TANESCO taabani; EWURA yaomba kupandisha gharama za umeme!


A

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
4,796
Points
2,000
A

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
4,796 2,000
Chanzo: Gazeti la HabariLeo | 11 December, 2012

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeomba kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 81.27 kutoka Sh 196 ya sasa hadi Sh 359 kwa uniti moja ya umeme ili litoe huduma bora za upatikanaji wake.

Jana ilikuwa siku ya wadau na wananchi wa kawaida iliyotengwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kujadili maombi hayo ya TANESCO katika mkutano wa taftishi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Lakini cha ajabu, wananchi ambao wamekuwa wepesi kulalamika juu ya bei hizo mpya, hawakufika kwenye mkutano huo na badala yake ni watendaji wa taasisi mbalimbali na wanahabari ndio waliokuwepo.

Mara ya mwisho, TANESCO ilipandisha gharama za umeme Januari mwaka huu, ikiomba kupandisha bei hizo kwa asilimia 155, kutokana na madai kuwa wanatumia mitambo ya dharura inayogharimu fedha nyingi.

Hata hivyo, EWURA ilipandisha gharama hizo kwa asilimia 40.29, licha ya kuwa bei hiyo ilikuwa iwe kwa miezi sita, EWURA waliongeza muda kutokana na mahitaji ya TANESCO.

Hali hiyo ya wananchi kutofika kwenye mjadala huo, ilimshtua hata Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, ambaye alionesha kusikitishwa na hali hiyo.

Sadiki alisema licha ya matangazo mengi yaliyotolewa ne EWURA kwenye vyombo vya habari, lakini idadi ya wananchi walioitikia mwito huo, ilikuwa ni ndogo mno.

"Wananchi bei zikipandishwa ni wepesi wa kulalamika, lakini walitakiwa wafike leo watoe maoni yao, cha ajabu wameshindwa kufika", alisema kwa masikitiko Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika mkutano huo, wengi walikuwa ni waandishi wa habari, maofisa wa EWURA na TANESCO na wadau kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Bei ya EWURA

Wakati TANESCO inaomba kupandisha kiasi hicho cha bei ya umeme, Mshauri Mwelekezi aliyekodiwa na EWURA baada ya kufanya utafiti na kukokotoa hesabu zake, amependekeza bei ya umeme ipande hadi kufikia Sh 254 kwa uniti moja kiasi ambacho ni asilimia 29.5.

Mtaalamu huyo katika maoni yake, amependekeza kuwa bei ipande kwa Sh 288.39 kwa wateja wa majumbani ambao wako kundi la D1, wateja wa T1 ambao ni wa majumbani na wafanyabiashara ndogo iwe Sh 306.52, wateja wa T2 Sh 167 na wateja wa T3 iwe Sh 134.

Wadau wapinga Wadau wachache ambao walifika kwenye mkutano huo, walipinga maombi hayo ya TANESCO kwa maelezo kuwa shirika hilo halijafanya jitihada za kupanua wigo wake wa mapato, badala yake limekuwa likikimbilia kwa wateja mara inapotokea ongezeko la gharama.

EWURA imetenga siku 14 kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao na wale ambao hawakupata muda wa kufika kwenye mkutano huo, wanaweza kutoa maoni yao na kuyawasilisha EWURA kwa barua au kwa njia yoyote ya mawasiliano kabla ya kuchukua uamuzi wa kupandisha au kutopandisha bei ya umeme.

Bei hiyo mpya inatakiwa ianze kutumika Januari mwakani na kwa hali ilivyo ni wazi kuwa gharama hizo zitaongezeka, kutokana na pendekezo la mshauri huyo pamoja na utetezi wa TANESCO ambao hata hivyo umepingwa na wadau waliofika kwenye mkutano huo kuwa hauna nguvu.

TANESCO taabani

Akitetea hatua hiyo ya kupandisha umeme, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felchesm Mramba, alipinga pendekezo hilo la EWURA ambalo limetolewa na mtaalamu mshauri, kwa maelezo kuwa halikuzingatia hali halisi ya TANESCO ilivyo kwa sasa.

Mramba alisema sababu za TANESCO kuomba kupandisha umeme kwa asilimia 155 mwaka jana, bado ziko pale pale ambazo ni ukame, aliofanya mabwawa ya maji yaendelee kukauka na kuilazimisha TANESCO kutegemea umeme wa mafuta, ambao ni wa kampuni binafsi.

Alisema pia mkopo wa Sh bilioni 408, ambao Serikali ilikuwa iweke dhamana, haukupatikana na kuifanya TANESCO kuendelea kuwa katika hali mbaya ya kifedha.

Alisema licha ya Serikali kutoa ruzuku ya Sh bilioni 136, ambazo awali ilikuwa ni mkopo, lakini bado hali ni mbaya. Alisema licha ya kuwepo kwa mitambo inayotumia maji; lakini hakuna maji.

Pia alisema licha ya kuwepo mitambo ya kutumia gesi ya Ubungo na Tegeta, gesi inayotoka Songosongo kwa sasa, haitoshelezi kuzalisha megawati nyingi za umeme, badala yake uwezo wa mitambo hiyo ya gesi ni megawati 329 tu.

Sh bilioni 32 kwa siku Kwa hali hiyo, alisema watalazimika kuendelea kutumia mitambo ya IPTL kuzalisha megawati 100, ambayo kwa siku TANESCO inatumia Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya mafuta, Agreko megawati 100 sawa na Sh bilioni 1.5 kwa siku kununua mafuta.

Kwa mitambo ya Symbion ambayo inazalisha megawati 160, Mramba alisema fedha zinazotumika kununua mafuta ni Sh bilioni 1.5 kwa siku.

"Gharama zote kwa siku ni Sh bilioni 5.2 kwa ajili ya kununua mafuta peke yake na gharama hizi ni nje ya Sh bilioni 27 ambazo zinalipwa na TANESCO kila siku kama Capacity Charge," alisema Mramba wakati akitetea uamuzi wa kuomba kupandisha gharama za umeme.

Kwa maana hiyo gharama za mafuta na Capacity Charge kwa siku ni Sh bilioni 32. Mramba aliendelea kudai kuwa iwapo bei ya umeme haitapanda, ikifika mwishoni mwa 2013 TANESCO itakuwa na hasara ya Sh bilioni 878,065, kwani gharama za uzalishaji zitakuwa kubwa kuliko mapato.

Alisema kwa sasa uendeshaji wa shirika hilo ni mbaya, hali ambayo imeilazimu Serikali kutoa Sh bilioni 138 kama ruzuku. Pia, alisema hadi kufika Oktoba mwaka huu, TANESCO imelimbikiza deni la Dola za Marekani milioni 250 kutoka kwa wazalishaji wa umeme na wadau wengine, ambao wanaisambazia vifaa mbalimbali.

Lakini, alisema iwapo bei itapanda, mapato ya shirika yatakuwa ni Sh trilioni 2, kiasi ambacho ni sawa na gharama za uzalishaji wa umeme.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchumi wa EWURA Felix Ngamlagosi, alisema bei zilizotolewa na mtaalamu mwelekezi, zimezingatia gharama za usambazaji, uzalishaji na usafirishaji na miundombinu ya TANESCO iliyopo.

 
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
4,260
Points
2,000
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
4,260 2,000
Duh, hii nchi tutakimbia muda si mrefu.
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,609
Points
2,000
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,609 2,000
Kuna haja ya serikali kufikiria kuondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye umeme (kama ilivyo kwa diseli/petroli).
 
Invisible

Invisible

Admin
Joined
Feb 11, 2006
Messages
9,101
Points
2,000
Invisible

Invisible

Admin
Joined Feb 11, 2006
9,101 2,000
Sh bilioni 32 kwa siku Kwa hali hiyo, alisema watalazimika kuendelea kutumia mitambo ya IPTL kuzalisha megawati 100, ambayo kwa siku TANESCO inatumia Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya mafuta, Agreko megawati 100 sawa na Sh bilioni 1.5 kwa siku kununua mafuta.

Kwa mitambo ya Symbion ambayo inazalisha megawati 160, Mramba alisema fedha zinazotumika kununua mafuta ni Sh bilioni 1.5 kwa siku.

"Gharama zote
kwa siku ni Sh bilioni 5.2 kwa ajili ya kununua mafuta peke yake na gharama hizi ni nje ya Sh bilioni 27 ambazo zinalipwa na TANESCO kila siku kama Capacity Charge," alisema Mramba wakati akitetea uamuzi wa kuomba kupandisha gharama za umeme.

Kwa maana hiyo gharama za mafuta na Capacity Charge kwa siku ni Sh bilioni 32. Mramba aliendelea kudai kuwa iwapo bei ya umeme haitapanda, ikifika mwishoni mwa 2013 TANESCO itakuwa na hasara ya Sh bilioni 878,065, kwani gharama za uzalishaji zitakuwa kubwa kuliko mapato.
Tell me this' a joke or some typing errors!

Can't be... Siamini, nadhani kuna makosa sehemu
 
A

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
4,796
Points
2,000
A

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
4,796 2,000
Tell me this' a joke or some typing errors!

Can't be... Siamini, nadhani kuna makosa sehemu
tutakulaje kama hatufanyi hivyo, na zile kofia, kanga, t-shirts hatutoi bure, kuna gharama zake
 
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
6,932
Points
1,500
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
6,932 1,500
(((IPTL megawati 100 = shilingi bilioni 1.4 kwa siku) (+) (Symbion megawati 160 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku) (+) (Agreko megawati 100 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku ))) = Gharama zote kwa siku ni shilingi bilioni 5.2 (????????)
 
Invisible

Invisible

Admin
Joined
Feb 11, 2006
Messages
9,101
Points
2,000
Invisible

Invisible

Admin
Joined Feb 11, 2006
9,101 2,000
tutakulaje kama hatufanyi hivyo, na zile kofia, kanga, t-shirts hatutoi bure, kuna gharama zake
Mkuu,

Are you serious hizi figures ni sahihi? Unajua inauma sana? Ni figures za SIKU MOJA? Seriously?
 
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
6,932
Points
1,500
Baba_Enock

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
6,932 1,500
Waziri wa Nishati (le Professeur - SOS-Peter Muhongo) balisema kuwa hakutakuwa na mgao wa umeme...!
 
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,478
Points
1,195
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,478 1,195
Hata mimi ni mdau, siwezi enda kwenye huo mkutano kwa sababu hata bei za sasa ziko juu sana ya uwezo wa kimaslahi.

Sasa kujadili kitu ambacho huna uwezo nacho ni sawa na kupoteza muda tu. Bora kusubiri hukumu tu kama ni kunyongwa acha tufe.
 
A

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Messages
4,796
Points
2,000
A

August

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2007
4,796 2,000
tunafanya mpango wa kuuza shares/kubinafsisha shrika ili tulete ufanisi, sasa lazima wanunuaji au wawekezaji tuwape uwezo
 
Tamatheo

Tamatheo

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Messages
3,287
Points
1,500
Tamatheo

Tamatheo

JF-Expert Member
Joined May 28, 2012
3,287 1,500
(((IPTL megawati 100 = shilingi bilioni 1.4 kwa siku) (+) (Symbion megawati 160 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku) (+) (Agreko megawati 100 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku ))) = Gharama zote kwa siku ni shilingi bilioni 5.2 (????????)
Nchi ya Kusadikika, ukiongea sana utajikuta Mabwepande, ngoja nisepe mimi sio Uli......
 
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,003
Points
1,500
K

Kishalu

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,003 1,500
(((IPTL megawati 100 = shilingi bilioni 1.4 kwa siku) (+) (Symbion megawati 160 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku) (+) (Agreko megawati 100 = shilingi bilioni 1.5 kwa siku ))) = Gharama zote kwa siku ni shilingi bilioni 5.2 (????????)
1.4+1.5+1.5= 4.4
 
Invisible

Invisible

Admin
Joined
Feb 11, 2006
Messages
9,101
Points
2,000
Invisible

Invisible

Admin
Joined Feb 11, 2006
9,101 2,000
Vicent daudi

Vicent daudi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2012
Messages
353
Points
195
Vicent daudi

Vicent daudi

JF-Expert Member
Joined Dec 9, 2012
353 195
Nafikiri viongoz makin wametutoa pale waliposema, chama chenye kujinadi kitamaliza matatizo ndio kinaleta matatizo viongozi wanaodaiwa kuwa na elimu za juu walizopata kwa upendeleo ndio wameshindwa kuangalia future ya tanzania, km alivyoacha nyerere, juzi walisema pesa hazitoshi kuendesha shirika wakaongeza bei ya unit miez michache tu wanataka kuongeza tena, kutukomoa na hazitatosha miezi miwili tena wataongeza
 
adakiss23

adakiss23

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Messages
3,382
Points
2,000
adakiss23

adakiss23

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2011
3,382 2,000
Deni la Dowans linazidi kukua wat u expect?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,156
Points
2,000
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,156 2,000
Hapo matumizi ya KAWAIDA hayajaainishwa!

Kwani nijuavyo ni kuwa matumizi yasiyoandikika hukaribia nusu kama si robo tatu ya matumizi jumla ya serikali na mashirika yake,mbona fungu la chai halijawekwa hapo? Mimi ningependekeza Unit moja ya umeme iwe angalau Tsh 1000/ ili iende sambamba na bei za sukari na mchele!!

Aaaagh hasira mpaka zinapitiliza! Halafu baadhi yenu mnaimba ccm yajenga nchi!! Muna ubongo kweli? Au mmejaza matambara kichwani?
 
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
7,005
Points
2,000
eliakeem

eliakeem

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
7,005 2,000
"Gharama zote kwa siku ni Sh bilioni 5.2 kwa ajili ya kununua mafuta peke yake na gharama hizi ni nje ya Sh bilioni 27 ambazo zinalipwa na TANESCO kila siku kama Capacity Charge," alisema Mramba wakati akitetea uamuzi wa kuomba kupandisha gharama za umeme.
Vitu ambavyo mimi binafsi sijavielewa na pia sikubaliani navyo...
1) Gharama ya kununua mafuta kwa nini IBEBWE NA TANESCO?
2) Gharama ya kununua vipuri kwanini iwe ya TANESCO?
3) Capacity Charge maana yake ni nini????
4) Kwa nini capacity charge inazidi gharama za kununua mafuta?
5) Ni nini jukumu la huyu anayeiuzia umeme TANESCO?
6) Kwa nini mitambo isibadilishwe itumie gesi ya asili?
7) Tanesco inawezaje kujiendesha wakati ifikapo mwishoni mwa mwaka 2013 itakuwa imepata hasara ya Sh Bilioni 878,065??? (binafsi tarakimu kama hii sijawahi iona na sijui inamaanisha nini, pengine kuna makosa ya uchapaji!!!)

Ninayo mengi moyoni kuhusu TANESCO, lakini kwa leo acha niishie hapa!!!!!

Hawa waliotuingiza kwenye mikataba ya aina hii wao WANACHEKELEA halafu SISI TUNALIA lakini kuna KIPINDI WATAYALIPA HAYA MACHOZI TUNAYOLIA..... NA HIYO ITAKUWA MBAYA MAANA ....ITAKUWA KILIO NA KUSAGA MENO..

 
W

wakubaha

Member
Joined
Nov 17, 2008
Messages
99
Points
70
W

wakubaha

Member
Joined Nov 17, 2008
99 70
Naomba kuuliza wataalamu wa mambo ya MAFUTA...
BILIONI 1.5 NI SAWA NA LITA NGAPI YA MAFUTA MAZITO?
NA MITAMBO INATUMIA LITA NGAPI KWA SAA?
Huu ni wendawazimu...maana TANESCO lingekuwa ni Shirika kama ATCL au KIWANDA cha UMA lingeshakufa zamani sana...hiyo hela wanayotaka kupandisha leo baada ya MWAKA watasema haitoshi...IKO WAPI MIPANGO???
 
mkandaboy

mkandaboy

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Messages
250
Points
225
mkandaboy

mkandaboy

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2012
250 225
tutakulaje kama hatufanyi hivyo, na zile kofia, kanga, t-shirts hatutoi bure, kuna gharama zake
....Yaa its true August, na ukizingatia 2015 imekaribia, ni lazima tuanze kukusanya fedha za kampeni.. Aahh bongooo.........
 

Forum statistics

Threads 1,283,665
Members 493,764
Posts 30,796,152
Top