Tanesco yailipa downs

Tores

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
551
475
Kwa taarifa zinavyoripoti kwenye gazeti la Mwananchi, inaelekea baada ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutaka ripoti ya matumizi ya kiasi fulani cha fedha toka TANESCO na TANESCO kushindwa kumpelekea ripoti ya matumizi ya fedha hizo, basi inasadikiwa kuwa shirika hilo la umeme Tanzania, TANESCO, limeilipa Kampuni ya kufua umeme ya DOWANS dola za Marekani 1.2 milioni ikiwa ni gharama ya kusafirisha mitambo ya kampuni hiyo kuja nchini kwa ndege, badala ya dola 120,000 tu.

Matumizi hayo ya ziada yanayokadiriwa kufikia shilingi za Kitanzania bilioni 1.4 yaliingizwa katika akaunti ya DOWANS kimakosa.

Matumizi mengine ya fedha yaliyohitaji ripoti wachilia hayo ya Bilioni 1 na ushee, ni mchanganuo wa matumizi ya dola za Marekani 4,865,000 sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 6.8!
 
Wahitaji wa umeme ni wengi sana lakini hawawezi kulipia "Service Line" Busara ingetumika badala ya kugawa pesa hizi kwa wachache basi pawepo na "RUZUKU YA NGUZO" ili na walala hoi waoine mwanga wa umeme kabla Mwenyezi Mungu hajachukua maisha yao hapa duniani.
 
eti yameingia kimakosa....sasa kwa nini hawakusahihisha.....haya mambo ya kujivua gamba haya....yatapelewa watu msituni....tumechoka jamaniiiiiiiii
 
eti yameingia kimakosa....sasa kwa nini hawakusahihisha.....haya mambo ya kujivua gamba haya....yatapelewa watu msituni....tumechoka jamaniiiiiiiii

Usiwabishie inawezekana warembo walioko kule Tanesco wengi wao ni watupu kichwani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom