Tangazo la kukaribisha maombi ya mashamba ya kulima Mkonge

Vogoso

Member
Mar 23, 2019
44
43
Habari wanajamvi nimeona tangazo kutoka BODI YA MKONGE TANZANIA wakitoa taarifa ya kuwa wanakodisha mashamba ya MKONGE Kwa wanachi wanaohitaji.

TANGAZO LA KUKARIBISHA MAOMBI YA MASHAMBA YA KULIMA MKONGE

1.0 Utangulizi

Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB) inaendelea kupokea maombi ya mashamba kutokakwa wananchi wenye nia ya kuendeleza kilimo cha mkonge kwa wakulima wadogonchini. Kwa awamu ya kwanza mashamba yanayokusudiwa kugawiwa kwa wakulimawadogo ni mashamba ya Hale Estate, Magoma Estate, Magunga Estate, NgombeziEstate na Mwelya Estate yaliyopo Wilaya za Handeni na Korogwe ambayoyanamilikiwa na Bodi ya Mkonge Tanzania.

2. Utaratibu wa Maombi ya mashamba

Waombaji wote watatakiwa kujaza fomu maalum inayopatikana katika ofisi zaBodi ya mkonge na au kupitia tovutihttps://www.kilimo.go.tz/index.php/en/resources/view/fomu-ya-kuomba-kulima-shamba-la-mkonge. Baada ya kujaza, fomu irejeshwe katika ofisi za Bodi yaMkonge Tanzania zilizopo Kiwanja Na.65 jengo la Mkonge (Mkonge House),Barabara ya Uhuru/Usagara,Tanga Jiji, kabla au ifikapo tarehe 01 Januari2021 au tuma kwa anuani ifuatayo:

Mkurugenzi mkuu,
Bodi ya Mkonge Tanzania,
S.L.P 277 Tanga.
Barua pepe: dg@sisalboard.go.tz
Kwa maelezo zaidi: Edger Msovela 0652 956 444 au Olivo Mtung’e 0738 754336

3. Masharti ya uombaji
Masharti ya uombaji wa mashamba ni kama yalivyoainishwa kwenye fomu yamaombi. Waombaji wote waliowasilisha maombi Bodi ya Mkonge kwa njia yabarua wanaelekezwa kuwasilisha upya maombi yao kwa utaratibu wa kujazafomu. Inasisitizwa kuwa maombi yote ya shamba yatakayowasilishwa auyaliyokwishawasilishwa nje ya utaratibu wa ujazaji wa fomuhayatashughulikiwa. Maombi yatashughulikiwa kwa utaratibu wa “Wa kwanzakuomba wa kwanza kushughulikiwa” (first in first served).

Limetolewa Na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Bodi ya Mkonge Tanzania,
S.L.P 277,
TANGA.

Natamani niwe miongoni mwa watakaofanikiwa kuipata shamba, Ila sina uzoefu na kilimo cha Mkonge katika:-
1. Gharama za kualima na kuhudumia shamba.
2. Uendeshaji na usimamizi WA shamba.
3. Namna ya kuuza(soko) na faida.
4. Muda unaotumika hadi kuanza kuvuna na je huchukua muda gani mmea kuzeeka na kuwa haifai kuendelea na kilimo (kuchakaa)

Kwa anayefahamu naomba anifahamishe na kama kujambo nimeliacha anaweza kuongezea ili wanajamvi tupate ujuzi zaidi.

Asante

Sent from my MI 8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Mo anakuambia hiyo Ni dhahabu nyeupe ...na yeye ndio mnunuzi mkuu was hiyo kitu
 
Katika mazao ya Kilimo Mkonge ni zao mojawapo ambalo halina complications katika kulilima. Ni zao ambalo kwa hesabu za bodi ya korosho Unaweza kuuaga umasikini.

Kuna mabandiko humu kuhusu hiki kilimo. Unaweza kupata taarifa zote za kilimo cha Mkonge. Jaribu ku search kilimo cha Mkonge humu JF utapata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom