Tangazo la ajira jeshi la polisi

MSATULAMBALI

Senior Member
Apr 1, 2012
187
55
TANGAZO LA AJIRA

Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.

Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.

Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.

Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku.

Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.

Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.

A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI

Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.

Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.

Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.

Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.

Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.

Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.

B: MASHARTI KWA MWOMBAJI

Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.

Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.

C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:

Ofisi ya Mkuu wa shule

Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu

Pata fomu hapa(sel-form)

Imetolewa na;

Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,

Makao Makuu ya Polisi,

S.L.P 9141,

DAR ES SALAAM.
 
Mnatangaza nafasi hizi za upolisi kwa faida ya watanzania wote au ni kwa faida ya CCM tu?
Maana mwenye macho aambiwe tizama....jeshi letu la polisi ni ccm,rushwa na kuwabambikizia
watu kesi....all in all hii ni kazi ya lawama kwa jamii na hii ni kazi ya maana na pongezi kwa ccm.
 
Yah!!kwa mwaka huu form 6 walivochemsha,watawapata wengi tu.
 
sijui niahilishe MBA yangu ili nikawe mamuruki kwa hawa policcm, maana hakuna idara inanikera ktk nchi hii kama hawa bendera, upepo utakako vuma tuu wapo
 
jamani mimi nina 29 yrs , bado tu mtanichukua?? lakini nipo tayari kabisa kabisa kabisa afande..
 
Mnatangaza nafasi hizi za upolisi kwa faida ya watanzania wote au ni kwa faida ya CCM tu?
Maana mwenye macho aambiwe tizama....jeshi letu la polisi ni ccm,rushwa na kuwabambikizia
watu kesi....all in all hii ni kazi ya lawama kwa jamii na hii ni kazi ya maana na pongezi kwa ccm.

i hate this kind of thinking!

anyway, wahenga walisema:
"Be the change you want to see around u"... badala ya kuponda why not join in the fight against the practices so that one day we can have a fair and helpful police force?

Mambo mengine, get to know why they do the things they do b4 u ropoka...believe me, i dont like how the police are working na mimi baadhi ya hayo mambo yameshanikuta ila siyo sababu ya kuwatukana polisi wote maana najua kuna those who are fighting against the status quo..bt ts a long fight!!
ni kama ukisema watu wasigombee ubunge since ubunge ni uccm..ni wizi, ni hujuma ni ufisadi...what will u say of the fighters like Zitto et al? do u want to tell me there are no people like them in the police force?

oh oh...ama u have worn the clothes of uchama in the sense that anything wrong hapenning gets thrown to ccm's faults? what hav u as a citizen done? mshikachuma
 
Last edited by a moderator:
sijui niahilishe MBA yangu ili nikawe mamuruki kwa hawa policcm, maana hakuna idara inanikera ktk nchi hii kama hawa bendera, upepo utakako vuma tuu wapo

haha. buhange usihamie kama mamluki bana..hamia uko ili uwe part of the change u want to see in the system. i was to join the force too bt something better came up...

jamani mimi nina 29 yrs , bado tu mtanichukua?? lakini nipo tayari kabisa kabisa kabisa afande..
mkaliwakitaa, last year kulikuwa na employment ya professionals, sijui mwaka huu vipi labda utumie fursa hiyo...
 
Last edited by a moderator:
i hate this kind of thinking!

anyway, wahenga walisema:
"Be the change you want to see around u"... badala ya kuponda why not join in the fight against the practices so that one day we can have a fair and helpful police force?

Mambo mengine, get to know why they do the things they do b4 u ropoka...believe me, i dont like how the police are working na mimi baadhi ya hayo mambo yameshanikuta ila siyo sababu ya kuwatukana polisi wote maana najua kuna those who are fighting against the status quo..bt ts a long fight!!
ni kama ukisema watu wasigombee ubunge since ubunge ni uccm..ni wizi, ni hujuma ni ufisadi...what will u say of the fighters like Zitto et al? do u want to tell me there are no people like them in the police force?

oh oh...ama u have worn the clothes of uchama in the sense that anything wrong hapenning gets thrown to ccm's faults? what hav u as a citizen done? mshikachuma
tangu nijiunge na huu mtandao ths z th 1st tym a mit a ril great thnkr. great bro/sis, hii k2 ya kuwaza kishabiki i ril hate t. lets b positive
 
Last edited by a moderator:
Mnatangaza nafasi hizi za upolisi kwa faida ya watanzania wote au ni kwa faida ya CCM tu?
Maana mwenye macho aambiwe tizama....jeshi letu la polisi ni ccm,rushwa na kuwabambikizia
watu kesi....all in all hii ni kazi ya lawama kwa jamii na hii ni kazi ya maana na pongezi kwa ccm.

umenena mkuu kwani hata sasa jeshi la polisi haliko kwa ajili ya kulinda na kutetea haki za raia bali kupokonya na kunyang'anya raia haki zao. Naweza kusema na nadhini wengi watakubaliana nami kwamba jeshi la polisi liko kwa ajili ya maslahi ya chama cha magamba(chukua chako mapema£ccm).
 
Let say something here akika vijana wamekuwa wakiingiza maswala ya itikadi za vyama kwenye maswala ya maendeleo.tunatakiwa tutibu tulipo umia na co kuangali mahali tulipojikwaa aitatusaidia .let us change
 
Naona kama ubaguz hv!yaan wale wa form four hawana elim?au hawa wanaenda kusoma uafsa?kwel nakubal ya wahenga"hatamu ikishikwa pund lazima/shartiaende"bas form4 iondolewe kwenye hat za ajira,maana that is unthinking ability.
 
baadhi ya wana jf mmezidisha uitikadi wa chama badala ya uzalendo kila jambo mnahusisha itikadi za chama, too much!
 
inaonekana huijui ccm'kama waijua basi wewe ni ccm.tabia za ccm hizo
 
umenena mkuu kwani hata sasa jeshi la polisi haliko kwa ajili ya kulinda na kutetea haki za raia bali kupokonya na kunyang'anya raia haki zao. Naweza kusema na nadhini wengi watakubaliana nami kwamba jeshi la polisi liko kwa ajili ya maslahi ya chama cha magamba(chukua chako mapema£ccm).

kama ni hivyo basi sehemu zote zilipo kambi/line za polisi wakati wa uchaguzi wangeshinda wagombea wa ccm...WAS IT SO BROTHER!??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom