Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 19,887
- 34,274
Heshima sana wanajamvi,
Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ambao uliasisiwa na watu wawili ambao sasa hawapo, tena bila ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili sasa unapitia katika msuko suko mkubwa.
Ni wazi Mwl Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume waliziunganisha zao Tanganyika na Zanzibar pasipo ridhaa za wananchi wa pande zote mbili.
Muungano wao (Nyerere & Karume) kwa hakika umejaa kasoro nyingi mno, kuubadili au kuufanyia marekebisho kutahitaji kuzifumua katiba za nchi zote mbili jambo ambalo kwa sasa ni vigumu sana.
Zanzibar wana serekali yao, wana bunge lao, wana wimbo wao wa taifa lao, wana bendera yao, wana uraia wao (Uzanzibari), wana mkuu wao wa nchi, wana ardhi yao (nchi) wana kila kitu chao.
Tanganyika hawana wimbo wa taifa, hawana mkuu wao wa nchi, hawana ardhi yao, hawana bendera yao, kifupi Tanganyika hawana chochote.
Kuna Taifa la Tanzania (JMT) ambalo limepora kila kitu cha nchi ya Tanganyika. Bendera? Wimbo wa taifa, Bunge.
Tanganyika haina mtetezi wa rasilimali zake eg misitu, ardhi, bandari.
Raia wa nchi ya Zanzibar anaiongoza Tanganyika kupitia mgongo wa Muungano anauza kila rasilimali ya Tanganyika bila huruma kwakuwa hazina mtetezi.
Watanganyika wameamka sasa lugha ya Mch. Mtikila na sasa Mheshimiwa Lissu imeanza kueleweka hadi ndani ya CCM. Ugomvi mkubwa wa Kinana, Makamba na wanaCCM wengi ni Tanganyika kutawaliwa na Rais kutokea nchi ya Zanzibar ambaye amekuwa dalali mkubwa wa kuuza rasilimali za Tanganyika.
Wanaoitaka Tanganyika sasa ni Watanganyika wote bila kujali mipaka ya vyama.
Ngongo kwasasa Mjini Magharibi.
Pia soma
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?