TANESCO Shinyanga wanawahujumu wananchi waliolipia gharama za kuunganishiwa umeme, Waziri Kalemani tusaidie...

FCR

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
213
177
Ikumbukwe kwamba Waziri wa Nishati Dr. Kalemani anafanya ziara katika mikoa mbalimbali kuangalia utekelezaji mbalimbali wa miradi ya umeme lakini hata hivyo pamoja na kumuona kwenye vyombo mbalimbali akikemea watendaji wake kutowajibika ipasavyo, hapa Shinyanga wakazi zaidi ya 90 ndani ya manispaa ya Shinyanga hawajapata umeme pamoja kwamba wamelipa gharama zote za kuweza kuwekewa umeme!

Waziri njoo hapa Shinyanga watendaji wako wamelala usingizi wa pono kila siku hutuma meseji kwa wateja kwamba hawana nguzo za umeme huku wakiwa wameshalipa gharama zote ikiwa ni pamoja na nguzo hizo.

Yapata miezi zaidi ya saba sasa hawajui hatima yao! Hapa Cha kujiuliza hizo nguzo zinatoka nje ya Tanzania na kama ni nje ya Tanzania kwanini mteja hudanganywa kulipia gharama hizo huku akiambiwa baada ya siku tisini anawekewa umeme?

Au nguzo zipo watendaji wako kama misemo ya kitanzania wanataka kitu kidogo?

Taarifa hii nimeipata kwa watu mbalimbali ambao wana meseji hizo za malipo ya TANESCO hata hivyo nilienda mbali zaidi kuulizia baadhi ya wahusika wa shirika hilo wakaniambia ni jambo la kawaida akadai kwamba wapo ambao hukaa hadi mwaka bila kuunganishiwa umeme.

Binafsi nasikitika Sana kuona haya yakitendeka katika utawala huu ambao hauwezi kumuonea huruma mfanyakazi ambaye anashindwa kuwahudumia wananchi ipasavyo.
 
Lazima kuwepo na mfumo, waziri kama yeye hawezi kufika kila sehemu hiyo ni njia yakijinga katika watendaji wakazi za umma.
 
Back
Top Bottom