Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,096
Asalaleee! Kuna video inayosambaa kumhusu trafiki anayeonekana akiomba rushwa kwa dereva wa lori kufuatia kosa la mwendokasi. Askari huyo baada ya kufanikiwa kupata rushwa, madereva walimuuliza walipo askari wenzake wenye tochi zinazopima mwendokasi. Askari aliwaelekeza sehemu waliojificha na sehemu yenye kizuizi(barrier) watakayosimamishwa.
Sasa taarifa mpya zinadai Askari huyo wa usalama barabarani ametiwa kibindoni na wakuu wake wa kitengo akisubiri hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yake.
"Afande Taarifa timamu, askari huyu ni namba F. 785 CPL Anthony Temu wa Kituo cha Polisi Kabuku ameajiriwa na Jeshi 01.07.1998. Ameshakamatwa yupo mahabusu pale Kabuku, section imeondoka kwenda kumchukua kumleta Tanga mjini, tunamsubiri kwa hatua. Toka RPC TANGA".
Hiyo ni meseji inayodaiwa kutoka kwa RPC Tanga baada ya kuona video ya Trafiki aliyeomba rushwa.

Attachments
Last edited by a moderator: