TANESCO WIZI MTUPU!! yaingizwa katika kashfa mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO WIZI MTUPU!! yaingizwa katika kashfa mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,347
  Likes Received: 5,653
  Trophy Points: 280
  TANESCO yaingizwa katika kashfa mpya

  Mwandishi Wetu Aprili 29, 2009

  CAG abaini malipo tata ya mabilioni

  Ni yanayolipwa kampuni ya Songas

  Sasa Bunge kuwasha moto mpya

  UTATA mpya umeibuka katika mkataba wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ukihusu shirika hilo la umma na kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas Limited, iliyolipwa kila mwezi zaidi Sh Bilioni tano katika mazingira yanayotia shaka, imefahamika.

  Fedha hizo ni zile zilizolipwa na TANESCO kila mwezi kwa ajili ya kununua umeme kutoka kampuni ya Songas Ltd ya Dar es Salaam, ikiwa ni malipo ya ‘capacity charges’ zinazoelezwa kwamba si sahihi, na zimelipwa katika mazingira tata.  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh
  Kutokana na hali hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amependekeza kupitiwa upya kwa mkataba huo unaotajwa kumalizika muda wake miaka 25 ijayo, yaani mwaka 2024. Bunge linatarajiwa kuazimia kumuunga mkono CAG kuhusu suala hilo.

  Hatua hiyo ya Bunge inatokana na taarifa ya CAG ya ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2007/2008 ndani ya TANESCO, shirika ambalo linaaminika kuwa katika matatizo makubwa ya kifedha lakini likiwa na mianya mingi ya kupoteza fedha, hususan katika ununuzi wa umeme kutoka kampuni binafsi au zenye ubia na Serikali.

  Taarifa iliyotolewa wiki hii ya CAG kuhusu ukaguzi wa hesabu za TANESCO imebaini kuwa shirika hilo pekee la ugavi wa umeme nchini lina haki ya kimkataba ya kutathmini gharama za awali za mradi wa Songas ili kujua uhalali wake, na gharama hizo zitumike kama kigezo cha kulipa capacity charges, lakini fursa hiyo ilipuuzwa na uongozi wa TANESCO.

  Kwa mujibu wa matokeo ya ukaguzi wa CAG TANESCO haikufanya tathmini ili kujiridhisha kuwa hizo Sh bilioni tano zinazolipwa kwa Songas ni sahihi au la, na badala yake ilikubali ‘kichwakichwa’ mapendekezo ya Songas na kulipa kiasi hicho ambacho ofisi ya CAG inaamini kuwa ni kikubwa mno na kingeweza kupunguzwa kama TANESCO wangekuwa makini.

  “Ukaguzi umegundua kuwa tathmini hiyo haijafanyika na hivyo TANESCO imeendelea kulipa capacity charges ya dola milioni 5 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 5) kwa mwezi kwa kuangalia makadirio ambayo yametolewa na Songas Ltd.

  Katika ripoti hiyo, CAG anaeleza mtazamo wake kuwa gharama zinazolipwa na TANESCO si sahihi kwa sababu tathmini haijafanyika na anapendekeza uongozi wa TANESCO kuchukua hatua za haraka kufanya tathmini ili kujua gharama halisi ambayo TANESCO inastahili kulipa Songas Ltd tofauti na hizo Sh. bilioni tano wanazolipa sasa.

  Lakini wakati Bunge likiwa na mtazamo huo kuhusu Songas kujizolea Sh bilioni tano kila mwezi, kiwango ambacho si sahihi na kinaweza kupunguzwa kwa kuzingatia umakini wa TANESCO, pia imebainika kuwa Kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba wa kampuni tata ya Richmond nayo ililipwa kwa makosa dola za Marekani 4,865,000 (zaidi ya Sh bilioni 4.9).

  Kutokana na hali hiyo CAG anataka kuchunguzwa kwa uhalali wa malipo hayo na kuchukuliwa kwa hatua ikiwa ni pamoja na kudai fedha hizo mara itakapothibitishwa kuwa zimelipwa kwa makosa.

  Katika kuonyesha kuwa sekta ya umeme nchini imezidi kuzongwa na matatizo lukuki, Bunge linatarajiwa na hasa kupitia Kamati yake ya Kudumu ya Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kuitaka rasmi Serikali kuhakikisha mgawo wa umeme unaojirudia mara kwa mara kutokana na kuharibika kwa mashine za Songas unakwisha na kwamba kuwepo mpango madhubuti utakaonusuru nchi kuingia gizani.

  Na ili TANESCO iweze kufanikisha malengo yake, wabunge wanaishauri Serikali kupunguza kuingilia shughuli za shirika hilo kama ilivyokuwa katika mikataba ya Kampuni ya Richmond na mingine.

  Katika hatua nyingine, wabunge wameelezea kuguswa kwao na mvutano wa kisheria kati ya wadau wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wameishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuingilia kati suala hilo limalizike haraka, hata ikibidi nje ya Mahakama.

  Ushauri huo unalenga kuharakisha ubadilishaji wa mitambo ya IPTL ili itumie gesi badala ya mafuta katika kuzalisha umeme hali inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa umeme wa megawati 100.

  Habari zilizopo zinabainisha kuwa wabunge kupitia moja ya kamati zake wamejiridhisha kuwa IPTL iliitapeli nchi na TANESCO kutokana na kampuni hiyo kulipwa zaidi ya kiasi cha fedha walichopaswa kulipwa .

  Hata Serikali kupitia taarifa yake rasmi iliyowasilishwa hivi karibuni bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imedhihirisha kuhusu udanganyifu uliofanywa na IPTL kuhusiana na kiasi cha fedha kampuni hiyo ilichowekeza.

  Kuhusu Songas, wabunge waliozungumza na Raia Mwema wamesema iwapo marekebisho ya mkataba wa sasa unaoiwezesha kampuni hiyo kulipwa Sh bilioni tano kila mwezi yatakataliwa na Songas, basi Serikali inunue hisa za Songas katika kampuni hiyo ya ubia ambazo ni asilimia 54.

  Kama Serikali itanunua hisa hizo za Songas itakuwa inamiliki mradi mzima kwa kuwa mradi huo ni wa ubia kati yake na Songas.

  TANESCO imekuwa katika wingu zito la matatizo kwa miaka kadhaa sasa tokea Serikali iliweke shirika hilo katika mchakato wa kulibinafsisha na hata kulikabidhi kwa menejimenti ya kigeni ya kampuni ya Net Group Solutions ya Afrika Kusini, hatua iliyoibua utata mkubwa na hata kuliyumbisha shirika.

  Tokea wakati huo, hali ya TANESCO imeendelea kuwa mbaya hadi kufikia hatua ya kuingia katika mikataba yenye utata kama ule wa Richmond na baadaye Dowans na Songas, huku wananchi wakiendelea kutokupata umeme wa uhakika.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  TANESCO yaingizwa katika kashfa mpya

  Mwandishi Wetu Aprili 29, 2009

  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  CAG abaini malipo tata ya mabilioni

  Ni yanayolipwa kampuni ya Songas

  Sasa Bunge kuwasha moto mpya

  UTATA mpya umeibuka katika mkataba wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ukihusu shirika hilo la umma na kampuni ya kuzalisha umeme ya Songas Limited, iliyolipwa kila mwezi zaidi Sh Bilioni tano katika mazingira yanayotia shaka, imefahamika.

  Fedha hizo ni zile zilizolipwa na TANESCO kila mwezi kwa ajili ya kununua umeme kutoka kampuni ya Songas Ltd ya Dar es Salaam, ikiwa ni malipo ya ‘capacity charges’ zinazoelezwa kwamba si sahihi, na zimelipwa katika mazingira tata.

  Kutokana na hali hiyo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amependekeza kupitiwa upya kwa mkataba huo unaotajwa kumalizika muda wake miaka 25 ijayo, yaani mwaka 2024. Bunge linatarajiwa kuazimia kumuunga mkono CAG kuhusu suala hilo.

  Hatua hiyo ya Bunge inatokana na taarifa ya CAG ya ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha 2007/2008 ndani ya TANESCO, shirika ambalo linaaminika kuwa katika matatizo makubwa ya kifedha lakini likiwa na mianya mingi ya kupoteza fedha, hususan katika ununuzi wa umeme kutoka kampuni binafsi au zenye ubia na Serikali.

  Taarifa iliyotolewa wiki hii ya CAG kuhusu ukaguzi wa hesabu za TANESCO imebaini kuwa shirika hilo pekee la ugavi wa umeme nchini lina haki ya kimkataba ya kutathmini gharama za awali za mradi wa Songas ili kujua uhalali wake, na gharama hizo zitumike kama kigezo cha kulipa capacity charges, lakini fursa hiyo ilipuuzwa na uongozi wa TANESCO.

  Kwa mujibu wa matokeo ya ukaguzi wa CAG TANESCO haikufanya tathmini ili kujiridhisha kuwa hizo Sh bilioni tano zinazolipwa kwa Songas ni sahihi au la, na badala yake ilikubali ‘kichwakichwa’ mapendekezo ya Songas na kulipa kiasi hicho ambacho ofisi ya CAG inaamini kuwa ni kikubwa mno na kingeweza kupunguzwa kama TANESCO wangekuwa makini.

  “Ukaguzi umegundua kuwa tathmini hiyo haijafanyika na hivyo TANESCO imeendelea kulipa capacity charges ya dola milioni 5 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 5) kwa mwezi kwa kuangalia makadirio ambayo yametolewa na Songas Ltd.

  Katika ripoti hiyo, CAG anaeleza mtazamo wake kuwa gharama zinazolipwa na TANESCO si sahihi kwa sababu tathmini haijafanyika na anapendekeza uongozi wa TANESCO kuchukua hatua za haraka kufanya tathmini ili kujua gharama halisi ambayo TANESCO inastahili kulipa Songas Ltd tofauti na hizo Sh. bilioni tano wanazolipa sasa.

  Lakini wakati Bunge likiwa na mtazamo huo kuhusu Songas kujizolea Sh bilioni tano kila mwezi, kiwango ambacho si sahihi na kinaweza kupunguzwa kwa kuzingatia umakini wa TANESCO, pia imebainika kuwa Kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba wa kampuni tata ya Richmond nayo ililipwa kwa makosa dola za Marekani 4,865,000 (zaidi ya Sh bilioni 4.9).

  Kutokana na hali hiyo CAG anataka kuchunguzwa kwa uhalali wa malipo hayo na kuchukuliwa kwa hatua ikiwa ni pamoja na kudai fedha hizo mara itakapothibitishwa kuwa zimelipwa kwa makosa.

  Katika kuonyesha kuwa sekta ya umeme nchini imezidi kuzongwa na matatizo lukuki, Bunge linatarajiwa na hasa kupitia Kamati yake ya Kudumu ya Mashirika ya Umma inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, kuitaka rasmi Serikali kuhakikisha mgawo wa umeme unaojirudia mara kwa mara kutokana na kuharibika kwa mashine za Songas unakwisha na kwamba kuwepo mpango madhubuti utakaonusuru nchi kuingia gizani.

  Na ili TANESCO iweze kufanikisha malengo yake, wabunge wanaishauri Serikali kupunguza kuingilia shughuli za shirika hilo kama ilivyokuwa katika mikataba ya Kampuni ya Richmond na mingine.

  Katika hatua nyingine, wabunge wameelezea kuguswa kwao na mvutano wa kisheria kati ya wadau wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wameishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kuingilia kati suala hilo limalizike haraka, hata ikibidi nje ya Mahakama.

  Ushauri huo unalenga kuharakisha ubadilishaji wa mitambo ya IPTL ili itumie gesi badala ya mafuta katika kuzalisha umeme hali inayotarajiwa kuongeza uzalishaji wa umeme wa megawati 100.

  Habari zilizopo zinabainisha kuwa wabunge kupitia moja ya kamati zake wamejiridhisha kuwa IPTL iliitapeli nchi na TANESCO kutokana na kampuni hiyo kulipwa zaidi ya kiasi cha fedha walichopaswa kulipwa .

  Hata Serikali kupitia taarifa yake rasmi iliyowasilishwa hivi karibuni bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, imedhihirisha kuhusu udanganyifu uliofanywa na IPTL kuhusiana na kiasi cha fedha kampuni hiyo ilichowekeza.

  Kuhusu Songas, wabunge waliozungumza na Raia Mwema wamesema iwapo marekebisho ya mkataba wa sasa unaoiwezesha kampuni hiyo kulipwa Sh bilioni tano kila mwezi yatakataliwa na Songas, basi Serikali inunue hisa za Songas katika kampuni hiyo ya ubia ambazo ni asilimia 54.

  Kama Serikali itanunua hisa hizo za Songas itakuwa inamiliki mradi mzima kwa kuwa mradi huo ni wa ubia kati yake na Songas.

  TANESCO imekuwa katika wingu zito la matatizo kwa miaka kadhaa sasa tokea Serikali iliweke shirika hilo katika mchakato wa kulibinafsisha na hata kulikabidhi kwa menejimenti ya kigeni ya kampuni ya Net Group Solutions ya Afrika Kusini, hatua iliyoibua utata mkubwa na hata kuliyumbisha shirika.

  Tokea wakati huo, hali ya TANESCO imeendelea kuwa mbaya hadi kufikia hatua ya kuingia katika mikataba yenye utata kama ule wa Richmond na baadaye Dowans na Songas, huku wananchi wakiendelea kutokupata umeme wa uhakika.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Apr 29, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lazima fisadi Dau anahusika....
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Dau au Dr?
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Umekosea kwa bahati Mbaya au.....otherwise thibitisha!!!!
   
Loading...