Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 22,525
- 23,378
Ngoja tumwage mboga ya Mkuu wa Wilaya mtarajiwa. Kuna thread aliiandika, ilikuwa na maneno makali ya kuvunja Muungano
Wapigania uhuru wa Zanzibar waungwe mkono!
Wapigania uhuru wa Zanzibar waungwe mkono!
Tanganyika haihitaji Zanzibar na haiitegemei Zanzibar kwa chochote. Ni kwa sababu hiyo naamini ili kuharakisha Zanzibar kujitoa na viongozi hawa wapigania uhuru kuweza kupata nafasi ya kuongoza taifa la Zanzibar natoa pendekezo kuwa kwa ukarimu wetu kutoka Tanganyika tutenge shilingi bilioni 400 hizi ili kuwasaidia Zanzibar kuanza maisha mapya wao wenyewe. Tuchukue madeni yao ya nje na kuwa tayari kuwalipia mshahara wa vyombo vile vilivyokuwa vya Muungano ili Zanzibar wasije wakasema kuwa wameonewa. Nina uhakika bilioni 400 ni fedha nyingi sana ambazo Wazanzibari watashukuru.