Tanesco ni wezi au wameniibia mimi tuu

hapa.mimi

Member
Joined
Mar 11, 2010
Posts
11
Reaction score
0
Wakuu nna hasira na TANESCO

Jana nilipitia kununua LUKU maala fulani, nilinunua umeme wa 10,000/- lakini ajabu risit ilionesha kuwa nimestahili umeme wa 5,800/- tu ambazo ni kama forty something units hivi. Sikuelewa kabisa nikajaribu kupitia kale ka-riceipt chao ndo lah!! nakutana na Vat 18% EwURA 2%, 1% sijui nini wamekula kama 2,600/- hivi, then another line fixed costs kaa 2000++, line number three imejirudia tena vat blaha blah wakakata kama 500 hivi.
Ndugu zangu hivi hawa TANESCO wako wako vizuri akilini kweli na huyu JK kweli anastahili kura zetu?
 
hapo kaka iko na uchangiaji wa kampeni za kikwete so lazima watu tulipie gharama zote...atasema nn sasa?Bongo ya Wadanganyika hiyo mkuu...2010 kikwete oyeeeeeeeeeeeeeeee
 
Yaani hapo umenigusa mie huwa siwaelewi kabisa tanesco kwenye luku, tena angalia vizuri ukinunua mwisho wa mwezi ndo wanakata na service charge ni kubwa mno mpaka utashangaa. We angalia vizuri kila ukinunu luku ni wezi bwana hawa hawana lolote
 


Mkuu hujaibiwa hata senti, nadhani ni kutojua vizuri makato yanavyokwenda, 18% ni VAT, 3% ni REA (Umeme vijijini) na 1% ni EWURA, pia unalipia service charges, kama mwezi uliopita hukununua umeme basi umekatwa service charges ya miezi 2. Hujaibiwa ni makato kisheria. KWA TAARIFA TANESCO WAMEPELEKA OMBI EWURA ILI KUONGEZA UMEME BY 35% tembelea website ya EWURA, download ombi la Tanesco soma na utoe maoni usisubiri wapitishe uje kulalamika JF.
 
Sijalalamika hata wakipandisha 50% haina shida . Shida yangu ni haya makato mara umeme kijijini mara ewura mara REA. Hivi tunaposema unalipia kodi maana yake ni nini? Sio ndio za kuchangia umeme kijijini, ewura, service charge, kikwete campaign etc?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…