Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,978
32,387
Wanaukumbi.

WAZEE+WA+TANU.jpg


Waliokuwa Katika Picha Hii na Ndilo lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU
(Wengine: Hawapo)


  1. [*=left]Abdallah Shomari (Tandamti No. 3)
    [*=left]Nassoro Kalumbanya (Simba)
    [*=left]Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo)
    [*=left]Mtoro Ally (Muhonda)
    [*=left]John Rupia (Misheni Kota)
    [*=left]Julius Nyerere (Pugu Sekondari)
    [*=left]Said Chaurembo (Congo/Mkunguni)
    [*=left]Jumbe Tambaza (Upanga)
    [*=left]Sheikh Suleiman Takadir (Mafia/Swahili)
    [*=left]Dossa Aziz (Mbaruku/Somali Kipande)
    [*=left]Mshume Kiyate (Tandamti)
    [*=left]Juma Sultani (Kitchwele Karibu na Kanisa Dogo)
    [*=left]Maalim Shubeti (Masasi/Likoma)
    [*=left]Rajab Simba (Kiungani)
    [*=left]Waziri Mtonga (Kilosa 18, Ilala)
    [*=left]Mwinjuma Mwinyikambi (Mwananyamala)
    [*=left]Makisi Mbwana (Aggrey/Congo)
    [*=left]Usia Omari (Sungwi, Kisarawe)
    [*=left]Sheikh Issa Nasir (Bagamoyo).


DSC03585.JPG
Kushoto Kwenda Kulia: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdul Sykes na Lawi Sijaona
Ukumbi wa Arnautoglo Kwenye dhifa ya Kumuaga Nyerere Kwenda UNO safari ya pili 1957, picha ya chini Nyerere yupo uwanja wa ndege wa Dar es Salaam akijiandaa na safari ya UNO huku amesindikizwa na kina John Rupia, Bibi Titi Mohamed, Mtevu na wengine.

nyerere_departing_for_UNO.jpg

ALLY+SYKES+AND+JULIUS+NYERERE.JPG


20140430_150609.jpg


20140430_151443.jpg

Hii Picha Ilipigwa Siku ya Nyerere Alipoweka Jiwe la Msingi
Chuo Kikuu Cha Waislam, Chang'mbe 1968 Nyerere
Anapeana Mkono na Mufti Sheikh Hassan bin Amir Katikati yao
ni Tewa Said Tewa Rais wa EAMWS Tawi la Tanganyika

scan0029.jpg
Katika wajumbe Waliohudhuria Mkutano Huu wa Kwanza wa TANU mwaka 1955 Ukumbi wa Hindu Mandal
Dar es Salaam walikuwa Salum Mpunga na Ali Mnjale kutoka Lindi Hawa ndiyo walikuwa
Waasisi wa TANU Jimbo la Kusini. Historia haiwatambui.


MSHUME+KIYATE.jpg
Mzee Mshume Kiyate Akimvisha Mwalimu Nyerere
Kitambi kama ishara ya kuungwa mkono na Wazee wa Dar es Salaam
Baada ya Maasi ya Wanajeshi wa Tanganyika Rifles (TR) tarehe
20 Januari 1964.


Mods msihamishe huu uzi achane watu wajifunze.
 
ccm ina wenyewe ukiona wamesahaulika ujue wao sio wenyewe.Wenyewe ni akina Makinda,Wasira,lukuvi,Nape,Savimbi n.k
 
ccm ina wenyewe ukiona wamesahaulika ujue wao sio wenyewe.Wenyewe ni akina Makinda,Wasira,lukuvi,Nape,Savimbi n.k
Vonix

Hiyo TANU hao wazee wala hawaijui CCM baada ya kutoswa TANU walirudi majumbani mpaka mauti yakawakuta.

Waangalie vizuri Nyerere bado kijana wao ni wazee wengine hata siku ya uhuru hawakuwepo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom