Tanga: SUMATRA yazifungia boti 22 Kutoa huduma

Tanga: SUMATRA yazifungia boti 22 Kutoa huduma

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,698
Reaction score
2,262
sumatra40.jpg
​

MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) Mkoa wa Tanga, imesimamisha boti 22 kutoa huduma za usafiri majini kutokana na kutokidhi vigezo vya ubora.

Boti hizo zimefungiwa kutokana na kutokuwa imara hivyo kukosa vifaa vya tahadhari ya majanga baharini.

Sambamba na kasoro hiyo, boti hizo pia hazikuandikwa majina, namba ubavuni kwa ajili ya utambuzi na kutochorwa
mstari ubavuni wa ukomo wa kupakia.

Mkaguzi wa Vyombo vya Baharini Mkoa wa Tanga, Injinia Christopher Mlewa, alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa boti hizo ni kati ya 87 zilizofanyiwa ukaguzi na kubainika zina matatizo.

Mhandisi Mlewa ambaye pia ni Kaimu Ofisa wa Sumatra Mkoa wa Tanga, alisema mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi huo Juni 16 hadi 25 katika Wilaya za Pangani na Mkinga. Alisema kutokana na kufungiwa huko, boti hizo hazitaruhusiwa kutoa huduma mpaka zitakapokamilisha taratibu kwa mujibu wa sheria.

Alisema Wilaya ya Pangani boti zilizosajiriwa na kuruhusiwa kutoa huduma ni 33 na Mkinga ni 32 baada ya kufungiwa boti hizo zingine.

Aidha, Mlewa alisema kuwa Sumatra imetoa tahadhari kwa wenye ngalawa na mitumbwi ipatayo 250 kati ya 300 zilizopitiwa na
ukaguzi huo kwa kuwataka manahodha kuwa makini wanapofanya shughuli zao majini ili kuepuka majanga.

Kadhalika, aliwataka wamiliki wote wa vyombo vya majini kutii sheria ili kuepuka adhabu na kubainisha kuwa kosa la kutosajili
chombo Sumatra na kupata cheti cha ubora. Alisema chombo kitakachofanya shughuli baharini bila kufuata taratibu kitatozwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila kosa.

Alisema ukaguzi huo wa Sumatra ni endelevu na ulianzia wilaya ya Tanga kabla ya Pangani na Mkinga.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom