TANESCO taabani; EWURA yaomba kupandisha gharama za umeme!

Yani kupanda kwa gharama za umeme ndo wanazidi kutuongezea mzigo wa maisha ss makabwela maisha yamekuwa magumu jamani kwanini lakini kila kukicha shida ndo zinaongezeka
 
From IPP MEDIA

Based on that figure, it implies that Tanesco needs Sh3.036 trillion ($1.89 billion) per annum, which exceeds 20 percent of the current country’s annual budget of Sh15.1trillion (for the 2012/13 fiscal year).

The exorbitant costs of generating electricity is rooted in the privately owned diesel and Heavy Fuel Oil (HFO) powered plants located in Dar es Salaam, Dodoma and Arusha, consuming Sh42 billion monthly in capacity charges -- which is nearly 50 percent of Tanesco’s total monthly revenue
Capacity charge is money paid to the owner of the power generating plant regardless of the operation of that plant, which means the money accumulates every month and has to be paid even if the plants were to switch off.
These costs do not include the price tag for buying power from the same independent power producers – while the so-called capacity charges still have to be paid whether Tanesco consumes electricity or not.
The financially troubled Tanesco is now asking for the 81.27 percents increase in power tariffs -- or risk bankruptcy.

How can you pay a business for doing nothing!!! this is the first time in my life I see this type of wizi wow!
 
This is so strange..i always wonder how come legal officers allow such a contract to be signed..in a way, at the end of the day, people are the one who are paying these extra costs..
 
Hiyo pesa ya Capacity Charges ni kwanini wasingenunua Generators zao. Je ukifanya business na Tanesco una risk gani kama unalipwa kwa kutokufanya kazi!!!
 
Halafu watu walioshiriki kuingia mikataba kama hii ya kulipia capacity charge kwa siku ndo kwanza ndo wanafanya kampeni za _Raisi 2015 na kuna watu humu JF wanawapigia debe! Wanadhani wananchi wanaweza kuisahau richmond kiurahisi namana hii wakati leo hii bado inaendelea kukwapua capacity charge kwa kujibadilisha jina! Wajinga ndo tuliwao nani anajua kuwa huyu jamaa hayumo kwenye hili jina jipya na anaendelea kupata mgao wake ambao ndo unaendelea kumpa kiburi cha kugombea Urais kwa kujiamini kuwa atatumia umasikini na ujinga wa watanzania kuwahonga 2015!

Najua hatuna la kufanya sisi kama wanyonge lakini tunaweza kumwambia Mungu kilio hiki na atalihurumia taifa hili! Kama alisikia mateso ya wanawaisiraeli kule utumwani Misiri atasikia hata ya wanyonge wa Tanzania wamekuwa ni mtaji wa watu wachache wanaoishi maisha ya kifahari wao na familiya zao ilihali mnyonge hana hata mlo mmoja kwa siku!

Ni watanzania wanagapi wanaweza kununua umeme kwa bei hii inayopendekezwa na Tanesco? Kwa pendekezo hili ina maana masikini anayetumia unit 50 kwa mwezi ni lazima sasa awe n angalau Tsh.15000 kitu amabacho nakishuhudia huku mtaani kwangu watu wamerudisha line za maji za dawasco ambazo gharama zake kwa mwezi si zaidi ya Tsh 12000. Kama maji ni muhimu zaidi kuliko umeme waliamua kuachana na dawasco je hili la umeme itakuwaje? Nadhani wanachi wataamua kutumia mishumaa sasa maana koroboi mafuta ya taa bei yake juu kuliko hata ya magari!
 
Capacity charge ya symbion nadhani bado inagawanwa na walewale watu wa Richmond ila kwa kuwa wanatzania tumelogwa kuna baadhi yetu tunawaza eti jamaa ndo anafaa kuwa Raisi tena 2015! CCM tena ???????? Mungu siyo maganga atasikia kilio cha wanyonge katika hili!
 
EWURA wanaishi kwa asilimia za TANESCO. Wakiongeza pato la TANESCO, ni kuongeza pato lao!

Utaratibu gani huuuuuuu!
 
CCM is a monster a blood sucker. Waswahili husema ukicheka na nyani utavuna
Mabua Richmond ni ya CCM ndio maana wameruhusu ibadilishe jina kuwa Dowans na Leo wanaitwa Dowans na Pacha wake Aggreko.

Hapakufanyika zabuni yoyote Mwaka Jana wakati Symbion inazaliwa. Tumeingizwa mkenge! Watu wazima wanaongea uongo. Haiwezekani kununua Umeme kwa wastani wa Shilingi Mia Nane( 800/=) na kuuza kwa Shilingi 221/= halafu hajasema utafidia vipi Hilo pengo? Utaendlea na ujuha wa kuzalisha hasara kila siku. Naishiwa maneno ya kuelezea.
Marehemu Dowans bado anadai lbilioni 100 na ushee lakini mrithi wake Symbion kapewa zabuni yenye bei ya umeme kubwa kuliko sehemu yoyote katika hii sayari inayoitwa Dunia.

Wajinga ndio waliwao. Hii mikataba ya Kukodi umeme wa dharura ni kichaa tu anayeweza kuafiki.
 
Mathematics: According to this chart: Approximate Diesel Generator Fuel Consumption Chart
Generator Size (kW)1/4 Load (gal/hr)1/2 Load (gal/hr)3/4 Load (gal/hr)Full Load (gal/hr)
200.60.91.31.6
301.31.82.42.9
401.62.33.24.0
601.82.93.84.8
752.43.44.66.1
1002.64.15.87.4
1253.15.07.19.1
1353.35.47.69.8
1503.65.98.410.9
1754.16.89.712.7
2004.77.711.014.4
2305.38.812.516.6
2505.79.513.618.0
3006.811.316.121.5
3507.913.118.725.1
4008.914.921.328.6
50011.018.526.435.7
60013.222.031.542.8
75016.327.439.353.4
100021.636.452.171.1
125026.945.365.088.8
150032.254.377.8106.5
175037.563.290.7124.2
200042.872.2103.5141.9
225048.181.1116.4159.6

Assumption:
Tanesco generators run at full load , 24 hours, and they are large enough to consume 159.6 gallons in an hour. So they consume approx. 160gallons per hour to generate 2.25MW.
Therefore to generate 100MW in an hour we need about 7,111 gallons. For full day we need170,667 gallons. Now one gallon is about 3.78 litres; which gives 646,827 litres in a day. Assuming I litre on diesel is TZS 2,000 ; we then need to have TZS 1,293,653,333; approx. TZS 1.3 Billion to run those damn machines.

So with these simple calculations, I understand, if the man say they pay 1.4Billion in day to have 100MW but if this is business to business why should one pay for your production costs and still pay you per unit and still pay the damn thing called capacity charge??? The bottom line is MIKATABA MIBOVU na kukosa ubunifu wa kibiashara, matumizi makubwa, over employment (wengine wanashinda wanasoma magazeti ofisini)!!!!!
 
Waachwe Tanesco waongeze bei january waliomba waongeZe kwa asilimia 155 lakini wakapewa asimia 40 sasa hapo tutegemee nini? Kwanza le profeseri anasema kwani hela wanazokusanya wanapeleka wapi anajifanya hajui zinakokwenda. Waache kutufanya watoto chanzo cha matatizo yote ni mafisadi wa Chama twawala.
 
... TANESCO is the worst company in Tz, kimechangia umaskini kwa zaidi ya 40% ya umaskini wa nchi sasa,

TANESCO ikiachwa iendelee inavyofanya.... maisha ya wananchi yataharibika kabisa, bidhaa kupanda bei, viwanda uwekezaji kuzorota hivyo kupunguza ajira, ajira binafsi ndogondogo nyingi zinategemea umeme kuzorota...

SERIKALI..... ndio haijachukua seriously TANESCO.... so hali itakuwa mbaya saana 2013
 
Waachwe Tanesco waongeze bei january waliomba waongeZe kwa asilimia 155 lakini wakapewa asimia 40 sasa hapo tutegemee nini? Kwanza le profeseri anasema kwani hela wanazokusanya wanapeleka wapi anajifanya hajui zinakokwenda. Waache kutufanya watoto chanzo cha matatizo yote ni mafisadi wa Chama twawala.

Shangaa na wewe! Hata haiingii akilini. Waziri hajui wapi pesa inapelekwa! Hata malipo ya capacity charge hajui. Nani sasa anajue kuhusu makusanyo ya TANESCO na matumizi ya fedha?
 
Tanesco hata wapewe Pesa zote Za Dunia Hii Lakini Umeme Utabaki Kuwa Wa Mashaka Ina Maana Hii Nchi imeshindwa Kuondoa Tatzo La Umeme Kwa Hali Hii Basi Hatuna Viongozi Jaman Tutabaki Tunanyonywa Mpaka Basi Kila Siku Watapandisha Bei Huduma Bora Hakuna Umeme Wa Mashaka

TANZANIA INATIA AIBU JAMANI
 
LICHA ya viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wale wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO), kujaribu kuficha ukweli kuhusu hali ya uzalishaji na usambazaji wa umeme wa uhakika nchini, Tanzania Daima imedokezwa kuwa hali ni tete.

Kutokana na mkakati wa wizara husika ulivyo sasa, inaelezwa kuwa ili mgawo wa umeme utoweke, kiasi cha sh bilioni 42 zitapaswa kutumika kila mwezi kwa ajili ya kuyalipa makampuni yanayoiuzia TANESCO umeme.

Kwa muda mrefu sasa TANESCO imeelezwa kuwa hoi kifedha licha ya kuwa na makusanyo makubwa lakini fedha hizo zimekuwa zikiishia mikononi mwa mafisadi na hivyo shirika hilo kubakia tegemezi kwa serikali.

Kwa mujibu wa takwimu za Waziri wa Naishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, alizozitoa bungeni wakati akihitimisha hoja ya hotuba ya bajeti yake kwa mwaka 2012/2013, TANESCO inakusanya mapato kati ya sh bilioni 60 mpaka 70 kwa mwezi.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza, licha ya matumizi ya shirika hilo kuwa sh bilioni 11 kwa mwezi, Waziri alishindwa kufafanua ni wapi zinakwenda sh takribani bilioni 40 zinazosalia.

Waziri Muhongo alilieleza Bunge upotevu huo wa mabilioni bila kufafanua Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), wamefanya nini kama fedha hizo zinaibiwa.

Wakati hali ikiwa hivyo, Muhongo amenukuliwa akikanusha kuwa hakuna mgawo wowote wa umeme kwa sababu TANESCO imejipanga kutafuta vyanzo vingine vya kuzalisha umeme wa uhakika.

Alisema suala la umeme kukatika kwa dakika mbili au tatu si mgawo bali ni kutokana na miundombinu ambayo imechakaa.

Kauli ya waziri haipishani na ile ya naibu wake, George Simbachawene, ambaye alizungumza na gazeti hili jana akisema wanachodhibiti sasa ni uzalishaji wa umeme ili umeme uwepo.

Alipobanwa afafanue ni kwa nini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara maeneo tofauti nchini, naye aliungana na waziri wake kusisitiza kuwa ni ubovu wa miundombinu na kwamba huo si mgawo.

Tanzania Daima ilitaka kufahamu miundombinu hiyo itaimarika lini wakati TANESCO iko hoi kifedha kutokana na kuelemewa na madeni ya makampuni yanayoliuzia umeme, lakini naibu waziri alijitetea akisema kuwa kazi yao kama wizara sasa ni kuhakikisha umeme upo.

Licha ya wizara kujaribu kukwepa, gazeti hili limedokezwa kuwa katika kila sh 100 ambazo TANESCO inakusanya, sh 86 zinakwenda kulipa madeni ya mikataba iliyosainiwa kifisadi ya Aggreko, Symbion, Songas na IPTL. (Waliosaini mikataba hii ya kifisadi ni wahujumu uchumi sijui kwanini hawashughulikiwi...Ooops! nilisahau kumbe tuna DHAIFU!!!!)

