Tangazo gani la biashara redioni au kwenye runinga uliwahi kulipenda sana?

Waqt huo makampuni ya tritel na mobitel wakitoza kwa dakika hata ukiongea sekunde kumi wanatoza dakika sasa vodacom wakaja na utozaji wa sekunde na tangazo likawa kwa nini ulipe kingi wakati umetumia kidogo? lilikuwa murua sana ingawa vijana wa mjini walilibadilisha maana kwa kupelekea kuwa unachukua demu bonge waqt unashughulika aah waqt umekwenda wapi!
 
Kazi kazi, tufanye kazi kwa nguvu zoteee tujenge taifa letu....kazi kazi.....
 
Hili tangazo lilisababisha nikalala mtaroni siku mbili kavu, usiku na mchana kwa sababu ya safari
Msafiri asili yake nchini Tanzania, safari ni safari. Iwe mchana au usiku, kiangazi au masika safari ni safari. Kupita jangwani au porini safari ni safari.........

Kitu ya safari Lager hiyo ilikua ni hatari sana
 
Wasalaam,

Muziki au matangazo ya kibiashara ni vitu vinaweza kutukumbusha hazina ya muda na mambo mazuri tuliwahi kuwa nayo zamani

Binafsi siwezi kulisahau tangazo la dawa ya kuzibia pancha baiskeli..."Vipi Rambooo? Pancha banaa...pancha wakati kuna okoo..."...hapo niko pembeni ya mshua nafanya zoezi la hisabati tena vile vya maswali 40.

Wewe unakumbuka tangazo gani na linakukumbusha "moment" gani nzuri?
Tangazo la sabuni ya Revola, sabuni ya Ushindi na Chibuku
Nakubuka kibwagizo cha "ATC Hewani"
 
Back
Top Bottom