Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,196
Kwa sasa karibu mikoa yote ya Tanzania inakabiliwa na katizo la umeme la kila siku. Vijiji vya pembezoni mwa Dar Es Salaam kama vila Pugu Majohe, vinakosa umeme kila siku kuanzia saa kumi jioni au wakati mwingine kuanzia saa moja na nusu jioni hadi saa sita za usiku. Wakati mwingine wakazi wa majohe wanakosa umeme usiku kucha. lakini hali ya ukataji wa umeme imeripotiwa pia huko Njombe, Mbeya, Arusha, Moshi, Mwanza na maeneo mengine mengi.
Pamoja na hali hii kukithiri na kuwa kero kwa watumiaji wa umeme, TANESCO haijatoa tamko lolote kuhusiana na mgao huu unaoendelea na wala haijawa tayari kutoa ratiba ya mgao huo. Binafsi napendekeza kwamba kwa maslahi ya wananchi, ni vema TANESCO wakatangaza ratiba ya mgao wa umeme ili wote tujue na tujiandae pale muda wa umeme kukatika unapofika. Utaratibu huu wa sasa wa ukataji umeme, unatuumiza sana watanzania wa hali ya chini, ambao maisha yetu yanategemea uuzaji wa ice cream na mabarafu.