Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,673
- 149,860
Nimeona kupitia taarifa ya habari ya ITV saa 2 usiku huu kuwa sasa Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi imerasimishwa kuwa ni siku ya usafi kisheria kupitia Tangazo la Serikali namba 139/2016 la tarehe 23/04/2016 na mtu yoyote ambae atakiuka agizo hilo atawajibika kulipa faini ya shilingi 50,000 (na kama sikosei kuna kifungo pia).Makampuni ambayo hayatashiriki katika usafi nayo yana adhabu yake ambayo ni kubwa zaidi.
Taarifa hii imetolewa na Naibu Waziri wa Mazingira,Luhaga Mpina na hii tunaambiwa ni sheria ya mazingira.
Sasa wadau,hasa wataalamu wa sheria,jambo hili ni sahihi kisheria?
Kama haitoshe,kuna sehemu abiria wameshushwa kutoka kwenye magari na wanajeshi ili wafanye usafi!!