Kwa mujibu wa chanzo chetu ni kwamba mpaka sasa Symbion inalipwa sh milioni 152 kila siku kama gharama za uendeshaji wakati IPTL inalipwa sh bilioni tatu kila mwezi na Songas sh bilioni 4.5.

"Agrreko wanaiuzia TANESCO umeme kwa senti dola 42 kwa unit moja halafu TANESCO inauza umeme huo kwa sentidola 11 kwa unit moja," kilisema chanzo chetu. (Tofauti ya senti dola 31 kwa unit moja!!!! Wacha TANESCO ijifie)

Serikali hii ambayo inababaika sasa kuhusu upatikanaji wa uhakika, ilikataa ushauri wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), wa kuinunua mitambo ya Dowans wakati huo ikiuzwa kwa dola milioni 59 kwa madai kuwa sheria ya manunuzi ya umma inakataza.

Lakini mitambo hiyohiyo ilinunuliwa baadaye na Symbion kwa dola milioni 159 na sasa kampuni hiyo inazalisha umeme na kuiuzia TANESCO.

Akizungumzia sakata hilo, Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, alisema kuwa kauli ya waziri na wasaidizi wake haielezi ukweli kamili kuhusu hali tete ya umeme kutokana na kususua katika utekelezaji wa Mpango wa Dharura wa Umeme kama nilivyohoji bungeni Julai 27, 2012.

"Kwa mujibu wa nyaraka nilizonazo za ndani ya Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO hali ya uzalishaji na usafirishaji na usambazaji wa umeme bado ni tete kwa sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa upatikanaji wa mafuta na gesi asili kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya kufua umeme," alisema.

Alisema kuwa serikali ina upungufu ya fedha za kununua mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya umeme, hivyo inapaswa kurejea katika mapendekezo yake aliyoyatoa bungeni Agosti 2011.

"TANESCO inakabiliwa na ufisadi na uzembe unaoongeza gharama za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme kwa upande mmoja na uendeshaji wa shirika kwa upande mwingine.

"Ufisadi na uzembe huo unapunguza uwezo wa TANESCO kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na unaongeza gharama na bei ya upatikanaji wa umeme hali inayoathiri uchumi wa nchi na maisha ya wananchi," alisema.

Aliongeza kuwa kwa sasa nchi haina Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambapo wizara ingelazimika kueleza ukweli kamili na halisi, hivyo amtaka Spika arejee barua yake hiyo na atumie madaraka na mamlaka yake kwa mujibu wa kanuni ya 116 na kanuni ya 114 fasili ya 14 kukabidhi suala hilo lishughulikiwe na kamati nyingine.

"Nitakabidhi sehemu ya nyaraka nilizonazo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge itakayoelekezwa na Spika kushughulikia jambo hili lakini iwapo hatua za haraka hazitachuliwa mpaka Januari 30, 2013 nitatoa baadhi ya nyaraka hizo kwa vyombo vya habari na umma," alisema.

CHANZO: Tanzania Daima
 
... TANESCO is the worst company in Tz, kimechangia umaskini kwa zaidi ya 40% ya umaskini wa nchi sasa,

TANESCO ikiachwa iendelee inavyofanya.... maisha ya wananchi yataharibika kabisa, bidhaa kupanda bei, viwanda uwekezaji kuzorota hivyo kupunguza ajira, ajira binafsi ndogondogo nyingi zinategemea umeme kuzorota...

SERIKALI..... ndio haijachukua seriously TANESCO.... so hali itakuwa mbaya saana 2013

natamani kujiunga na jeshi halafu nipande vyeo haraka haraka hadi ukuu wa majeshi.....aaargh!
 
hii bei uliyosema imeombwa na tanesko ipande mbona tumeshaanza kuitumia tangu mwaka juzi... unit moja ilikuwa ni sawa na shs:350/= ila nilichomsikiliza MKURUGENZI WA TANESCO ameeleza kuwa ameiomba EWURA kuridhia mabadiliko ya gharama tulizokuwa tunatozwa kutoka kulipia service charg, ewura charg, tra nk hizi ziondolewe na pia gharama zishushwe kwa kiwango cha 1.8% ya matumizi kwa watumiaji wa majumbani tu. UPOOOO HAPO? acha kuropoka kama umelishwa LIMAO.
Chanzo: Gazeti la HabariLeo | 11 December, 2012

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeomba kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 81.27 kutoka Sh 196 ya sasa hadi Sh 359 kwa uniti moja ya umeme ili litoe huduma bora za upatikanaji wake.

Jana ilikuwa siku ya wadau na wananchi wa kawaida iliyotengwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kujadili maombi hayo ya TANESCO katika mkutano wa taftishi, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Lakini cha ajabu, wananchi ambao wamekuwa wepesi kulalamika juu ya bei hizo mpya, hawakufika kwenye mkutano huo na badala yake ni watendaji wa taasisi mbalimbali na wanahabari ndio waliokuwepo.

Mara ya mwisho, TANESCO ilipandisha gharama za umeme Januari mwaka huu, ikiomba kupandisha bei hizo kwa asilimia 155, kutokana na madai kuwa wanatumia mitambo ya dharura inayogharimu fedha nyingi.

Hata hivyo, EWURA ilipandisha gharama hizo kwa asilimia 40.29, licha ya kuwa bei hiyo ilikuwa iwe kwa miezi sita, EWURA waliongeza muda kutokana na mahitaji ya TANESCO.

Hali hiyo ya wananchi kutofika kwenye mjadala huo, ilimshtua hata Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, ambaye alionesha kusikitishwa na hali hiyo.

Sadiki alisema licha ya matangazo mengi yaliyotolewa ne EWURA kwenye vyombo vya habari, lakini idadi ya wananchi walioitikia mwito huo, ilikuwa ni ndogo mno.

&[HASHTAG]#8220[/HASHTAG];Wananchi bei zikipandishwa ni wepesi wa kulalamika, lakini walitakiwa wafike leo watoe maoni yao, cha ajabu wameshindwa kufika&[HASHTAG]#8221[/HASHTAG];, alisema kwa masikitiko Mkuu huyo wa Mkoa.

Katika mkutano huo, wengi walikuwa ni waandishi wa habari, maofisa wa EWURA na TANESCO na wadau kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Bei ya EWURA

Wakati TANESCO inaomba kupandisha kiasi hicho cha bei ya umeme, Mshauri Mwelekezi aliyekodiwa na EWURA baada ya kufanya utafiti na kukokotoa hesabu zake, amependekeza bei ya umeme ipande hadi kufikia Sh 254 kwa uniti moja kiasi ambacho ni asilimia 29.5.

Mtaalamu huyo katika maoni yake, amependekeza kuwa bei ipande kwa Sh 288.39 kwa wateja wa majumbani ambao wako kundi la D1, wateja wa T1 ambao ni wa majumbani na wafanyabiashara ndogo iwe Sh 306.52, wateja wa T2 Sh 167 na wateja wa T3 iwe Sh 134.

Wadau wapinga Wadau wachache ambao walifika kwenye mkutano huo, walipinga maombi hayo ya TANESCO kwa maelezo kuwa shirika hilo halijafanya jitihada za kupanua wigo wake wa mapato, badala yake limekuwa likikimbilia kwa wateja mara inapotokea ongezeko la gharama.

EWURA imetenga siku 14 kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao na wale ambao hawakupata muda wa kufika kwenye mkutano huo, wanaweza kutoa maoni yao na kuyawasilisha EWURA kwa barua au kwa njia yoyote ya mawasiliano kabla ya kuchukua uamuzi wa kupandisha au kutopandisha bei ya umeme.

