TANESO yaibuka, yataka Sh 312 bilioni kununua mitambo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESO yaibuka, yataka Sh 312 bilioni kununua mitambo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jun 2, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,127
  Likes Received: 5,566
  Trophy Points: 280
  Tanesco yaibuka na tahadhari mpya yataka Sh312 bilioni kununua mitambo

  Na Leon Bahati

  BAADA ya kimya cha muda mrefu, Shirika la Umeme (Tanesco) limeibuka na kuiangukia Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ikiomba iikingie kifua ili itengewe Sh312 bilioni kwa ajili ya kununulia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura nchini, huku ikitahadharisha kuwa nchi inaweza kuingia gizani.

  Shirika hilo limeamua kuachana na Wizara ya Nishati na Madini, ikidai kuwa ilishawasilisha maombi hayo muda mrefu, lakini ikaona hayafanyiwi kazi ndio maana limeamua kuyapeleka maombi hayo ya dharura kwenye kamati hiyo ili iikingie kifua.

  Tanesco, ambayo sakata lake la kutaka kununuliwa kwa mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited, lilizimwa na kamati hiyo ya Bunge, limesema kama serikali haitaharakisha mpango huo mapema, kuna hatari ya nchi kuingia gizani kwani tayari baadhi ya vituo vya umeme nchini vimezidiwa nguvu ya matumizi kwa asilimia 10.

  Akiwasilisha ombi hilo mbele ya kamati hiyo, jana, mkurugenzi mtendaji wa Tanesco, Dk Idris Rashidi alisema upungufu huo wa umeme tayari umesababisha kuanza kwa mgawo wa umeme kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na sasa tatizo hilo linaunyemelea mkoa wa Arusha.

  Alisema mahitaji ya fedha hizo ni kwa ajili ya nakisi ya Sh44.23 bilioni kwa ajili ya kukamilisha seti za jenereta 12 zitakazozalisha umeme wilaya za Kasulu, Loliondo, Kibondo na Sumbawanga, Sh161 bilioni kwa ajili ya mtambo wa kuzalisha megawati 100 utakaowekwa Ubungo na Sh107 bilioni kwa ajili ya mtambo unaotumia mafuta mazito utakaowekwa Mwanza, ukitegemewa kuzalisha megawati 60 za umeme.

  "Tanesco inaomba angalau Sh312 bilioni katika kipindi cha mwaka 2009/10 kukamilisha miradi hiyo ya umeme wa dharura. Inashauriwa fedha hizi zipatikane kwa wakati ili kukamilisha jitihada hizi kubwa kabla ya mwishoni mwa Juni, 2010," inasema taarifa ya Dk Rashidi.

  Mkurugenzi huyo wa Tanesco alikabidhi ombi hilo kimaandishi kwa mwenyekiti wa kamati hiyo ya Bunge, William Shelukindo, ambaye ni mbunge wa Bumbuli kwa tiketi ya CCM na kusihi Bunge liipigie debe ili serikali iridhie kuipa fedha hizo.

  Akifafanua ombi ya shirika lake, Dk Rashidi alisema ombi siyo geni kwa serikali, akiwa na maana kwamba tayari alishaliwasilisha, lakini akasema utekelezaji wake umekuwa ni wa kusuasua.

  Hivyo, akaitaka Kamati ya Nishati na Madini iongeze nguvu ili serikali iidhinishe fedha hizo katika mwaka ujao wa fedha 2009/2010.

  Alisisitiza serikali kupitisha fedha hizo mapema kwa sababu mchakato wa kununua mitambo hiyo mipya huchukua zaidi ya mwaka hadi kuwasili nchini na kuanza kufanya kazi.

  Shelukindo alipokea ombi hilo lililokuwa kwenye karatasi yenye kurasa tatu na kuahidi kuwa kamati yake, italijadili na kuweka mikakati ya kuishinikiza serikali, ilitekeleze.

  Kamati hiyo ilipokea ombi hilo wakati ikiwa njiani kwenda kutembelea kituo cha kuzalisha umeme wa megawati 45 kilicho Tegeta wilayani Kinondoni.

  Ombi hilo, Tanesco imeligawanya katika sehemu tatu ambazo zinahusisha ununuzi wa jenereta 17 kwa maeneo ambayo hayafikiwi na mtandao wa gridi ya taifa na mitambo miwili, mmoja kwa ajili ya kuzalisha umeme kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam na mwingine Mwanza kwa ajili ya Kanda ya Ziwa.

  Kuhusu suala la jenereta 17, Dk Rashidi alisema kuwa bunge tayari liliidhinisha kwenye bajeti ya mwaka 2008/2009, lakini kiwango cha fedha kilichotolewa kilitosha kununua jenereta mbili tu ambazo zinatarajia kuanza kufanya kazi mkoani Kigoma kabla ya Juni, mwaka ujao.

  Dk Rashidi alisema Tanesco inahitaji Sh44.23 bilioni kwa ajili ya kununua jenereta 12, ambazo zitagawanywa katika miji ya Loliondo, Kasulu, Kibondo na Sumbawanga.

  Zabuni ya kununua jenereta hizo, alisema Dk Rashidi, ilitolewa kwa kampuni ya M/S Zwart Techniek Januari mwaka huu na ilikuwa ikamilishwe ndani ya miezi 15 kwa mkataba wa Sh59.5 bilioni.

  Mradi wa pili kwenye ombi hilo ni wa kununua mtambo wa megawati 100 inaotumia gesi asilia, ambao utagharimu Sh161 bilioni.

  Dk Rashidi alisema kuwa lengo la mtambo huo ni kukidhi mahitaji ya umeme katika kipindi cha mwaka 2009/2010.

  Mradi wa tatu ni wa kununua mtambo wa megawati 60 unaotumia mafuta ambao utawekwa Mwanza na ambao utaigharimu serikali Sh107 bilioni.

  Dk Rashidi alisisitiza kuwa mitambo ya umeme kwenye Kanda ya Ziwa tayari inaelemewa kutokana na mahitaji ya umeme kuzidi kwa asilimia 10 ya uwezo wake.

  Kwa sababu hiyo, alisema tayari wameanza kutoa umeme kwa mgawo eneo hilo.

  Lakini alisema mradi huo ni wa dharura tu kwa sababu Tanesco inatengeneza njia ya Umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga na inatarajia utakamilika katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia 2010 hadi 2014.

  Ombi hilo la Tanesco limekuja miezi michache baada ya vuta nikuvute iliyosababisha malumbano juu ya kununua ama kutonunua jenereta mbili za kuzalisha umeme wa dharura zinazomilikiwa na Kampuni ya Dowans ambayo ilirithi zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond Development Limited LLC iliyoshinda zabuni hiyo kwa utata.

  Hata hivyo, serikali ilifikia uamuzi wa kutonunua jenereta hizo zilizokuwa zinauzwa kwa Sh90 bilioni na zenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, badala yake ikaahidi kununua mpya.

  Waliokuwa wanashawishi ununuzi wa jenereta hizo, walisema kuwa bado zipo katika hali nzuri, ni za bei nafuu na tayari zinafanya kazi badala ya kutumia muda mrefu kuziagiza hadi kuzifunga.

  Lakini Kamati ya Shelukindo ilisema Sheria ya Manunuzi ya Umeme inakataza serikali kununua vitu vilivyokwishatumika.
   
 2. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,966
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160
  Kinachonichanganya hivi tanesco wanashindwa nini kuwekeza kwnye migodi ya kiwira ili tupate umeme. au migodi ingine ya makaa ya mawe iliopo nchini naomba mwenye datas za vianzo vya nguvu ya umeme ambavyo tanesco inakwepa kuwekeza huko badala yake kutaka kununua mitambo atuelimishe
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Pesa ya 2010 au?
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa nini mipango yao yote ni ya dharura na sio long-term?

  Amandla..........
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Walipewa kiasi kama hicho miezi kadhaa iliyopita. Hatujaambiwa zimefanya nini. Labda Mh Zitto na kamati yake wanaelewa kinachoendelea?
   
