TANESCO taabani; EWURA yaomba kupandisha gharama za umeme!

Jamen hizo bilioni zinatumiwa na TANESCO ni sahihi hakuna kilichokosewa jamani shirika hili litumia fedha nyingi katika kununua mafuta, kuyalipa makampuni binafsi yanayoiuzia umeme, capacity charges yaani kwa sasa halina kitu linadaiwa hadi uvunguni. Na hivi sasa suppliers wao kibao wanawadai na wengine wamekwenda kuwashitaki mahakamani kweli wanadaiwa!!!!

Cha msingi nao wao wapunguze matumizi yasiyo ya lazima kama safari kuna taarifa ndani ya TANESCO kwamba viongozi wa TANESCO wanasafiri kupita maelezo hadi wengine wamepewa majina ya VASCO DAGAMA!!!! kingine matumizi ya magari ni makubwa katika shughuli binafsi na wengine wanakwenda na magari ya shirika nyumbani kwa matumizi binafsi.

Profesa Muhongo uko wapi TANESCO wamekuzidi maarifa wenzio ulisema wabane matumizi lakini ndiyo kwanzaaaaa wanakula kuku kwa raha zao!!!!!! mikutano kila kukicha ukienda TANESCO kutaka huduma hasa Makao Makuu utaambiwa viongozi wapo kwenye vikao kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa huku chai na vibakuli vya maandazi na michuzi kikatisha utadhani kuna sherehe Profesa Muhongo unalijua hilo hebu vamia siku moja TANESCO bila taarifa hasa wakati wa saa nne au saa saba mchana utakuna na mabakuli ya vyakula profesa kazi kwako!!!!
 
naomba kuuliza wataalamu wa mambo ya mafuta...
Bilioni 1.5 ni sawa na lita ngapi ya mafuta mazito?
Na mitambo inatumia lita ngapi kwa saa?
Huu ni wendawazimu...maana tanesco lingekuwa ni shirika kama atcl au kiwanda cha uma lingeshakufa zamani sana...hiyo hela wanayotaka kupandisha leo baada ya mwaka watasema haitoshi...iko wapi mipango???

tafuta mwenyewe kwa kufanya average ya bei ya mafuta unazoziona ktk vituo vya mafuta, utapata wastan in ltrs, mengine fika ofc za tanesco omba uelekezwe utakapojibiwa maswali yako
 
Hivi kama Ewura walishaajiri mchambuzi wao na akatoa mwongozo wa bei anayoona inafaa, mawazo ya wadau yana nafasi gani katika upangaji wa bei? Kwa nini hayo maoni ya wadau isingekuwa input kwa mshauri wao katika kufikia bei wanayotaka?

Kwa mazingira hayo yanasababisha wananchi wasijitokeze kwani wanaona kama hakuna badiriko lilakaloletwa na michango yao.

Naungana na wadau katika kushangaa kwa nini Tanesco wanunue mafuta wao na kisha wanunue umeme pia, au huwa wanakatana kwenye bei ya umeme wanayonunulia?
 
Mie nimejawa na hasira na si kingine na ndio maana watu wanaiba umeme alafu tunawacheka kumbe tatizo linaanzia kwao TANESCO na hao wanaojiita EWURA kwa kupandisha bei kiholela wasio wavumilivu wanaita vishoka wanafanya mambo
 
(((IPTL megawati 100 = shilingi bilioni 1.4 kwa siku) (+) (Symbion megawati 160 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku) (+) (Agreko megawati 100 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku ))) = Gharama zote kwa siku ni shilingi bilioni 5.2 (????????)
Hapo ilionekana wanataka tu kufikia bilioni 5.2, ukichunguza kwa undan gharama hizo za tanesco utakuta zinahusisha mi 10% ya wakubwa wengi sana. Mimi nadhanifike sehem tuseme tu inatosha, tuvute handbreak na kwenye gari tushuke tukae chini!!!
 
TANESCO wanatuhamashisha tuanze kuiba umeme, sababu wengi wao na viongozi serikalini hawajui jinsi tunavyopata shida.
 
wadau,

CAPACITY CHARGES & MIKATABA MIBOVU NDIO MATATIZO MAKUBWA!!

nimejaribu kucheki kwa haraka, inaelekea matumizi ya mafuta na gharama ya hayo mafuta hayana tofauti sana na jinsi ilivyoelezwa kwa kutumia mifano michache niliyoweka links zake hapo chini.

tatizo nafikiri ni

1) mpango mzima wa maendeleo wa TANESCO una matatizo .... hauko "realistic". Vitu vya muhimu havipewi kipaumbele au havipati fedha za kutosha na ufuatiliaji wake una walakini. Tutategemea umeme wa dharura mpaka lini? Naipongeza serikali kwa juhudi za kujenga bomba la gesi lingine kuongeza uwezo, nategemea litasaidia sana.

2) kuna watu wameingia mikataba mibovu, sababu gharama kubwa ni hiyo "capacity charge" wala si ununuzi wa mafuta. Je hii mikataba inaweza kubadilishwa? hasa hizi gharama za capacity charges?

3) kwenye mamlaka kama EWURA wajitahidi kuajiri wataalam wao wenyewe wa kufanya hizo kazi sio kila kitu wao wanatafuta wataalam/washauri elekezi, je wao EWURA kazi yao ni nini?

4) waandishi wa habari nao wajitahidi kufanyia uchunguzi habari zao ikiwa pamoja na kuhoji mambo wanayosikia na kuambiwa sio wafanye "copy and paste" wanachoambiwa. Hii inaonekana sehemu nyingi sana ambazo wanaandika habari zisizofanyiwa uchunguzi au zina makosa.


Approximate Diesel Generator Fuel Consumption Chart

The Technical Program of 100MW HFO Power Generating Plant

Calculation of investment income 100MW HFO Diesel Generator power plant

Institute for Energy Research | Levelized Cost of New Electricity Generating Technologies
 
Solution sio kupandisha bei, baada ya mwaka tutarudi palepale. Hiyo mikataba ni noma
 
1. Gharama za mafuta na vipuri inabidi vibebwe na TANESCO kwa kuwa ni sehemu ya gharama za kuzalisha umeme anaouziwa TANESCO. Kimkataba gharama hizi hujulikana kama Energy Charge.
2.Capacity Charge maana yake ni gharama ya kilipa deni (debt), mtaji (equity), faida ya deni (interest), faida ya mwekezaji (return on Equity) na gharama za uendeshaji na matengenezo (Fixed operation and maintanance cost)
3. Capacity Charge siku zote inazidi gharama za ununuzi wa mafuta (angalia mchanganu katika kipengere cha 2.0 hapo juu)
4.Jukumu la anayemuuzia TANESCO umeme ni kuhakikisha mitambo yake ipo tayari wakati wote ili TANESCO anapohitaji umeme aweze kuzalisha.
5.Kubadilisha mitambo itumie gesi asilia inawezekana, hata hivyo changamoto iliyopo hivi sasa ni kutukuwepo kwa uwezo wa kutosha kuleta gesi asilia ya kutosha kutoka Songo Songo hadi Dar es Salaam. Mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara utakapokamilika utasaidia kupunguza tatizo.
6.Kuhusu uwezo wa kujiendesha kwa TANESCO, ni kweli kwamba kama hatua hazitachukuliwa kurekebisha bei za umeme pamoja na kuongeza mtaji kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme itakuwa ni ndoto kwa TANESCO kujiendesha yenyewe bila msaada wa Serikali.

Natumai umepata uelewa wa hali halisi ya shirika la TANESCO.
 
jaman hizo figure ni za kweli hawajakosea hilo shirika linafilisiwa na makampuni binafsi yanayoiuzia umeme mbona kipindi cha nyuma hatujawahi kusikia TANESCO haina pesa kama hivi sasa Symbion, Agrekko, Songas wanaifilisi TANESCO, mafuta nao yanaifilisi TANESCO kila siku yananunuliwa. lakini mbona na wao hawatuambia wamejipanga vipi kupunguza matumizi ya fedha tunasikia wanatumia magari ya kifahari tena ya ofisi na mbaya zaidi wanakwenda nayo majumbani na yanatumika kwa shughuli za nyumbani na si za kiofisi na pia tuna nyepesi nyepesi tumepata kwamba TANESCO wanaongoza kwa takrima na vikao vingi sana huku vikiambatana na vibakuli vya vyakula na chai kwa wingi je nayo ni muhimu?
 
Capacity charge maana yake ni mgao wa wakubwa . Au kwa jina jingine wizi wa wazi wazi. Kweli wajinga ndio tuliwao
 
Ukiona raia wamegoma kuhudhuria ujue wamechoshwa na usanii na wanaona kuhudhuria sio issue issue ni kudeal na chanzo cha haya yote..ccm
 
why capacity and not fixed charges? mfano, mwenye mitambo angeweza kununua mafuta mwenyewe, vipuri, na all incidentals, then tanesco wakanunua umeme kwake cost per unit fullstop, hayo mambo ya ku-supply mafuta na kama mtambo ni mbovu unakula mafuta zaidi hiyo cost ni ya nani?
 
Loh!
Bora tujitenge Mibara MIJIZI sana.

Si walisema gharama kushuka january?

Mtawasingizia tu hao raia kutohudhuria, ina maana hao wengine hawajui kuwa gharama za umeme ni kubwa? kwani ukiwa mfanyakazi kwenye shirika huna ndugu wanaotumia umeme! Hebu acheni hoja za KIPUUZI EBO.
 
Back
Top Bottom