganisha scania Historia ikajirudia.Happy Valentine with your loved one
 
Last edited by a moderator:
Mie sijawahi ona maana ya hii siku kwa kweli.Ni wafanyabiashara wameikuza tu kwa faida yao binafsi..Ukizingatia majuto huwa yanakuwa mengi kuliko furaha.
 
Dah pole sana kijana wa "ALLIANCE"..
Ila wengine tukikutwaga na maswahibu kama hayo tunashukuru zali limetuangukia......
 
Mie sijawahi ona maana ya hii siku kwa kweli.Ni wafanyabiashara wameikuza tu kwa faida yao binafsi..Ukizingatia majuto huwa yanakuwa mengi kuliko furaha.
Zion Daughter
Yaani kila ikitajwa mie moyo mbio,,hamu iliniishia MAY BE wenye wapendwa wao wanaelewa maana yake
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom