Tangazo gani la biashara redioni au kwenye runinga uliwahi kulipenda sana?

musicarlito

Senior Member
Dec 29, 2020
176
289
Wasalaam,

Muziki au matangazo ya kibiashara ni vitu vinaweza kutukumbusha hazina ya muda na mambo mazuri tuliwahi kuwa nayo zamani

Binafsi siwezi kulisahau tangazo la dawa ya kuzibia pancha baiskeli..."Vipi Rambooo? Pancha banaa...pancha wakati kuna okoo..."...hapo niko pembeni ya mshua nafanya zoezi la hisabati tena vile vya maswali 40.

Wewe unakumbuka tangazo gani na linakukumbusha "moment" gani nzuri?
 
Wasalaam

Muziki au matangazo ya kibiashara ni vitu vinaweza kutukumbusha hazina ya muda na mambo mazuri tuliwahi kuwa nayo zamani

Binafsi siwezi kulisahau tangazo la dawa ya kuzibia pancha baiskeli..."Vipi Rambooo???...pancha banaa...pancha wakati kuna okoo..."...hapo niko pembeni ya mshua nafanya zoezi la hisabati tena vile vya maswali 40...

Wewe unakumbuka tangazo gani...na linakukumbusha ..."moment" gani nzurii
Unao chaguo
La kizazi kipya
Pepsi chaguo lako
 
nayakumbuka matangazo mawaili

CRDB
tunasonga mbele kwa pamoja mafanikio yetu ya pamoja miaka 10 ya kuhudumia wateja wetu wa Tanzania, CRDB bank tunasinga mbeleeee

Vodacom Mpesa
Nifuraha nchi nzima, watanzania tunapounganishwa na huduma toka voda Mpesa inakufikia, tuma pesa kwa familia, hata kibiasha oooh tuma pesa na Mpesa

Tusker lager
Twende pamoja mimi na wewe bega kwabega ( Milele eeeeh) Huuu umoja wetuu (Aaah milele) twende pamoja, bega kwa bega, marafiki halisi, Bia bora tusker marafiki halisi
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom