Kutoka
www.necta.go.tz:
Toleo la Septemba[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style], [/FONT][/FONT]
2014
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]PICHA YA MTAHINIWA
[/FONT][/FONT]
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
CM
FOMU YA OMBI LA CHETI MBADALA (REPLACEMENT CERTIFICATE)
A. SOMA MAELEKEZO YAFUATAYO KABLA YA KUJAZA FOMU HII.
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](i) Hakikisha kwamba taarifa utakazoandika katika fomu hii ni sahihi. Iwapo tarifa uliyoandika haitakuwa sahihi, cheti mbadala hakitaandaliwa.
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](ii) Gharama ya cheti mbadala ni Tsh. [/FONT][/FONT]
100,000/=[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]. [/FONT][/FONT]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](iii) Ombi la cheti mbadala litapokelewa baada ya miezi mitatu (03) kupita tangu kutangazwa gazetini kwa upotevu wa cheti cha awali.
(iv) Mchakato wa uchunguzi utafanyika katika kipindi cha siku thelathini (mwezi mmoja) tangu kupokelewa kwa ombi la cheti mbadala ambapo Jeshi la Polisi (kitengo cha uchunguzi wa picha) litahusika katika kukamilisha uchunguzi huo.
(v) Cheti mbadala kitatolewa mara moja tu.
(vi) Iwapo cheti kilichopotea kitabainika kutumika katika soko la ajira au mafunzo na mtahiniwa akabainika kushiriki katika kulidanganya Baraza la Mitihani katika kumwezesha mtumiaji wa cheti hicho kukitumia wakati sio chake, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu wote waliohusika katika udanganyifu huo.
(vii) Hakikisha kwamba unavyo viambatisho vifuatavyo:
[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]2
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]Tangazo la gazeti la upotevu wa cheti (taarifa muhimu kwenye tangazo hilo ni Jina la mtahiniwa, Namba ya mtihani, aina ya mtihani, mwaka wa mtihani, jina la shule, picha ya mtahiniwa na mahali cheti kilikopotea), Hati ya polisi ya upotevu wa cheti, Picha (Passport size) utakayobandika kwenye fomu ya ombi la cheti mbadala, Nakala ya kitambulisho na Risiti halisi ya malipo.
Iwapo cheti chako kiliungua moto, kuharibiwa na mchwa, mafuriko, panya au kwa namna nyingine yoyote hutatakiwa kutangaza gazetini uharibifu huo bali utawasilisha vielelezo vilivyotajwa hapo juu pamoja na barua ya serikali ya mtaa wa eneo la tukio la moto au mafuriko yalipotokea. Iwapo yapo mabaki ya cheti husika utatakiwa kuwasilisha mabaki hayo Baraza la Mitihani.
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](viii) Baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu na malipo, tafadhali tuma au wasilisha fomu yenye viambatisho vilivyotajwa kwa [/FONT][/FONT]
Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania, S.L.P 2624 Dar es Salaam[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]. Fomu hii inapatikana katika tovuti ya Baraza ambayo ni:[/FONT][/FONT]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]www.necta.go.tz [/FONT][/FONT]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style][/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style][/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]Iwapo cheti kitatumwa kwa EMS, utapaswa kuongeza malipo kwenye gharama iliyotajwa kadri utavyoelekezwa na posta.
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]Malipo yafanyike kwenye mojawapo ya [/FONT][/FONT]
akaunti [FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]za [/FONT][/FONT]
NECTA [FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]zifuatazo: [/FONT][/FONT]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style] NBC 11103001074 BANK CORPORATE BRANCH
 NMB 2011100238 NMB BANK-BANK HOUSE
 CRDB 01J1013540000 CRDB BANK-TAWI LA
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]KIJITONYAMA. [/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]3 [/FONT][/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][/FONT][/FONT] 
B. MASHARTI YA KUOMBA CHETI MBADALA
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]Mwombaji wa cheti mbadala unatakiwa kutimiza masharti yafuatayo:
(a) Uwe ni mtahiniwa halisi uliyefanya mtihani na kutunukiwa cheti cha awali chenye picha kisha kikapotea, kuharibika au kuungua moto.
(b) Uwe mkweli, mwaminifu na mwenye dhamira ya kweli ya hitaji la cheti mbadala baada ya kutokuwa na cheti cha awali kwa sababu ya matukio yaliyotajwa katika kipengele (a) hapo juu.
(c) Picha yako itafananishwa na picha iliyotumika kufanya mtihani husika. Iwapo picha hizo hazitafanana, uchunguzi utafanyika ili kubaini ukweli wa tofauti hizo. Aidha, iwapo matokeo ya uchunguzi yatabaini kuwa aliyefanya mtihani huo ni mtahiniwa tofauti na wewe, basi itakuwa imethibitika kuwa ulikuwa unajaribu kujipatia cheti mbadala isivyo halali kinyume cha sheria. Hivyo, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yako.
(d) Cheti mbadala kitatumiwa na mtahiniwa husika tu katika ajira na mafunzo. Iwapo cheti kilichopotea (kwa waliopoteza vyeti) kitapatikana, cheti mbadala kirudishwe Baraza la Mitihani mara moja.
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](e) Uwe umetekeleza maelekezo yote yaliyoainishwa katika vipengele ([/FONT][/FONT]
i[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style])-([/FONT][/FONT]
iv[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]) hapo juu. [/FONT][/FONT]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style][/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]4
[/FONT][/FONT] 
C. KIAPO
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]Mimi
. nathibitisha kwamba taarifa nilizojaza katika fomu hii ni sahihi. Aidha, nitatekeleza masharti yote ya matumizi ya cheti mbadala kama yalivyoainishwa katika fomu hii. Iwapo nitabainika kuwa sikutoa taarifa sahihi na nikashindwa kutekeleza masharti ya matumizi ya cheti mbadala nichukuliwe hatua za kisheria.
Saini:
arehe:
.
[/FONT][/FONT]
D. TAARIFA ZA MTAHINIWA:
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](a) Jina kamili lililotumika katika mtihani
..
(b) Aina ya mtihani aliofanya (CSEE, ACSEE, GATCE, GATSCCE, DEE/DSEE, DTE, FTC, ADE)
.
(c) Mwaka wa mtihani
(d) Namba ya mtihani
(e) Anwani
(f) Simu
(g) Barua pepe
Cheti mbadala kitakabidhiwa au kutumwa kwa mtahiniwa husika tu. Mwakilishi hataweza kupewa cheti hicho.
i. Kiasi cha fedha iliyolipwa ni Tshs
.
.
Saini
Tarehe
ii. Cheti Mbadala kitumwe kwenye anwani ifuatayo au nikabidhiwe (jaza kipengele unachotaka kitumike):
[/FONT][/FONT][FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[/FONT][/FONT][FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]5 [/FONT][/FONT]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman]
[FONT=Times New Roman,Times New Roman][/FONT][/FONT] 
E. KWA MATUMIZI YA OFISI TU.
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style]
[FONT=Bookman Old Style,Bookman Old Style](i) Nathibitisha kupokea ombi hili na/pasipo viambatanisho vilivyotajwa:
Jina
Saini
arehe
(ii) Ombi limeshughulikiwa/halijashughulikiwa kwasababu
Jina:
Saini:
Tarehe:
[/FONT][/FONT]