TANGA KINONDONI wanaongoza kwa tigoooooooooooooooo

TANGA KINONDONI wanaongoza kwa tigoooooooooooooooo

MOORIINGEE

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
381
Reaction score
190
BAADHI ya wanawake kutoka katika Wilaya za Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile.

Hayo yalielezwa na Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) wakati akiwasilisha utafiti uliofanywa na watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji Ngono kinyume na maumbile katika kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini na kuwasilishwa mbele ya Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.

“ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao wal;ihusishwa katika utafiti huo,” alisema Mtafiri Irine.

Aidha alisema wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambayo ni sawa na 26.5% huku 76.4% ya waliohojiwa walidai kufanhamu njia hiyo ya kufanya mapenzi.

Wilayani Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbe na wanaume kuwafanyia wanawake kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.

Wanaume waliohojiwa katika utafiti huo wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai kupunguza raha wanayo ipata.

Wanawake pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga msichana kuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku suala la Mimba nalo likichukua nafasi.

Watafiti hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana.

Aidha imedaiwa kuwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto, jambo ambalo limekuwa likileta tabu kwa wahudumu wa Afya hasa wakunga ambao ni wachache mahospitalini kutumia muda mrefu kumhudumia mjazito mmoja huku wengine wakiendelea kuteseka wodini wakati wa kujifungua.

Watafiti hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia salama za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya kujamiiana kinyume na maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.

Watafiti walioshiriki katika utafiti huo ni pamoja na Akili kalinga, Elizabeth H Shayo, Irene Mremi , Godlisten materu, Stella Kilima, Gibson Kagaruki, Anjela Shija, Judith Msovela, Dk. Leornad Mboera, Dk.Julius Massaga, Kesheni Senkoro na Basiliana Emid wote kutoka NIMR.

source! WANAWAKE WAKIRI KUFANYA NGONO KINYUME NA MAUMBILE: UTAFITI ~ Father Kidevu
 
Kinondoni ndo dsm ndo zao wala hawajawasingizia

Hii yote tu eti aolewe na bikra mila zingine hazina maana, Wengine wakiona video za wazungu wanataka wao wafanye hivyo mtakufab bure wale wanamadawa mengi sana sana wanatumia.
 
Huwa sina comment kwenye maswala haya..
Its ril an unquitable flavour.. Try it not my friend!
 
Mapenzi ya kwenye video si Mchezo
 
Tanga jamani wamekosa bahati,yani hata akifanya wengine lakini Tanga lazima iwepo ndani......
 
Bado nauliza kwanini watu wanaponda matumizi ya ani kwenye ngono lakin hawapingi matumizi ya midomo.......
 
Kufanya ngono kinyume na maumbile kati ya mwanaume na mwanamke, ni sawa tu na kufanya mwanaume na mwanaume, yote ni ushoga. Anayefanywa na anayefanya wote ni mashoga tu. Na wote wanaofanya hivyo, wanaenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu.
 
Back
Top Bottom