Tangazo gani la biashara redioni au kwenye runinga uliwahi kulipenda sana?

Wasalaam,

Muziki au matangazo ya kibiashara ni vitu vinaweza kutukumbusha hazina ya muda na mambo mazuri tuliwahi kuwa nayo zamani

Binafsi siwezi kulisahau tangazo la dawa ya kuzibia pancha baiskeli..."Vipi Rambooo? Pancha banaa...pancha wakati kuna okoo..."...hapo niko pembeni ya mshua nafanya zoezi la hisabati tena vile vya maswali 40.

Wewe unakumbuka tangazo gani na linakukumbusha "moment" gani nzuri?
Tangazo la CRDB "hata safari iwe ndefu ya kilometer elfuuu,tunasonga mbele....... ,Yule manzi aliyeimba anaweza mtoa nyoka pangoni"
 
nayakumbuka matangazo mawaili

CRDB
tunasonga mbele kwa pamoja mafanikio yetu ya pamoja miaka 10 ya kuhudumia wateja wetu wa Tanzania, CRDB bank tunasinga mbeleeee

Vodacom Mpesa
Nifuraha nchi nzima, watanzania tunapounganishwa na huduma toka voda Mpesa inakufikia, tuma pesa kwa familia, hata kibiasha oooh tuma pesa na Mpesa

Tusker lager
Twende pamoja mimi na wewe bega kwabega ( Milele eeeeh) Huuu umoja wetuu (Aaah milele) twende pamoja, bega kwa bega, marafiki halisi, Bia bora tusker marafiki halisi
Huyu manzi aliyeimba hiyo kitu ya CRDB alitisha sana
 
Wasalaam,

Muziki au matangazo ya kibiashara ni vitu vinaweza kutukumbusha hazina ya muda na mambo mazuri tuliwahi kuwa nayo zamani

Binafsi siwezi kulisahau tangazo la dawa ya kuzibia pancha baiskeli..."Vipi Rambooo? Pancha banaa...pancha wakati kuna okoo..."...hapo niko pembeni ya mshua nafanya zoezi la hisabati tena vile vya maswali 40.

Wewe unakumbuka tangazo gani na linakukumbusha "moment" gani nzuri?
Hebu jitokezee ,simama,mbele ya watuuuuu,,,KIWI ,,,sijui ilikuwa mwaka gan vile ila lilikuwa Tangazo tamu sana aaa
 
nayakumbuka matangazo mawaili

CRDB
tunasonga mbele kwa pamoja mafanikio yetu ya pamoja miaka 10 ya kuhudumia wateja wetu wa Tanzania, CRDB bank tunasinga mbeleeee

Vodacom Mpesa
Nifuraha nchi nzima, watanzania tunapounganishwa na huduma toka voda Mpesa inakufikia, tuma pesa kwa familia, hata kibiasha oooh tuma pesa na Mpesa

Tusker lager
Twende pamoja mimi na wewe bega kwabega ( Milele eeeeh) Huuu umoja wetuu (Aaah milele) twende pamoja, bega kwa bega, marafiki halisi, Bia bora tusker marafiki halisi
Hilo la m pesa Dah
 
Tangazo la vifo RTD, baada ya taarifa ya habari saa saba kamili mchana
 
H
Tangazo la sabuni ya Revola, sabuni ya Ushindi na Chibuku
Nakubuka kibwagizo cha "ATC Hewani"
ahahaa 'mshindi sabuni mpya yeenye nguvu, yenye kutakasa kuliko zoote ,mshindii yeyee'. Daah kitambo sana
 
  • Thanks
Reactions: ram
Jambo aisee, waliua😂. “Mimi naitwa jambo ndogo, mimi naitwa jambo katikati, mimi naitwa jambo kubwa. Sauti ya jambo ndogo ilikuwa ni balaa
 
PAKITI YA BLISTA NI RAHISI KUTUMIA!
UNAKUNJA NA KUBONYEZA TU!
NA ISITOSHE HEDEX INAPATIKANA KWA BEI ILEILE!
 
Back
Top Bottom