Tanesco Ya Idrisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco Ya Idrisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima, Jan 3, 2008.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Waungwana,

  Hii sio mada ya siasa lakini naomba ikae hapa kwa muda labda nitapata mtu wa kunisaidia.

  Nina biashara yangu ambayo inahitaji umeme mwingi (three phase) lakini wakati tuananza Tanesco walifunga single phase kwasababu
  tulianza na kazi chache.

  Mwanzoni mwa mwaka jana tulilipia three phase meter ili waondoe single phase na kutuletea mpya lakini mpaka leo hakuna meter.

  Mimi naingia hasara maana vyombo vikubwa vya music vikipingwa umeme unakatika, AC hatuwezi kuwasha na customers wanatukimbia kwa ajili ya hilo.

  Nimefuatilia Tanesco kupitia watu mbalimbali na mpaka sasa ni uzungushaji tu.

  Idrisa juzi hapa niliona alivyokuja juu na kuwakatia umeme Tanga Cement kwa kutokulipa. Sasa je wao wanapochukua pesa za wateja na kushindwa kutoa service, sisi tuna haki gani?

  Mimi nataka kuongea na Idrisa mwenyewe au msaidizi wake kama inawezekana. Kama kuna mtu ana namba yake tafadhali nisaidieni.

  Ikishindikana nitapeleka suala langu kwenye vyombo vya habari weekend hii.

  Ubabaishaji wao huu na ambao unaleta hasara kwa watu wengine lazima uumbuliwe.

  Kuna ugumu gani kuagiza meter za kutosha kwa ajili ya wateja wao?

  Tafadhali yeyote mwenye msaada kwenye hili jambo naomba aandike hapa ili tupate ufumbuzi wa kudumu maana kwa mwendo huu tutaanda mpaka mwisho wa 2008, huku hakuna kinachoeleweka.

  Siwezi kuendelea kupata hasara kwasababu Idrisa na shirika lake wanashindwa kutimiza wajibu wao.
   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Asante Mkuu. Haya ndiyo ninayoyapigia kelele. Dharau, dhuluma kwa wateja ndivyo vilivyotanda Tanesco. Sitashangaa huyu mkuu akiambiwa alipe nyongeza ya bei mpya kabla hajapatiwa 3-fez wakisahau kuwa waliishakopa kwake bila kumlipa riba!
   
 3. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwa nini usiwapeleke mahakamani iliwakulipe hasara unayoipata mpaka pale watakapo kuwekea hiyo mita nyingine.muda wa kuwabenbeleza umekwisha.
   
 4. C

  Chuma JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mifumo yetu ya kimahakama nayo ni tatizo, itakubidi ulipe twice or thrice ili kupata HAKI yako. kesi zipo nyingi hata ARDHi..ila kwa kesi yako ipo wazi unless uwe NJE ya DSM. Check website ya Tanesco, then utapata namna ya kumpata mkurugenzi....Ukishindwa hapo huna haja ya kutishia weka LIVE ktk Magazeti ya Nyumba na ktk Mtandao na FULL details.
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  katibu tarafa umesomea Sheria nini? nimeona hata zile post zako za TRA ukisisitiza mahakama...mahakama ni NJIA NDEFU ya kupata haki yako, na wapo wajanja wanaocheza na sheria(mawakili) ili uje ukose haki zako
   
 6. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2008
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  siku hizi kuna mahakama za biashara na watu wanakomba kama hawana aliki nzuri fidia kutokana na kutowajibika kwao,hizi sio zile mahakama za kisutu,huku bwana jinsi wanavyochelewesha kesi yoako ndivyo dau linavyopanda.wale wajanja wakiona tu hapana ushindi basi wanaomba suluhu nje ya mahakama.
  Nauwakika akipeleka kesi mahakamani hata chukua zaidi ya mwezi kila kitu kwisha na mita wanamuwekea tena kwa kumpigia magoti,lakini ukiwasikiliza wao bila kuwachapa kiboko utasubiri mpaka uchaguzi ujao
   
 7. C

  Chuma JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  hapo itabidi tufuatilie...its good attempts..
   
Loading...