Bei hiyo mpya inatakiwa ianze kutumika Januari mwakani na kwa hali ilivyo ni wazi kuwa gharama hizo zitaongezeka, kutokana na pendekezo la mshauri huyo pamoja na utetezi wa TANESCO ambao hata hivyo umepingwa na wadau waliofika kwenye mkutano huo kuwa hauna nguvu.

TANESCO taabani

Akitetea hatua hiyo ya kupandisha umeme, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felchesm Mramba, alipinga pendekezo hilo la EWURA ambalo limetolewa na mtaalamu mshauri, kwa maelezo kuwa halikuzingatia hali halisi ya TANESCO ilivyo kwa sasa.

Mramba alisema sababu za TANESCO kuomba kupandisha umeme kwa asilimia 155 mwaka jana, bado ziko pale pale ambazo ni ukame, aliofanya mabwawa ya maji yaendelee kukauka na kuilazimisha TANESCO kutegemea umeme wa mafuta, ambao ni wa kampuni binafsi.

Alisema pia mkopo wa Sh bilioni 408, ambao Serikali ilikuwa iweke dhamana, haukupatikana na kuifanya TANESCO kuendelea kuwa katika hali mbaya ya kifedha.

Alisema licha ya Serikali kutoa ruzuku ya Sh bilioni 136, ambazo awali ilikuwa ni mkopo, lakini bado hali ni mbaya. Alisema licha ya kuwepo kwa mitambo inayotumia maji; lakini hakuna maji.

Pia alisema licha ya kuwepo mitambo ya kutumia gesi ya Ubungo na Tegeta, gesi inayotoka Songosongo kwa sasa, haitoshelezi kuzalisha megawati nyingi za umeme, badala yake uwezo wa mitambo hiyo ya gesi ni megawati 329 tu.

Sh bilioni 32 kwa siku Kwa hali hiyo, alisema watalazimika kuendelea kutumia mitambo ya IPTL kuzalisha megawati 100, ambayo kwa siku TANESCO inatumia Sh bilioni 1.4 kwa ajili ya mafuta, Agreko megawati 100 sawa na Sh bilioni 1.5 kwa siku kununua mafuta.

Kwa mitambo ya Symbion ambayo inazalisha megawati 160, Mramba alisema fedha zinazotumika kununua mafuta ni Sh bilioni 1.5 kwa siku.

&[HASHTAG]#8220[/HASHTAG];Gharama zote kwa siku ni Sh bilioni 5.2 kwa ajili ya kununua mafuta peke yake na gharama hizi ni nje ya Sh bilioni 27 ambazo zinalipwa na TANESCO kila siku kama Capacity Charge,&[HASHTAG]#8221[/HASHTAG]; alisema Mramba wakati akitetea uamuzi wa kuomba kupandisha gharama za umeme.

Kwa maana hiyo gharama za mafuta na Capacity Charge kwa siku ni Sh bilioni 32. Mramba aliendelea kudai kuwa iwapo bei ya umeme haitapanda, ikifika mwishoni mwa 2013 TANESCO itakuwa na hasara ya Sh bilioni 878,065, kwani gharama za uzalishaji zitakuwa kubwa kuliko mapato.

Alisema kwa sasa uendeshaji wa shirika hilo ni mbaya, hali ambayo imeilazimu Serikali kutoa Sh bilioni 138 kama ruzuku. Pia, alisema hadi kufika Oktoba mwaka huu, TANESCO imelimbikiza deni la Dola za Marekani milioni 250 kutoka kwa wazalishaji wa umeme na wadau wengine, ambao wanaisambazia vifaa mbalimbali.

Lakini, alisema iwapo bei itapanda, mapato ya shirika yatakuwa ni Sh trilioni 2, kiasi ambacho ni sawa na gharama za uzalishaji wa umeme.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchumi wa EWURA Felix Ngamlagosi, alisema bei zilizotolewa na mtaalamu mwelekezi, zimezingatia gharama za usambazaji, uzalishaji na usafirishaji na miundombinu ya TANESCO iliyopo.

 
Back
Top Bottom