 6. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Fundi,
  Yaani sijawahi kuona uongozi bogus kama huu wa TANESCO na wizara ya nishati kwa ujumla. Hawa jamaa hawana mipango endelevu wamekalia kutuletea zima moto tu. Mpaka inatufanya wengine tuamini kuwa hii ni mipango ya CCM kutafuta pesa za kampeni mwakani. Wanataka bilioni 312, tena kabla ya mwezi juni mwakani, lol! Nchi nyingi zenye umeme wa uhakika kama US, China, Australia, Afrika ya kusini etc wanatumia makaa ya mawe kuzalisha umeme wao. Zaidi ya 50 % ya umeme wa Marekani unatokana na makaa ya mawe ambayo sisi tunayo kwa wingi. Kama ni suala la Climate Change, hivi sasa kuna teknolojia za kuyatumia makaa ya mawe bila kuchafua mazingira. Bila umeme wa uhakika, hakuna maendeleo. TANESCO na Wizara ya Nishati na madini amkeni.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  na long term plans zilikuwepo, sijui zimefia wapi. nadhani mfumo uko desperate kupata pa kuanzia kujipatia fedha za kampeni mwakani.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  What is wrong with Tanesco strategies and approaches? Ni hawahawa ambao waliiendea kwanza kamati ya Bunge ya uwekezaji wakati walipotaka kununua mitambo ya Dowans. Walipoona wamewekewa kauzibe, wakaruka hadi kwenye kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma. leo hii, wamepeleka maonmbi wizarani, wanaona yamekaliwa wameruka hadi kwenye kamati ya Bunge!
   
 9. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tz na hekaya za umeme wa dharura! Sasa naamini kuwa huu nimradi wa watu wachache. Hivi karibuni Kenya waingia kwenye kutengeneza umeme kwa kutumia upepo, Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi naye katoa kipaumbele kuzalisha umeme wa upepo, na tayari nchi hiyo ndogo imeanza kuchimba madini ya uranium tena mpakani na Tanzania maeneo ya Karonga, hivyo ni wazi si muda mrefu tukasikia wanazalisha umeme kwa kutumia nishati ya nyuklia.

  Sisi tunaendelea na hadidhi za umeme wa dhararua kutumia majenereta wakati mkaa wa mawe tunao, upepo upo, na madini ya uranium tunayo, wizi mtupu!
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tanesco wahakikishe wanazalisha umeme kupitia makaa ya mawe kutoka kiwira au kwingineko,hizo mashine ni nguvu za zima moto kesho itaharibika kwa nini wana njia za mlipuko hawa nao
   
 11. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yaani ni kukosa uzalendo wa dhati kwa viongozi wetu.Mbali na makaa ya mawe ya Mchuchuma yanayoweza kuzalissha megawati 400 kwa miaka hadi 40,pia tunayo gesi (natural gas) ya kumwaga ila mipango ni mibovu kwa mfano Songosongo peke yake kuna 726 billion cubic feet. Na pia kuna significant gas field huko Mnazi bay (Mtwara). Tungeweza kuwa na umeme wa uhakika kabisa na na uchumi ungekua kwa kasi kama nchi yetu ingekuwa na viongozi wenye uchungu na maendeleo ya nchi yao. Kwa sasa tuna wezi watupu wenye kujali matumbo yao. Ubinafsi umejaa vifuani mwao.
   
 12. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli viongozi wetu wasipobadili mtazamo; kutakuwa hakuna tofauti ya zama za UTUMWA na leo; mtumwa siku zote hawajibiki juu ya maisha yake badala yake mtu mwingine anawajibika juu yake. Tupo huru lakini hatujui jinsi ya kuutumia uhuru wetu, kwani wakati wote tumekuwa tunafikiri juu ya kununua mitambo na vitu vinginevyo badala ya kuwa na mtazamo wa jinsi gani ya kuzalisha kilicho chetu. Mtazamo huu wa kuwafikiria WAZUNGU au nchi zilizoendelea wao kufikiri zaidi juu ya miundo mbinu yetu ni kujiweka utumwani. Hivyo tubadili mtazamo na kuanza kutafuta kuzalisha cha kwetu ambacho kizazi na kizazi wataendeleza.
   
 13. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kiwira che nkapa
  mchuchuma che nkwete

  kwa hiyo TZ hatuna makaa ya mawe yote yanamilikiwa na watu binafsi
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Makaa ya mawe yapo bwerere nyanda za kusini lakini hakuna cha maana tunachofanya kuendeleza miradi ya kuzalisha umeme huko.
  Tunafikiria kuwa East African power pool bila ya kwua na mipango ya kustimulate available powers sources kama hayo makaa ya mawe na stiglers. Tumebakia kupiga siasa tu
   
Loading...