TANGAZO LA MDAHALO WA KATIBA - Changamoto za Mchakato wa Katiba mpya

Neiwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
728
633
TANGAZO LA MDAHALO WA KATIBA


Muungano wa Asasi za Kiraia Tanzania umeandaa Mdahalo wa wazi kuhusu Changamoto za Mchakato wa Katiba mpya.

Mdahalo huo utafanyika tarehe 31 /5/2014 katika Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 Jioni.

Mdahalo huo utatangazwa moja kwa moja na vituo vya ITV, ABM Radio ya Dodoma, pamoja na Chuchu FM na Istiqama Radio za Zanzibar.
Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza Mdahalo huu kwa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.

Watoa Mada ni waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba: Prof. Mwesiga Baregu na Bw. Awadhi Ally Saidi.

Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata katiba mpya inayokidhi maslahi ya watanzania.


Wote Mnakaribishwa !!!
 
Inatutaidia nn?

Wewe aminangalo si ndio yule mlokole uliyekuwa unatupa hapa JF, taarifa za kuuaga mwili wa Askofu Mkuu Moses Kulola, kule Temeke, mwishoni mwa mwaka jana !!!???? Unafikiri tumesahau? Wewe ni mlokole wa ajabu, mlokole gani anaweza kuwa katika Chama Cha Mafisadi, na kutetea ufisadi wa Interahamwe kwa nguvu zake zote, kama unavyofanya wewe? Inakubidi uchague moja kati ya ufisadi au ulokole. SHAME!!!!!!
 
tangazo la mdahalo wa katiba


muungano wa asasi za kiraia tanzania umeandaa mdahalo wa wazi kuhusu changamoto za mchakato wa katiba mpya.

mdahalo huo utafanyika tarehe 31 /5/2014 katika ukumbi wa blue pearl hotel, ubungo plaza, jijini dar es salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 jioni.

Mdahalo huo utatangazwa moja kwa moja na vituo vya itv, abm radio ya dodoma, pamoja na chuchu fm na istiqama radio za zanzibar.
Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza mdahalo huu kwa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.

watoa mada ni waliokuwa wajumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba: prof. Mwesiga baregu na bw. Awadhi ally saidi.

Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili kuhakikisha kuwa tanzania inapata katiba mpya inayokidhi maslahi ya watanzania.


wote mnakaribishwa !!!

asante kwa taarifa. Tutajumuika kushiriki
 
Back
Top Bottom