Tanganyika Law Society (TLS)

Tanganyika Law Society (TLS)

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Tarehe 21 na 22 ya mwezi huu,sisi wanachama wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) tulikuwa na mkutano wa siku mbili.Mkutano husika ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC). Vikao husika vilifanyika katika Ukumbi wa Simba.

Katika mkutano huo, hasa sku ya kwanza, mada mbalimbali ziliwasilishwa na kujadiliwa. Mada zilizowasilishwa zililenga hasa Mchakato unaoendelea hapa nchini wa kuandika Katiba mpya ya nchi yetu. Watoa mada na wachangia mada walikuwa machachari na waliojiandaa vya kutosha. Wataalamu wa Sheria kama akina Prof. Hamudi Ismail Majamba na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi walichagiza mada hizo.

Jioni ya tarehe 21, TLS ikaadhimia kuwa na tamko la pamoja juu ya Mchakato wa Katiba mpya Tanzania kwakuwa ilionekana mchakato huo kuanza kwenda mrama. TLS,kama chama cha Wanasheria, kikataka kuweka mambo sawa katika kukemea,kuelekeza na kusahihisha mchakato husika. Timu ya manguli wa sheria ikaundwa kuandaa maadhimio. Ikawajumuisha Mawakili Wasomi kama Prof. H.I. Majamba, Alute Mughway, Beatus Malima na Peter Kibatala.

Maadhimio yakaandaliwa na kusomwa tarehe 22/2/2014. Maadhimio husika yalijikita katika,pamoja na mambo mengine, kusema kuwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba lazima wazingatie maoni ya wananchi katika kuchakata Katiba mpya. Hii ni kusema,Bunge Maalum la Katiba halina mamlaka ya kuacha kabisa Rasimu ya Pili ya Tme ya Jaji Warioba na kuongelea litakayo. Lazima Rasimu iwe ndiyo msingi wa majadiliano kwakuwa ndiyo iliyobeba maoni ya watanzania.

Lakini,tangu maadhimio hayo, kumekuwa na ukimya. Maadhimio hayasikiki wala kutambulika. Hata sina taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Waandishi wa Habari kutoa Maadhimio hayo. Maadhimio yale ya Arusha yaliishia wapi?
 
teh......teh.....teh....sasa kama nyinyi wanasheria ambao ndiyo moja ya wadau wakubwa mnakumbana na ugumu wa aina hiyo sasa sisi wananchi wakawaida itakuwaje?, mwe tumuombe mungu tu atusaidie.
 
Sio siri binafsi napata taabu sana na utayari na umakini wa TLS katika kutekeleza majukumu yake na kutoa muongozo wa masuala tata ya kisheria nchini..Hivi nchi hii tofauti ya wasomi na wasiosoma iko wapii???
 
Duh! MIZENGWE hata kwenu wanasheria WASOMI? Au nanyi mna makundi ama mrengo wa kisiasa? Tutafika kweli?
 
Hiki chama toka kilipohalalisha mwenendo na matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 kilipoteza heshima yake!
 
Hiki chama toka kilipohalalisha mwenendo na matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010 kilipoteza heshima yake!

TLS ni pro Government so tusitegemee waongee lolote litakalowaumiza watawala,wao wale tu fes zetu basi hakuna jipya;hata LHRC inawashinda na wasomi woote..by the way update ya Uchguzi mbona hujatuwekea??man kuna Rais ,Makamu rais wote wapyaaaaaaaa,na Treasurer pia,,cjajua council members wala chapter Convener wa DAr;tujuze basi wakili msomi
 
Kama huyu mwehu aliweza kuwa Rais hiki ni chama kweli?

1.jpg
 
Kama kuna asasi ambayo imeonyesha kutokuwa na uzalendo wowote katika nchi hii, kwa miaka nenda miaka rudi, asasi hiyo ni TLS. Kama itakavyokumbukwa nchi yetu imekuwa ikishuhudia vitendo vingi vya uvunjaji wa katiba na sheria za nchi, na serikali yenyewe pamoja na vyombo vya dola lakini asasi hiyo, hiyo pamoja nakuwa na magwiji wa sheria imekuwa kimya siku zote!
 
Kama huyu mwehu aliweza kuwa Rais hiki ni chama kweli?

1.jpg

Mimi nadhani wewe ndio mwehu acha kumchafulia heshima mzee wa watu, wewe sio mwanasheria wala wakiliiweje udhalilishe viongozi wetu wakati wewe si mmoja wetu au amekuchukulia mkeo.
 
Counsel Peter Mselewa nadhani umefika muda mawakili tuliopo humu JF tuanzishe vuguvugu la mabadiliko sababu kiukweli chama chetu kimekuwa kama mbwa koko kimejaa viongozi waoga(sijui hawa tuliowachagua jumamosi) na wasio na ujasiri wa kianasheria kwa mfano tu huwezi kulinganisha role inayoplay law society ya kenya na hii ya kwetu wenzetu ndio wamekuwa chachu ya mabadiliko lakini sisi wanachojua viongozi wetu ni kujipendekeza ili wateuliwe kuwa majaji.
 
Hivi ukiwa Raia wa Nchi nyingine unaweza kuwa mwanachama wa TLS?

Anaweza isipokuwa awe Mkazi (Resident) na kuwe na Special Resolution ya kum-admit kwenye membership! (Section 8 (1) (e) of TLS Act)
 
Counsel Peter Mselewa nadhani umefika muda mawakili tuliopo humu JF tuanzishe vuguvugu la mabadiliko sababu kiukweli chama chetu kimekuwa kama mbwa koko kimejaa viongozi waoga(sijui hawa tuliowachagua jumamosi) na wasio na ujasiri wa kianasheria kwa mfano tu huwezi kulinganisha role inayoplay law society ya kenya na hii ya kwetu wenzetu ndio wamekuwa chachu ya mabadiliko lakini sisi wanachojua viongozi wetu ni kujipendekeza ili wateuliwe kuwa majaji.

Nina imani na Vice President wetu wa TLS ataleta changamoto;ila kwa President mmh im afraid asije akaleta zile za kizamani..uzuri safu ya sasa ina vijana wako kiuanaharakat zaidi
 
Back
Top Bottom