Tanga: Mwalimu ajinyonga kisa wivu wa mapenzi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,450
Reaction score
5,277
Mwalimu Enock Peter (32) wa Shule ya Msingi Potwe wilayani Muheza mkoani Tanga, amedaiwa kujinyonga kwa kutumia shuka nyumbani kwake, wakati Kesi yake dhidi ya anayedaiwa kuwa Mpenzi wake ikiwa Mahakamani.

Leo Jumatano Julai 16, 2025, Mratibu Elimu Kata ya Pongwe, Rajabu Msuya amesema alifika shuleni kwa mwalimu huyo kwaajili ya kufanya kikao ambapo alimu wote walikuwepo kasoro mwalimu Enock.

“Nilimtuma mwanafunzi aende nyumbani kwake akamuite, lakini aliporudi akasema amegonga lakini hakuitikiwa. Baadaye mwalimu mwingine alienda naye, wakagonga bila kuitikiwa, akaamua kuchungulia dirishani ndipo akamuona mwenzetu amejinyonga,” amesimulia Msuya.

Amesema baada ya kubaini hayo, walitoa taarifa polisi na askari walifika na kuingia ndani na kukuta amejinyonga kwa kutumia shuka aliyoifunga kwenye mbao za juu ya paa la nyumba ya shule aliyokuwa akiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi.

Soma Pia: Geita: Mwalimu ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia

“Katika uchunguzi wetu tumebaini marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake (jina limehifadhiwa). Waliwahi kugombana na alichana vyeti vya mwenza wake na kesi ilikuwa inaendelea mahakamani. Wakati kesi ikiendelea, ndiyo mwalimu huyo ameamua kujinyonga,” amesema.

Amesema Enock alishawahi kukamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani akituhumiwa kwa uharibifu wa mali za mwenza wake na aliachiwa kwa dhamana huku kesi ikiendelea.

Shuhuda wa tukio hilo, Abdulrazaq Kikungo amedai siku mbili kabla ya kujinyonga, Enock aligombana na mwenza wake baada ya kudai kumkuta na ujumbe wa mapenzi kwenye simu. Alimtishia kumuua kwa kisu, jambo lililomfanya mwenza huyo kukimbia.
Screenshot 2025-07-16 214440.png

“Baada ya mpenzi wake kutoroka, Enock alichukua kisu na kukatakata baadhi ya vyombo, kuvunja kabati na kuchana vyeti vya chuo vya mwenza wake. Alishtakiwa polisi na alikamatwa, akaamriwa kulipa gharama za vyeti.”

Amesema wakati mvutano huo ukiendelea na kesi ikiwa mahakamani, jana ndipo waligundua mwalimu huyo amejinyonga, wakihisi chanzo ni wivu wa mapenzi.

“Baada ya ugomvi huo, Enock alikuwa hatoki nje. Mchana alikuwa anakaa ndani pekee yake, usiku kidogo ndio anaenda dukani kununua mikate au viazi."
 
Enock angetafuta mshauri, au rafiki amuelezee hiyo changamoto.

Kukaa peke yako na kuweza kudigest makitu yaumizayo moyo nacho ni kipaji wakiwezacho wachache sana.
Wengine wakipata janga heri aongee kuliko kukaa nalo ndio kama hivyo linamzidi uwezo na kuhisi hamna njia anaweza kuchomoka kumbe si ajabu ni jambo dogo tu angeweza saidiwa akilisema.
 
Tukumbuke Hapo ni Potwe historia ya Potwe si mnaijua
 
Mwalimu Enock Peter (32) wa Shule ya Msingi Potwe wilayani Muheza mkoani Tanga, amedaiwa kujinyonga kwa kutumia shuka nyumbani kwake, wakati Kesi yake dhidi ya anayedaiwa kuwa Mpenzi wake ikiwa Mahakamani.

Leo Jumatano Julai 16, 2025, Mratibu Elimu Kata ya Pongwe, Rajabu Msuya amesema alifika shuleni kwa mwalimu huyo kwaajili ya kufanya kikao ambapo alimu wote walikuwepo kasoro mwalimu Enock.

“Nilimtuma mwanafunzi aende nyumbani kwake akamuite, lakini aliporudi akasema amegonga lakini hakuitikiwa. Baadaye mwalimu mwingine alienda naye, wakagonga bila kuitikiwa, akaamua kuchungulia dirishani ndipo akamuona mwenzetu amejinyonga,” amesimulia Msuya.

Amesema baada ya kubaini hayo, walitoa taarifa polisi na askari walifika na kuingia ndani na kukuta amejinyonga kwa kutumia shuka aliyoifunga kwenye mbao za juu ya paa la nyumba ya shule aliyokuwa akiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi.

Soma Pia: Geita: Mwalimu ajinyonga kisa migogoro ya kifamilia

“Katika uchunguzi wetu tumebaini marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mpenzi wake (jina limehifadhiwa). Waliwahi kugombana na alichana vyeti vya mwenza wake na kesi ilikuwa inaendelea mahakamani. Wakati kesi ikiendelea, ndiyo mwalimu huyo ameamua kujinyonga,” amesema.

Amesema Enock alishawahi kukamatwa na kufunguliwa kesi mahakamani akituhumiwa kwa uharibifu wa mali za mwenza wake na aliachiwa kwa dhamana huku kesi ikiendelea.

Shuhuda wa tukio hilo, Abdulrazaq Kikungo amedai siku mbili kabla ya kujinyonga, Enock aligombana na mwenza wake baada ya kudai kumkuta na ujumbe wa mapenzi kwenye simu. Alimtishia kumuua kwa kisu, jambo lililomfanya mwenza huyo kukimbia.
View attachment 3408312
“Baada ya mpenzi wake kutoroka, Enock alichukua kisu na kukatakata baadhi ya vyombo, kuvunja kabati na kuchana vyeti vya chuo vya mwenza wake. Alishtakiwa polisi na alikamatwa, akaamriwa kulipa gharama za vyeti.”

Amesema wakati mvutano huo ukiendelea na kesi ikiwa mahakamani, jana ndipo waligundua mwalimu huyo amejinyonga, wakihisi chanzo ni wivu wa mapenzi.

“Baada ya ugomvi huo, Enock alikuwa hatoki nje. Mchana alikuwa anakaa ndani pekee yake, usiku kidogo ndio anaenda dukani kununua mikate au viazi."
Shida ya kuwa na demu mmoja
Mwanaume hakikisha unakuwa na tahadhari muda wote na kwenye kikao tulikubaliana usimhudumie mwanamke hadi amekuzalia mtoto.
Atakuwa amejisaidia kabla roho haijamtoka maskini
 
Back
Top Bottom